Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Toka yalipoanza kumiminika magari ambayo ni automatiki kila mtu anajiweka barabarani ili mradi anajuwa kunyoosha usukani na kukanyaga mafuta ipasavyo. matokeo yake ni vurugu tupu barabarani na kujifanya wanaharaka. mtu haelewi maana ya alama za barabarani hata moja inakuwaje yupo barabarani anaongoza usukani! tusipojifunza kufwata utaratibu mambo haya hayataisha kamwe.

    ReplyDelete
  2. msaada kwenye tuta. siioni shida hapo. saidia mimi taka jifunza kuendesha magari

    ReplyDelete
  3. hakuna tatizo hapo hapo gari zote zinakwenda upande mmoja ila mweye haraka anatakiwa akae kulia na kawaida kushoto

    ReplyDelete
  4. Barabara zetu zina walakin, mbona sioni road markings. Ndio maana huwezi kumshtaki mtu yeyote kwenye hiyo picha hatari . Mtu akiwasha gari yake anaonyeha nguvu ya gari yake akielekea ahera na wale atakaowasababishia ajali.

    ReplyDelete
  5. Nadhani hiyo ni barabara ya Morogoro Rd. Hata ningekuwa mimi nadhani ninge 'overtake'. Tatizo ni kuwa hiyo barabara inapaswa kuwa 'motorway' hivyo kuna kiwango cha mwendo kinachotakiwa, lakini kuna baadhi ya madereva wanaendesha kama wako kwenye harusi. Mmoja anaenda Mbeya mfano, mwingine anaenda Mbezi mwisho.. hivyo hawana haraka.
    Mi nakaa Kibaha nafanya kazi Dar, bila kufanya hivyo (ku overtake).. haufiki.. barabara hiyo hiyo baiskeli, hiyo hiyo waenda kwa miguu, guta, daladala, kila kitu humo humo hivyo hamna kufika. Sema ni umaskini, ila ilipaswa kuwa na motorway ya magari na piki piki tu, ambapo magari local yangepita njia tofauti ya pole pole.

    ReplyDelete
  6. Niionavyo mie, hakuna anayevunja sheria hapo. Hakuna mchoro wala sign inayokataza kuovateki. Njia inaonekana vizuri na wote wanamuda wa kurudi upande wao. Iwapo nimekosea, tupelekene shule bila matusi.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  7. Sheria za usalama barabarani pia hukamilika kwa kuwepo na road markings and signages, ni hatari kwa kweli, wahusika wanashtuka pale ajali inapotokea

    ReplyDelete
  8. Wizara husika inatakiwa kufanya kazi hapo.Hivi hawwasomi blogs za lugha nyingine zinavyoelezea ajali nyingi za uzembe zinazotokea Tanzania? Barabara nzuri watu wanaendesha ovyo,je ndiyo inawezekana bara bara za juu au ?
    Wanausalama barabarani wako wapi? si bora wasiwepo.

    ReplyDelete
  9. tatizo nini? Hiyo si ndio ONE WAY...

    ReplyDelete
  10. Hakuna road marking.Pengine ni one way . Kama siyo usiovertake gari zaidi ya moja

    ReplyDelete
  11. nadhani it is a one way road,
    Otherwise you can not overtake while climbing up hill, also once you overtake you must take back your lane before deciding to overtake again,
    Are cars supposed to keep left or right ?

    ReplyDelete
  12. Ankal,habari za kazi na matumaini uko poa!!!hapa mimi sioni kwanini walaumiwe madereva hata kama kuna Automatic cars!!!Hao wanaotengeneza hizo barabara hawaweki alama za barabara!!sehemu nyingi duniani,zinapojengwa barabara hata za vichochoroni zinaweka alama za matumizi ya barabara hata kwa kupakwa rangi nyeupe kwenye barabara zenyewe hata kama hakuna vitenganishi vya kuonyesha hii barabara ni ya magari yanayokuja upande mmoja wa kulia na yanayoenda upande wa kushoto(kwa mtazamo wa picha iliyotolewa)!!na Madereva wenyewe wanaheshimu alama hizo kwa kuwa sheria inafuatwa na watumiaji,uki kihuka sheria,penati notice na 3 points zinakatwa kwenye licence yako. Tuvumilie na tusubiri tusheherekee miaka mingine 50 ya uhuru(100 yrs)kimchongo mchongo.

    ReplyDelete
  13. Ila unaona barabara siyo?

    ReplyDelete
  14. Mimi naona wako sawa kutokana na mazingira ya hilo eneo iwapo tu speed waliyo nayo iko katika kiwango cha kawaida na siyo 140+. Unaovertake pale ambapo kuna visibility na unaweza kuona vizuri mbele ya gari unaloovertake. Kama gari la pili kutoka mbele likiovertake basi ni hatari kwani hakuna clear visibility mbele yake na hawezi kuona kinachokuja mbele ya gari iliyotangulia.

    Wa kumlaumu hapo sana sana ni TANROADS kwani hakuna alama yoyote na barabara haijachorwa hivyo dereva atatumia uzoefu zaidi na siyo maelekezo ya usalama barabarani.

    I stand for corrections if I am wrong kwani we are talking about lives here na ninachoandika kuna mtu atakichukua kama somo. Ila ni mtazamo wangu tu kutokana na ujuzi wangu.
    Mdau - Mwanza.

    ReplyDelete
  15. nimesoma comments nyingi za hapo juu na kimsingi nimeshtushwa na nyingi ya hizi comments zinazodai hapo hamna tatizo.Na pengine ndo maana ajali haziishi kwenye mabarabara yetu.

    Wadau hilo eneo ni mpandisho/mlima,kimantiki siyo eneo salama kuovateki.Huihitaji alama ya TANROAD kuona ni eneo lenye mlima.Kwa kanuni za usalama barabarani za Tanzania (ndizo ninazozifaham)ni marufuku kuovateki eneo la mpandisho km hilo.Hizo blabla za kuwahi kibaha ndizo zinazosababisha ajali kila leo.

    Tii sheria bila shuruti

    ReplyDelete
  16. Ni kweli alama za barabarani hakuna ila kutumia common sense unapo drive muhimu.Driver huoni mbele vizuri since kuna mlima,mteremko,kona,folen ya magari mbele yako ni ndefu so huwezi overtake ukizingizia alama za road hakuna.Kama ni kupoteza maisha ni driver,abiria wake so tutumie akili tuwache visingizio au tumezira?.Wanausalama nao waangalie matatizo kama haya yakutokuwa na alama za barabarani ni chanzo kikubwa cha ajali na vifo vingi Tz.

    ReplyDelete
  17. Is't one way or two ways you can not tell

    ReplyDelete
  18. Ndio maana hata darasani kuna wa kwanza na wa mwisho kama dereva unatakiwa kufwata sheria za barabarani sio mpaka uamrishwe jaman tutasukumwa kwenye kila jambo mpaka lini nyie msioona hapo kuna makosa kweli mmenishangaza kwanza hutaki kutembea taratibu kuliko kawaida hilo ni kosa pili ni kosa ku overtake kwenye kilima

    ReplyDelete
  19. Hii picha iko tricky kwa jinsi nilivyoielewa ni kwamba magari haya yanatoka katika kilima yaani yako/yanaingia katika mteremko!

    Kwanza magari yoote yanayo-overtake yanafanya makosa ukiangalia vizuri hamna hata moja lililowasha indicator! Na kama labda picha imeshindwa kuonyesha basi kuna vitu viwili vya kuzingatiwa katika hali kama hii ile nissan nyeupe inayo-overtake kule mbele inaruhusiwa tu ku-overtake ile suzuki nyeupe na si salon na haitakiwi ku-overtake yale magari mawili kule mbele maana kuna gari inakuja (oncoming vehicle)na kuna uwezekano mkubwa wa kuhatarisha gari inayokuja!

    Pili hii salon ndogo ya mwisho inafanya makosa maana itambidi afanye overtaking hizo gari mbili kwa vile nafasi kati ya vitara na landcruiser nyeusi ni ndogo! Pili huyu mwenye vitara nyekundu anapaswa kupunguza mwendo kuiruhusu hii salon ya mwisho ku-feed in!

    Pili hii landcrusier nyeupe ilipaswa ionyese inaanza kurudi upande wake na cha kushangaza ni kwamba ina nia ya ku-overtake suzuki ni makosa!

    Na kwa kuzingatia hii ni barabara kuu yaani gari ndogo haziruhusiwi kwenda zaidi ya 100km/hr basi kwa yeyote anayezuka hiyo limit amevunja sheria!

    kazi kweli ipo hapo

    ReplyDelete
  20. Hakuna alama hapo!

    ReplyDelete
  21. Kwa uzoefu wangu mdogo wa kusoma picha nilioupata sekondary inaonekana na wewe uliyepiga picha ulikuwa kwenye upande wa ku-over take.Kazi kweli kweli.

    David V.

    ReplyDelete
  22. To me the road is clear NO problem at all, ila sina uhakika zaidi na ninachokiona. sielewi kama kule mbele jinsi picha ilivyopigwa manake aliyepiga alikuwa juu basi kama kuna mlima au mwinuko mkali hao wanaopiga overtake hawaruhusi kufanya hivyo eneo hilo ni hatari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...