![]() |
Hayati Hanipha “Kange” Omari Sultani (14.3.59 - 9.12.2011) |
Tarehe 9 Desemba 2011, siku ya kusherehekea Uhuru wa Tanzania Bara, Bi Hanipha “Kange” Omari Sultani, mzaliwa wa Kijiji cha Kashoju, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera na mkazi wa eneo la Africana, Mbezi Beach , Dar es Salaam , aliaga dunia. Ndugu, jamaa na marafiki walitoa msaada tangu Bi Hanipha alipoanza matibabu Hospitali ya Lugalo na Muhimbili jijini Dar es Salaam na baadaye katika Hospitali ya Appolo ya Bangalore nchini India alipoenda mara kadhaa kwa ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu.
Aidha, tuliendelea kupata ushirikiano wenu wakati Bi Hanipha alipokuwa akipata tiba, ushauri na uangalizi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, na Hospitali ya Rubya, Wilaya ya Muleba hadi mauti yalipomkuta na hatimaye mwili wake kusafirishwa kwenda Ngujini, Taarafa ya Usangi, wilayani Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro, kwa mazishi yaliyofanyika tarehe 12 Desemba, 2011.
Familia ya Omari na Sultani Muyanza, Familia ya Alhaji Omar Kahabuka ya Kashoju Muleba na ile ya Mwalimu Sultani Issa Mundeme wa Chuo Kikuu cha Ardhi na wanawe Mage “Dokta” Adua, Mwatum “Tush” Kwame, Karama “Braza Kay” Sultani, na Asia “Kisura” Sultani walifarijika sana kwa dua na ushirikiano wenu katika kipindi cha mtihani mkubwa uliowafika. Kwa vile si rahisi kuwashukuru mmoja-mmoja maelfu ya watu na taasisi mbalimbali kwa maliwazo na misaada yenu ya hali na mali , tunaomba kwa moyo mkunjufu mpokee ujumbe huu kama tamko letu la kusema: “Havacheni mno”/”Mbakasinge muno” - AHSANTENI SANA. Mwenyezi Mungu awabariki na kuwazidishia neema na baraka zake.
Hata hivyo, tunaomba kutoa shukrani mahsusi kwa hawa wachache wafuatao: Utawala na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), madaktari wa hospitali za Lugalo, Appolo na Rubya; Masjid Akram ya Mbezi Beach, Msikiti wa Ngujini, Umoja wa Kina-mama wa Masjid Akram; uongozi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Tiger Friendship Society, Tanganyika British Legion, Gimco Ltd (Nairobi), Utawala na wafanyakazi wa Gimcoafrica Ltd (Dar) na Africa Property Ltd; AGIP House Owners Association na Ultimate Security.
Tunaomba pia kuwataja Mhe. Cleopa David Msuya, Mhe. Mathias Chikawe, Mhe. Profesa Jumanne Maghembe, Alhaj Ramadhani Salim, (Bakwata – Kilimanjaro), Balozi Fadhili Daudi Mbaga, Mabwana Audax Rusenene, Harry Mugo, Heriel Muro, Davis Senkoro, Richard “RK” Muzo, Dr Alex Nguluma, Prof Yunus Mgaya, Dr Othman Chande, Haroun Madoffe, Rashid “Madou” Othman, Hamis Kindoroko, Lovice Liberty, Col Masangya, Agrey Kajiru, Mwalimu Muro na familia yake, Stephen Kangero, Mama Kafanabo, Eidris Mavura, Fanuel Kibakaya (Maun, Botswana), Ziddy Mgaya, Prof Ward Mavura, Dr Issa Mbaga, Dr Doctor Angella Thomas, Doctor Diwani Msemo, Dr Juma Nyangasa, Bibi Koku, Bi Ashura Pyaru, Mama Pamba na Familia ya Nkini Godfrey, Bi Hanipha, Mkurugenzi Mteule wa Manispaa ya Mtwara wakati anafikwa na mauti, alikuwa mtoto wa kwanza wa Alhaj Omari Kahabuka na Bi Asia Kagaruki, Dada wa Eng. Shaaban “Mgurusi”, Hidaya “Ma-Fatu” Muyanza, Sophia “Mwai Mdori” Omari, Nadhipha “Ma-mdogo” na Majid. Aidha alikuwa na swahiba mkubwa wa Bi Halima “Boss” Sekoutoure, Omari “Ba-Fatu” Iddi, Dr Huba Ndama-Nguluma, Rukia Hatibu-Madoffe, Kipwele “Namoshi” Kipwele, Ali “Gopal” Juma, Eileen “Mama Naiz” Mavura, Zeal “Papaa” Mundeme na Abdi “Baba Tush” Sultani.
* Mpenzi Hanipha, ni kweli umetutoka kimwili, lakini umebaki na utaendelea kubaki ndani ya mioyo yetu daima. Upendo, ukarimu, ucheshi, uchapa kazi, hekima na busara zako zitadumu nasi kama dira na changamoto kwa ulotaucha nyuma, katika juhudi za kutenda mambo bora kama njia ya pekee ya kukuenzi. Hebu tumrejelee Sh. Robert
“Amina (soma Hanipha) umejitenga, kufa umetangulia,
Ninakutakia mwanga, peponi kukubalia,
Sikutaka ushindike, maradhi kukuchukua,
Ila kwa rehema yake, Mola amekuchagua.
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua”
n ‘Amina’ kutoka Shaaban Robert, `“Maisha Yangu” (1958)
ìInna lillah wa ina illayh rajíunnî
MOLA NA AILAZE PEMA PEPONI, ROHO YA BI HANIPHA - AMINA.
Pole sana Sultani, our thoughts are with you and your family - FM, Oz
ReplyDeletePunzika pema mama Karama! Nakukumbuka sana enzi zetu za magorofani Breweries!
ReplyDeleteMungu wafariji wafiwa! Amen
Nawapa pole watu wote wa familia ya Kahabuka na Mundeme kwa msiba huu mkubwa. Tunamwomba Mwenyezi Mungu Muumba wa yote amweke dada yetu Hanifa mahali pema peponi. Amin.
ReplyDeleteINNA LILLAH WA INNA ILAYHI RAJIUUUN
ReplyDeleteHabari za kusikitisha sana. Tunamuomba Mwenyezi Mungu apumzishe roho ya marehemu kwa amani, Amen! Baada ya kusoma vizuri tangazo, nimegundua kuwa nilipata kumfahamu marehemu. Hii ilikuwa zaidi ya decade mbili zilizopita kwa mara ya kwanza na labda ndio ilikuwa ya mwisho, kupitia kwa rafiki yangu na former Jangwani high school class mate Leda Issa ambaye alikuwa wifi wa marehemu. Tulikuwa wanafunzi enzi hizo. Poleni sana Leda na wafiwa, Mungu awajaze imani.
ReplyDeleteMungu aiweke roho ya marehemu shemeji yetu mahali pema peponi, Amin - MO
ReplyDeleteTulikupenda bali Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema alikupenda zaidi. Kwa kuwa ulikuwa mtu wa watu,
ReplyDeleteutaendelea kubaki mioyoni mwetu daima. Umetuachia majonzi makubwa sana kwa sababu "you have gone too early', lakini tunakubali kuwa hayo ndiyo mapenzi ya Mola wetu. Amechagua Ua lililo zuri kwenye Bustani yake, akachuma. Mwenyezi Mungu ailaze Roho yako Mahali pema peponi mpaka hapo tutakapokutana tena tena, Amina.
Poleni sana familia ya marehemu. I remember Hanifa as a friend and colleague tukiwa OUT. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
ReplyDeleteeeeh !mwenyezimungu kila nisomapo ujumbe huu nahisi kama vile ndugu yangu nadio kwanza kaondoka muda si mrefu na huwenda siku moja karejea!jamani pumzika my dada pumzika Hanifa wewe ulikuwa ni mshumaa katika familia na ghafla ukazima bila kutarajia.ni miaka 8 sasa lkn bado upo ktk nyoyo zetu.R.I.P dada ipo siku tutakutana.Mungu ndio ajuaye.inna illahi wahillah rajuun.
ReplyDelete