Hii ni Barabara ya Mandela ambayo inatumiwa na magari mengi sana yakiwemo makubwa na madogo,lakini kumekuwa na tabia kwa magari makubwa kama haya kusimama hovyo hovyo Barabarani tena bila ya kuwepo na ishara yeyote inayoonyesha kuwa gari hiyo imepatwa na matatizo au ni maamuzi tu ya dereva kwamba anakaa maeneo hayo na amekwenda nyumbani kwake kula ugali,jambo ambalo linaweza kusababisha ajali wakati wowote kutokana na uzembe wa namna hii. 
Hata hili pia sio kama lipo kwenye mwendo,Limesimama na Dereva wake hata hayupo garini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. miezi michache ilopita tulimzika jamaa baada ya kugonga semi ilopaki kizembe km hizo zilizowekwa na mdau hapo pichani. jamaa kaacha watoto bado wapo primary skuli ni wadogo kabsa.trafiki inapaswa kuwathibiti hawa wajinga wachahce wanaongeza mayatima tu.

    ReplyDelete
  2. Kwaufupi hio barabara sasa ni chinjachinja.... kama unaitumia usiku inabidi uwe roho mkononi...magari makubwa huwa yanaharibika barabarani na wanayaacha hapohapo bila alama yoyote, so kinachotokea nii magari madogo kuingia uvunguni tu (ajali) maana hio barabara haina taa za barabarani so usiku hata ukiwasha full haitoshi...watu wengi wamepoteza maisha hilo eneo..
    something has to be done.
    ahsante

    ReplyDelete
  3. Waandishi wa habari hivi mnaishia tu kublog picha? Hali kama hiyo kwa nini msiipigie madebe hadi polisi usalama barabarani au yeyote anayehusika achukue hatua.Bongo ni bongo,ndiyo maana Babu na kikombe chake aliwaingiza watu mkenge.

    ReplyDelete
  4. INAUMA,INASIKITISHA,INATISHA,INATIA AIBU,INAKERA,INATIA HASIRA NCHI KUWA KAMA HAINA SERIKALI WATU WANAISHI FREEL STYLE KTK KILA NYANJA IWE BARABARANI NA HATA SEHEMU HATALISHI KAMA HIVYO.

    KWA MFANO HIYO NCHI INAMAANA HAINA SHERIA ZA BARABARANI???

    KWAUFUPI NI HIVI MAGARI MAKUBWA KAMA HAYO KWAZA HAYATAKIWI YAWE KTK UPANDE WA KULIA KUTOKANA NA KWAMBA HAYANA MWENDO.

    JAMANI TANZANIA INATIA AIBU SANA SIWEZI HATAKUELEZA.

    ReplyDelete
  5. INAUMA,INASIKITISHA,INATISHA,INATIA AIBU,INAKERA,INATIA HASIRA NCHI KUWA KAMA HAINA SERIKALI WATU WANAISHI FREEL STYLE KTK KILA NYANJA IWE BARABARANI NA HATA SEHEMU HATALISHI KAMA HIVYO.

    KWA MFANO HIYO NCHI INAMAANA HAINA SHERIA ZA BARABARANI???

    KWAUFUPI NI HIVI MAGARI MAKUBWA KAMA HAYO KWAZA HAYATAKIWI YAWE KTK UPANDE WA KULIA KUTOKANA NA KWAMBA HAYANA MWENDO.

    JAMANI TANZANIA INATIA AIBU SANA SIWEZI HATAKUELEZA.

    ReplyDelete
  6. INAUMA,INASIKITISHA,INATISHA,INATIA AIBU,INAKERA,INATIA HASIRA NCHI KUWA KAMA HAINA SERIKALI WATU WANAISHI FREEL STYLE KTK KILA NYANJA IWE BARABARANI NA HATA SEHEMU HATALISHI KAMA HIVYO.

    KWA MFANO HIYO NCHI INAMAANA HAINA SHERIA ZA BARABARANI???

    KWAUFUPI NI HIVI MAGARI MAKUBWA KAMA HAYO KWAZA HAYATAKIWI YAWE KTK UPANDE WA KULIA KUTOKANA NA KWAMBA HAYANA MWENDO.

    JAMANI TANZANIA INATIA AIBU SANA SIWEZI HATAKUELEZA.

    ReplyDelete
  7. huku mtoni kwa AZIZ ALI kuna watu wanapaki barabarani kama nyumbani kwao ni hapa kuna barabara inaiyongia kushoto kama unatoka mtongani nje kuna baa na gesti nadhani huyu mwenye hii biashara ndio anawaambia nyie mpaki hapo barabarani.Inakera kwa kweli.TANROADS mko wapi????

    ReplyDelete
  8. Kwa kweli ni hatari sana na uzembe wa hali ya juu. siku ya mkesha wa xmas kulikuwa na ajali mbaya iliyosabisha kifo, kulikuwa na lori limeharibika katikati ya barabara kwenye barabara ya kuelekea tabata na kwenye mwinuko hivi na lilikaa pale kwa takribani siku tatu! mpaka ajali ilipotea ndio likatolewa

    ReplyDelete
  9. Nawaambieni kelele zenu hazisaidii kitu sie ndio wenye nchi tunalotaka ndio linakua,nani kakwambia kwamba hilo gari limepaki vibaya??Msifuatefuate mambo ya watu nyinyi yenu mbona hatujayaweka humu?

    ReplyDelete
  10. Tumeshachoka kutowa maoni hapa sababu hakuna linalobadili Tanzania wahusika hawajulikani nikina nani wala hawana mapenzi na hii nchi

    ReplyDelete
  11. kwa nini vituo vya Television wasianzishe vipindi vya usalama barabarani ili kuwaelimisha wananchi na kuwakumbusha wanausalama pia?kwa sababu matukio mengine yanahitaji kukumbushana hasa kwa tanzania.

    ReplyDelete
  12. wananchi wapewe namba za wanausalama ili waweze kutoa taarifa kama kuna uzembe hupo barabarani kabla maafa hayatokea.ili wahusika wapigwe faini

    ReplyDelete
  13. Ni moja ya njia mbaya sana hasa usiku kwenye dry port ya AMI,Fiat nyeupe iliishia kwenye baloon coz haikuwa na break!town trips lorries ni mbovu balaa!Hakuna Hooks za kuhold containers ndio maana moja ikaachia ubungo mataa 40 feet!!Jah bless I n I!!

    ReplyDelete
  14. bongo tambarare katoe taarifa polisi ili uwape ulaji polisi.kila mtu anajihamini anafanya anavyotaka.Tukae kimya tuache mambo yaende kama kawaida.ukipata tatizo tatua mwenyewe.

    ReplyDelete
  15. Tusilalamike saana maana sote sisi tunamatatizo. Majuzi tu nilishudia ajali ya ajabu saana. Kulikua na semi limeharibika sehemu ya Iyovi Iyovi baada ya mikumi.

    dereva wa semi aliweka miti na majani kwa umbali wa kutosha tu na triangle kuashiria kuna gari mbele limeharibika. Huyu derva wa gari ndogo alikamua akaishia nyuma ya trela na kuua. Mdau nani mwenye makosa hapo.

    Swala la mandela road ni swala sugu kwani gari likiharibika hata kama unauwezo wa kulipaki service road inakua dili kwa watu wa manispaa. ila likiwa barabarani wanaamini kua gari bovu.

    Sasa ukiwa ni wewe utapaki wapi??? Ukiweka ishara wanakuja umeharibikiwa mda mrefu usipoweka una avoid usumbufu...

    Mdau upooooo

    ReplyDelete
  16. Alilipoti ............ akazushiwa kesi mbaya ya rushwa (shukuru Mungu ameshinda) hii ndo bongo, lakini tusichoke kupiga kelele.
    Ajali barabarani nyingi zinaletwa na malori makubwa hasa njia kuu za mikoani kwa kupaki ovyo, ovatake ovyo, kusafiri msafara na kuziba njia bila sababu. Nailaumu sana serikali kwa kuua reli. Reli ndo chombo cha kusafirisha mizigo, alafu malori yapungue barabarani, yafanya network baada ya reli kufikisha mzigo vituoni. Lakini hapa sababu maroli ni yao basi reli haifanyi kazi. Kumbuka enzi za Kambarage jinsi reli ilivyokuwa inafanya kazi. Alafu tunasema miaka 50 tumeweza tunasonga mbele (hizi ni lugha sa kisiasa tu). Watu wanakufa kwa tamaa zenu. Utakuta roli semi-trela kwenye kichochorocha mtaa. Hii nchi kweli haina sheria.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...