Marehemu Jeremiah Sumari
Kwa masikitiko Makubwa, Ofisi ya Bunge inawatangazia Waheshimiwa Wabunge na Wananchi wote kuwa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 19 Januari, 2012 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia na Chama chake imeandaa shughuli ya kuaga rasmi mwili wa Marehemu siku ya Jumamosi, tarehe             21 Januari, 2012 katika Viwanja vya Karimjee kuanzia saa 5 asubuhi na baada ya hapo atasafirishwa siku ya Jumapili asubihi kuelekea Kijijini kwao Akeri, Meru, Mkoani Arusha kwa mazishi yatakayofanyika siku ya Jumatatu tarehe 23 Januari, 2012.

Kutokana na msiba huo, shughuli za Kamati kwa siku za Jumamosi tarehe       21 Januari, 2012 na Jumatatu tarehe 23 Januari, 2012 zimesitishwa na zitaendelea tena siku ya Jumanne tarehe 24 Januari,2012 baada ya maziko.

Marehemu alikuwa anaumwa Saratani ya Ubongo ambayo ilimsumbua kwa muda mrefu na mnamo mwaka 2010 alipelekwa nchini India kwa upasuaji na alirejea nchini na hali yake ilikuwa ikiendelea vizuri. Hata hivyo mwishoni mwaka 2011 hali yake ilibadilika ghafla na kuanza kuwa mbaya alirejea nchini tarehe 9 Januari, 2012 na kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alifariki dunia tarehe 19 Januari, 2012.
 Marehemu ameacha mjane na watoto wanne (4).

MWENYEZI MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU
MAHALI PEMA PEPONI, AMEN
 Imetolewa na:
 Idara ya Habari, Elimu kwa Umma
     na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge
S. L. P. 9133
DAR ES SALAAM
 19 Januari, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Poleni wafiwa kwa msiba huu

    ReplyDelete
  2. Poleni familia ya marehemu Sumari,kazi ya Mungu haina makosa,sote tunapita humohumo.
    Amina!.

    ReplyDelete
  3. Poleni sana wanafamilia wa Jeremiah Sumari. Arumeru Mashariki imepoteza mwakililshi mtu wa watu na kiongozi mwenye busara. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amen. Ndokuaruu.

    ReplyDelete
  4. Mwenyezi mungu ablaze roho ya marehemu mahali Pema peponi. Amin

    ReplyDelete
  5. Poleni sana wafiwa, Jerry alikuwa mtu wa watu mchechi na msikilizaji wa kila mtu awe mdogo au mkubwa. Mungu ailaze roho yake Pema Peponi.

    ReplyDelete
  6. hivi! "kifo cha marehemu" maana yake nini? jamani, kama lugha yetu ikitushinda nani aiweze?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...