Haya ni Baadhi ya Magofu ya Kale yaliyopo katika kitongoji cha Tongoni,njiani kama unaelekea Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga ambayo ni moja ya sehemu za historia ya nchi yetu kama tulivyoletewa taswira hizi na Mdau aliopo huko.Eneo hilo lipo karibu sana na bahari na mandhari yake ni nzuri mno kwani kuna breeze nzuri sana kutoka baharini. Msimuliaji alisema kuwa waliokuwa wanaishi hapo kwa wakati huo ni Washirazi, ambao kwa sasa wameenea maeneo ya mwambao na wengine visiwani (Zanzibar na Pemba)
Home
Unlabelled
Taswirazz za Magofu ya Kale Mkoani Tanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Loh hongera sana kwa aliyeleta picha hizi. Hii kwa uhakika ilikuwa ni jamii ya Kishirazi kama vile ilivyokuwa kwa Kilwa, Bagamoyo, Unguja na Pemba. Design ya makaburi ni hiyo hiyo.
ReplyDeleteHassan bin Ali alikuja na wanawe saba kutoka Shirazi na kila mwana alihamia kwenye kisiwa chake.
Hii ya Tongoni ndiyo kwanza nione na nimeongeza ujuzi wa historia yetu.
kwa kweli inasikitisha sana kuona serikali haina bajcentseti kabisa ya kifedha kuhifadhi na kurekebisha majengo haya yote
ReplyDeleteserikali iyaangalie haya magofu maana yanatoweka yatakua baadae kiwanja tu,Kule UGIRIKI haya magofu yanatoweka kama hivi lakin yanajengwa tena utafikiri ni mepya mfano ACROPOLIS linajengwa upya kila siku kwa kutumia udongo ule ule uliotumika kujengea zamani -wanakwenda kuchukua visiwani mwao kujenga upya na si kwasababu ya kale yaachiwe tu
ReplyDeleteHii ni hazina kubwa ya Historia, bora matumizi ya mabilioni katika ankara zisizo na umuhimu yangeelekezwa hapa!
ReplyDeleteTanga is historic town, but it can be reflected in the way it is today. What is the problem?
ReplyDeleteTanga ina Historia kubwa sana, Mjerumani aliweka ndio Makao ya Serikali yake ya Afrika ya Mashariki (DEUTSCHE OAST AFRIKA BUNDESTAG)
ReplyDeleteKwa kuienzi Historia hii ya Utawala wao huku Afrika ya Mashariki, Ujerumani Mjini Berlin kuna gazeti la Kiswahili linaloitwa TANGAMANO.