![]() |
Wananchi marekani wakipinga sheria hiyo |
Kama ulitembelea tovuti kubwa kama Google, Wikipedia na hata Facebook, nadhani uliona kuna ujumbe uliokuwa unaonesha kupinga miswaada miwili ambayo serikali ya marekani inatizamia kuipitisha kuwa sheria. Miswaada hiyo ni SOPA na PIPA.
Lakini unaweza kujiuliza hii SOPA na PIPA ni vitu gani? SOPA ni kifupi cha Stop Online Piracy Act (SOPA) na ile nyingine ya PIPA ni Protect Intellectual Property Act , ni muswaada ya huko marekani ambayo lengo lake ni kukazia zaidi haki miliki kwenye sheria za marekani, kwa sheria hii lengo kubwa ni kulinda wamiliki wa vitu au huduma zinazotolewa online pia kutoa adhabu kali kwa watakaokubwa na kosa hilo.
Kwan sheria hii itampa mamlaka zaidi mmiliki wa haki miliki kuweza kuwasilisha suala lake kwa mapana zaidi huku yakiwaweka kizuizini makampuni au tovuti zote zitakazo vunja sheria hii, iwe ni ya marekani au ya Tanzania.
Swali kuwa ambalo unaweza kujiuliza ni kuwa kwanini wamiliki wengi wa tovuti wameigomea? Je sheria hii haimaanishi kitu kizuri? La hasha, sio kila kitu kizuri lazima kikubaliwe. Kupitishwa kwa sheria hii kutaondoa uhuru wa kujieleza ambao ndio umejenga ulimwengu wa tovuti za leo. Kwa mfano, mtandao wa Facebook na Wikipedia umejengwa kwa misingi ya watu kugawana maarika au taarifa.
Sasa ndani ya sheria hii hutoruhusiwa kugawa taarifa au kumbukumbu ambayo sio yako au bila ruhusa ya mwenye taarifa. Kinyume chake mmiliki wa tovuti atachukuliwa hatua. Hapa tunaenda kwenye kile kitu kilichowafanya Google kutimka Uchina( censorship). Chukulia mfano leo hii unataka kuweka habari kwenye Facebook, ni lazima uhakikishe ile habari ni yako au mmiliki anaruhusu kuiweka kule, la sivyo itakuwa ni kosa.
![]() |
Picha inaonesha mtandao wa Wikipedia ukipinga sheria hiyo. |
Kutokana na maelekezo yaliyomo kwenye sheria hiyo,tovuti zote za marekani zinatakiwa zisifanye biashara wala kuionesha tovuti yoyote ambayo itapatikana na kosa na kwenda kinyume na sheria hii, hii inamaanisha kila tovuti inatakiwa kuwa makini katika mambo mawili
1. Kuangalia kila taarifa wanayoweka haijavunja sheria ya haki miliki(censorship)
2. Kutofanya biashara ya namna yoyote na kampuni yoyote iliyo nje ya Marekani ambayo imeorodheshwa katika wakiukaji wa sheria hii.
Kwa muono wa mbali, hatua hizi ni kuzuia uhuru wa intanet kama wenyewe wanavyouita( Internet Democracy)
Je sisi inatuhusu?
Swali ambalo unaweza kuanza kujiuliza, sheria ya marekani inatuhusu vipi sisi Watanzania? Ukweli ni kuwa sheria hii haitoishia marekani tuu, kwani makampuni ya marekani hayatoruhusiwa kufanya biashara na kampuni yoyote duniani ambayo imevunja sheria ya Marekani na kutofanya hivyo ni kutenda kosa. Pia wasajili wa majina, wahifadhi tovuti(hosting) watatakiwa kuiondoa tovuti yoyote iliyokiuka sheria hii toka kwenye seva zao na mengine mengi. Sheria hii itakuwa na athari kubwa mno kwa mataifa yanayoendelea kama Tanzania ambao hatuna vitu vya kwetu wenyewe.
Hivyo basi, kwa mtazamo wangu naona sheria hii ni changamoto kwetu kujitahidi kuwa na vitu vyetu wenyewe kitu ambacho kitatufanya tuweze kusimama bila shaka kwani kila taifa huleta sheria ambazo zina faida kwao. Ingawa sheria hii imepata upinzani mkubwa toka kwa wamarekani, lakini haukutungwa kwa ajili ya kuwashambulia wamarekani, ni kwa ajili ya mataifa ya nje ila kwakuwa tunaishi katika ulimwengu ulioungannika hivyo kwa njia moja au nyingine wamarekani nao wataathirika. Si unakumbuka waziri mkuu wa uingereza alivyoshikia bango mambo ya jinsia moja na kuzilazimisha nchi zetu kufuata matakwa yake?
Kutokana na sababu hizo, makampuni mengi ya ya intaneti yanaod=na sheria hii ni kama kuwaziba midomo na kuanza kuwa China ya pili.
Je wewe unaonaje??
MIMI NAIPINGA, NLIKUWA SIJAELEWA KWA MAKINI NA NILIHISI NI KITU KIDOGO TU.
ReplyDeletePRINCE SAB
Sheria ni nzuri kwa kuwa haitamuonea mtu na wezi wote wa kazi za watu watashughulikiwa ipasavyo. Kuhusu kuwa nchi zitakazoaathirika ni zinazoendelea ikiwamo Tanzania yetu hilo ni kweli kabisa kwa kuwa hatuna kitu chetu tunachokitegemea wenyewe kila kitu mpaka tudandie vya ulaya na Marekani. hii ni changamoto kwetu kuwa tuamke usingizi na tujuwe kuwa tupo vitani sasa. Chanzo cha sheria hii mpya ya wamarekani inayokuja ni makampuni ya filamu Hollywood na yale ya music ndiyo yaliyo nyuma ya pazia la Kongresi. hawa watu wanajaribu kulinda biashara yao ambayo kwa sasa imezimia wote ni mashahidi Filamu iliyotoka jana wewe unaitazama leo online bureeeeeeeeeee hata senti ulipii zaidi ya internet unayotumia sasa hili ni tatizo hata kwa akina kanumba wetu nao hawapati hata hivyo visenti vichache. Google walikimbia uchina, ndiyo kabisa, lakini china ndo inasonga mbele tena kwa spidi ya ajabu mpaka na wao wanatetemeka leo hii inafikia hatua mpaka ya kutaka kuinunua Ugiriki ambayo imefilisika. Facebook pia ilishakomeshwa uchina siku nyingi tu lakini zote hizi ni changamoto kuwa sisi nchi changa tuamke sasa na yatakuja mengi tu kama kukata misaada ya kibajeti na kadhalika. sheri hii ina madhara kwetu ila AMKENI ACHENI KULALA. mwisho asante mtoa mada kwa ufafanuzi mzuri wa muswada tena umeuleta kwa lugha rahisi kabisa hongera sana. naomba kutoa hoja.
ReplyDeleteMaoni yako ni mazuri. Kwa mtazamo wangu jambo hili ni muhimu kwa dunia nzima lakini zaidi kwa Wamarekani wenyewe ndiyo maana wanaandamana.
ReplyDeleteKwa upande wa pili wa shilingi kama hii sheria ikipita Marekani tu, na iskuwe kufikia kiwango cha 'Customary International Law', raia na wenye-server kutoka nchi zingine kama China, India na South Korea zitafaidika na PIPA na SOPA kupita, kwa sababu watu nje ya Marekani watataka na wataendelea na biashara na kawaida kati yao.
Swahili moja kwa mwandishi: Je, Unamaanisha nini haswa unavyosema hatuna kitu cha kwetu?
Mdau ubarikiwe sana kwakutuelimisha.hata mimi siikubali sheria hii maana si ajabu hata blog ya jamii ingepaswa kuomba kibali Marekani kabla ya kubandika haya maelezo yako -:)
ReplyDeleteMaana yake kina Michuzi na Magazeti ya kibongo waache kudesa!!
ReplyDeletemarekani kwa kupitisha hii sheria itakuwa imekiuka kitu tunaita net neutrality na pia itawapa kazi kubwa ISP na wengineo kuangalia kila taarifa inayoingia kitu ambacho ni garama kwao, na pia inahitaji garama kuweka vifaa vya kuangazia kila content inayopitia kwao.miswada hiyo ikipita itanyonga uhuru wa kujieleza ktk mitandao mikubwa kama facebook na google.leo hii wamefunga kampuni kubwa ya kushare mafile MEGAUPLOAD kitu ambacho kilikuwa kinsaidia nchi maskini kama Tanzania,,usa WANASEMA NI BIASHARA HARAMU KWANI WANAKIUKA COPYRIGHTS HATIMILIKI.
ReplyDeleteHata mimi, nashukuru mdau kwa uchambuzi kwani nimeelewa sasa, Anko unaweza kutuwekea details za mdau nahitaji kumuuliza maswali zaidi.
ReplyDeleteMi napenda kumshukuru mtoa mada kwa kutuelewesha kiundani na nafikiri taairifa hii ni vizuri uwafikie hao viongozi wetu ili wajue kuwa tunahitajia kujiendeleza wenyewe na kuacha malumbano ya kisiasa.
ReplyDeleteMDAU HILI NI SWALA PAANA SIO KAMA LINAVYOONEKANA. HII NI NJIA MOJA WAPO YAPO YA VYOMBO VYA DOLA KUTAKA KUWACONTROL WATU HEART NA MIND. LEO PRESS TV LICENCE YAO IMEKUWA REVOKED UK. SHAME ON A SO CALLED "DEMOCRATIC WORLD".
ReplyDeleteMdau ingawa hukutaka kujitambulisha ila mimi bibnafsi kama wengine hapo juu walivyosema nakushukuru sana kwa kutuelimisha.
ReplyDeleteDavid V
Muswada hii ya PIPA na SOPA si tu itaathiri matumizi ya kawaida ya mitandao lakini itatuendesha kwenye kulipia taarifa zote zilizopo mitandaoni... mambo ya shareware/freeware, public domains ndo mwisho wake. it is a very stressful moment to a person such as mark zuckerberg.
ReplyDelete