Flashback January 3, 2008: Mama Lucy Mwandosya akiwa na yatima wa Lufilyo anaowasaidia. Ujumbe wake ulikuwa huu chini...
" Happy New year.Check hayo maisha ya watoto wengi huko Lufilyo, Tukuyu, Wilayani Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Ndio maisha taharishi! Naomba wadau wako wanisaidie niweze kuwajengea angalau nymba ya matofali mabichi masikini yatima hawa".
LUCY' S HOPE CENTRE FOR ORPHANS
P.O.BOX 5511,
DAR ES SALAAM
ama P.O.BOX 260,
TUKUYU
Yatima hao nje ya kibanda chao
Kibanda cha yatima Lufilyo
Fast Forward to 2012: Hatimaye juhudi za Mama Lucy Mwandosya zimezaa matunda na ndoto yake ya kuwahifadhi yatima hao imetimia kwa msaada wa wafadhili pamoja na wasamaria wema
Mama Lucy Mwandosya akikabidhi mahitji muhimu kwa yatima hao na babu yao. Globu ya Jamii inatoa pongezi kwa Mama Lucy Mwandosya kwa moyo wa huruma na juhudi zake kuwakomboa yatima.
Mwenyezi Mungu akuzidishie mama Lucy,umefanya jambo la maana mno hapa ulimwenguni na katika Akhera yako,,,Roho imeniuma sana sana,,ila tu baada ya kuona hiyo nyumba mpya nimepata unafuu kidogo,lakini bado naumia kwa watoto wengine masikini huko vijijini wanateseka kama hao au na zaidi...Nimesoma habari ya nyuma Rais akizungumza watu wanaojifanya kuwa na vituo vya kulelea yatima au kutunza walioathirika,huwa wanajaza matumbo yao wenyewe bila kuwafikishia walengwa msaada huwo..Jamani watu hatuogopi Mungu kabisaaaa!Yaani mtu jifikirie nani aliyekuumba wewe na akakuwezesha kuwa na nafasi kama hiyo,,na nani aliyewaumba hao mpaka akawanyima hiyo nafasii!Ukilijuwa hilo na ukakumbuka wote tulizaliwa na wote tutakufa,,utakoma kula riziq za yatima,,na ukisikia msaada kama huwo unahitajika haraka utasaidia,,,mfano ni huyo Mama Lucy Shukrani sana Mama!!!!Ahlam ,,,UK
ReplyDeleteMama Mwandosya Mungu akubariki kwa bidii zako kusaidia hawa Malaika wa Mungu! Natamani ningejua hili ningechangia japo kidogo, lakini tutasaidiana!
ReplyDeleteShukran,
Storming
Hawa ndio watu wanahitaji zawadi za kijamii, watu na matumbo yao wanazurura mjini wanajifanya kufungua center za kulelea yatima ila mwisho wa siku wanafaidika wao na familia zao, hongera sana Mama Lucy, mungu akupe maisha marefu ili uweze kuwasiaida wengine, tupo pamoja na nipo tayari kusaidia kama itawezekana, just email me via kitutujr@gmail.com
ReplyDeleteMama hongera sana, hii nyumba mpya inagharimu kiasi gani ili tuwezi kuchangia?
ReplyDeleteHongera sana Mama....hili ni swala zuri sana!
ReplyDeleteINAWIWA SHUKRANI NYINGI KWAKO NA KWA MUNGU KWA MICHANGO YAKO YA HALI NA MALI ILI KUFANIKISHA UJENZI WA NYUMBA KUPITIA KWAKO. MUNGU WETU TUNAMTEGEMEA DAIMA NDIO AMETUWEZESHA KUFANIKISHA HILO. BASI NASI TUNAMRUDISHIA MUNGU SIFA, UTUKUFU NA SHUKRANI KWA KUKUWEZESHA! ZAIDI SANA TUNAKUOMBEA MUNGU AKUZIDISHIE MARA DUFU KATIKA HAZINA YAKO DUNIANI NA MBINGUNI KWA MOYO WA UPENDO ULIOTUONYESHA.
ReplyDeleteHongera Mama, laiti kama NGOs zingine zingeiga mfano wako, mateso wanayopata watoto yatima yange pungua. Tunawaomba pia wale watu wenye mabilioni benki hawajui wayafanyie nini, waige mfano wa Mama Lucy katika kusaidia wahitaji. Asante Mama na MUNGU akuzidishie Moyo wa Upendo
ReplyDeleteKwa wale wanayopenda kujua zaidi email: lufilyo@yahoo.com
ReplyDelete