Ndugu Wananchi;
Leo tunauaga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012. Naungana nanyi Watanzania wenzangu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na bahati ya kuiona siku ya leo. Wapo ndugu, jamaa na marafiki zetu wengi ambao hawakujaaliwa kuwa nasi kwa kuwa wametutangulia mbele ya haki. Tuzidi kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape mapumziko mema na sisi tuendelee kumuomba Mola wetu atujaalie rehema na neema tele katika mwaka ujao.
Mapitio ya Mwaka 2011 na Matarajio kwa Mwaka 2012
Miaka 50 ya Uhuru
Ndugu wananchi;
Mwaka 2011 ulikuwa mwaka wa aina yake na wa kihistoria kwa nchi yetu na wenye mchanganyiko wa mambo. Kulikuwa na matukio ya furaha na majonzi na ulikuwa mwaka tuliopata mafanikio mengi na changamoto mbalimbali. Tumeweza kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa heshima stahiki kama nilivyoelekeza katika hotuba yangu ya kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011. Tumezitumia vizuri sherehe hizo kufanya tathmini ya maendeleo tuliyoyapata tangu Uhuru mpaka hapa tulipo sasa pamoja na kutambua changamoto zilizo mbele yetu.
Kupata hotuba KAMILI BOFYA HAPA
Kupata hotuba KAMILI BOFYA HAPA
KIONGOZI: UCHUMI NA FEDHA NDIO KILA KITU!
ReplyDeleteJitahidi kuhakikisha Benki Kuu inazidi kurudisha thamani ya Shilingi ya Tanzania iliyoporomoka majuzi.
ULINGANISHI AFRIKA MASHARIKI:
SEPTEMBA 2011 DISEMBA-2011
KEN 107KS=1US$:84KS=1US$
TAN 1,750TS=1US$:1,610TS=1US$
UGA 2,450US=1US$:2,200US=1US$
RW 870RWF=1US$:805RWF=1US$
BR 1,900BRF=1US$:1,950BRF:1US$
Tukose mengi yote kimaisha lakini hili ni muhimili sana kwa Maisha yetu!