TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI TAHADHARI YA ONGEZEKO LA MVUA MAENEO YA KUSINI MWA NCHI.

Msimu wa mvua unaendelea katika maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka (mikoa ya Mtwara,Lindi, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Morogoro kusini,Rukwa, Dodoma, Singida, Kigoma na Tabora.)

Katika kipindi cha siku tano kuanzia Januari 5 hadi Januari 10, 2012, mgandamizo mdogo wa hewa katika eneo la rasi ya Msumbiji unatarajiwa kuendelea kuimarika hivyo kusababisha ongezeko la mawingu katika maeneo ya kusini mwa nchi.

Hali hii inatarajiwa kuimarisha makutano ya upepo wenye unyevunyevu katika maeneo hayo, hivyo kusababisha vipindi vya mvua kubwa katika maeneo ya Nyanda za juu kusini magharibi (mikoa ya Iringa, Mbeya na Rukwa), maeneo ya kusini (mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi), baadhi ya maeneo ya Kusini mwa mkoa wa Pwani na Kusini mwa mkoa wa Morogoro (Mahenge).

Aidha mvua za kawaida za masimu zinatarajiwa kuendelea kunyesha katika maeneo ya kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida) na magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma na Tabora).

Maeneo ya Pwani ya kaskazini ( mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani na visiwa vya Unguja na Pemba), baadhi ya maeneo ya Nyanda za juu kaskazini mashariki yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua ambazo ziko nje ya msimu.

Mvua hizi zinatarajiwa kuambatana na upepo mkali katika maeneo ya Bahari ya Hindi, hivyo watumiaji wa Bahari wanashauriwa kuchukua tahadhari.

Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya Hali ya hewa na athari zake na itaendelea kutoa taarifa.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hii taasisi haina vifaa vya kisasa vya kupimia hali ya hewa.Nchi za wenzetu wanakwambia kabisa mvua ni saa flani sehemu flani.Sio hapa tahadhari halafu hakuna kitu .kuna kipindi ghfala tu mvua ikinyesha kesho yake ndo wanaibuka

    ReplyDelete
  2. Wewew Mdau, sawa pana wakati mambo yanakwenda ndivyo sivyo isipokuwa Hii taarifa imetoka jana kukiwa hakuna hata dalili na leo kama upo jijini Dar unaonaje anga lilivyo?

    Si ndio dalili zanyewe hizi za mvua?

    ReplyDelete
  3. Nakuuunga mkono mdau wa kwanza wewe wa pili unachemka tu walisema mvua sio dalili za mvua!

    ReplyDelete
  4. Mdau hawa ni watabiri, "tabiri kiswahili ni hali ya kutegemea huenda kitu kikatokea au la" kwa maana hiyo itokee au isitokee matokeo yoyote ni sahihi.tabiri=kubahatisha!

    ReplyDelete
  5. Kiswahili kigumu, na mdau no 1 kukaa kwako huko nchi ya wenzako usituzingue, kwa sasa tumepiga hatua, mshukuru Mungu kwa yale mafuriko kila mara sasa utabiri uko wazi. taratiibu vifaa vya kisasa vitakuwepo kwa sasa watapunguza ufisadi.

    ReplyDelete
  6. watu nwa hali ya hewa siku hizi mnajitahidi... mnatoa tahadhari kabla ya hatari haijatokea. Hongera DR kijakazi

    ReplyDelete
  7. Ubishi wa wa Tanzania ni balaa, sasa wana bisha nini, Dalili za mvua hakuna?

    Wanaoishi Dar anga lipo vipi leo?

    Tatizo Wa Tanzania ni watu wa Siasa zaidi kuliko Sayansi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...