Familia ya Dkt. Fanuel Maro wa Upanga/Kariakoo jijini Dar es Salaam,inasikitika kutangaza Kifo cha Baba yao Mpendwa Dkt. Fanuel Maro (pichani) kilichotokea jana jioni (tarehe 7/1/2012) katika Hospitali ya Regency iliopo Upanga jijini Dar es Salaam.
Utaratibu wa Kutoa Mwili wa Marehemu hospitali hapo na Kupelekwa Nyumbani kwa Marehemu Upanga Mtaa wa Longido zinafanywa hivi sasa.
Ibada ya Kuaga Mwili itafanyika katika Kanisa la KKKT Azania Front jijini Dar es Salaam siku ya jumanne (tarehe 10/1/2012) na baada ya kufanyika kwa ibada hiyo Mwili ya Marehemu utasafirishwa kuelekea Old Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa Mazishi ambayo yatafanyika siku ya Jumatano (tahere 11/1/2012).
Mungu aiweke Roho ya Marehemu Dkt. Fanuel Maro mahala pema peponi
-Amein.
Poleni wafiwa. Huyu ni babayake mzazi Balozi wetu nchini zambia? Mhe. grace Mujuma?
ReplyDeleteRIP Dr. Maro, ninatoa pole kwa familia yote ya Dr. Maro. Mungu aifariji familia ya marehemu.
ReplyDeleteJirani Upanga.
RIP Dr Maro, Pole kwa wote mliofiwa Dada Grace na wote. Poleni na kazi kubwa mliyofanya kumtunza mgonjwa. Mama Maro I hope you find peace and acceptance....
ReplyDeleteDr. Peter pole sana na kufiwa na mpendwa Baba yeti.
ReplyDeleteApumzike kwa Amani. Dr. Ngirwa
Poleni sana wapendwa wetu. Babu yetu umeondoka kwenda mbinguni kwa aliyetuumba. Tutakukumbuka sana kwa huduma zako bora, utumishi uliotukuka na utu uliokuwa nao. Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema. Amina.
ReplyDeletePoleni sana familia ya Maros, Tarimos na ndugu na jamaa wote waliopo Old Moshi Tella na sehemu nyingine mbali mbali. Mungu awape faraja kwa wakati huu mgumu. Ameni
ReplyDeletePole Maureen and the entire Maro family.
ReplyDelete