Siku ya Jumamosi tarehe 28 January ilikuwa ni siku ya furaha na muhimu sana ambapo wanafunzi waliopitia katika shule hiyo walikutana na kushiriki katika michezo mbali mbali,Chakula cha Pamoja,maongezi mbali mbali ya maendeleo na changamoto.
Shule hii ilianza toka mwanza 1959 mpk sasa watu mbali mbali wamepitia katika shule hii.Mwalimu Mkuu Mama G.Mtenga alitoa taarifa ya shule toka ilipoanzishwa Mpaka hivi sasa wanafunzi wengi waliohudhuria waliumia sana roho zao mpk wengine Machozi yaliwatoka baada ya kusikia Changamoto zifuatazo na vile vile kuziona kwa Macho yao;
Uchakavu wa majengo yanayohitaji ukarabati mkubwa.
Ukosefu wa Chumba cha Computer kitakachotumika kuwafundishia wanafunzi somo la TEHAMA.
Upungufu wa samani kama vile madawati,viti na meza kwa ajili ya walimu.
Ukosefu wa Umeme kwenye jengo la Utawala na Madarasa.
Baada ya Hotuba hiyo kutoka kwa Mwl Mkuu kamati ya Maandalizi ilipokea changamoto hizo na kujipanga kuzikabili kwa kushirikiana na wanafunzi wote waliokuwepo na wasiokuwepo kwa kuwapa taarifa kwa njia mbali mbali.
MCHANGO WA KAMATI;Kamati imeahidi kukabidhi shule set ya Dstv iliyounganishwa katika Education Package itakayowawezesha walimu na wanafunzi kupata masomo mbali mbali kupitia Television.
Kwa sasa shule haina TV kwa hiyo inabidi kuchangia kupata T.V hiyo mpk siku ya Jmosi 4th February 2012 iwe imepatikana ili Kamati ikabidhi Full set.Watu mbali mbali walitoa michango na wengine Ahadi…Tshs 165,000 zilikusanywa na Ahadi za Tsh 630,000 walioahidi waliafiki kukamilisha ndani ya Juma hili..Kwa hiyo kuna upungu wa shs 205,000 ili kuweza kununua Flat Screen yenye thamani ya Tshs 1,000,000/=.
KUKABILI CHANGAMOTO;Kamati imejipanga kuanza kukabiliana Kuweza kupata Computer 80 kwa ajili ya somo la Tehama ili zikishapatikana ndio nguvu za kuanza kuandaa Chumba maalumu cha kufundishia somo hilo zianze.Twajua watu wengi waliosoma katika shule hiyo wanaweza kutoa Computer kwa haraka zaidi,tupo tayari kupokea kiasi chochote cha Computer kwa atakayeguswa na hili.
MWISHO;Twaomba wadau wote watupe moyo na ushirikiano katika kuendeleza Umoja wetu kwa Manufaa ya shule yetu na Taifa kwa Ujumla.
Josiah Malekani –Mwenyekiti wa Kamati
Imenishika huzuni shule yangu tu pamoja ktk hili wana chang'ombe....Bila wewe Mwl Shilatu,Matemu,Mushi,Matanyanga,Mama mwanza,Mama Nachenga,Mwl mfuko,Mama Humba,Mwl Amani obote,Nisinge kuwepo nilipo sasa!.....mwanfunzi 1976-1982
ReplyDeleteShule haina TV?? Na TV zetu tulizoshinda miaka ile kwa matokeo mazuri ya mitihani ya darasa la saba zimekwenda wapi?
ReplyDeleteNa zawadi gani walipata kutoka mwaka wetu Last year 1999? Sisi ndio tulioweka rekodi ambayo haijavunjwa mpaka sasa ya kua nambari moja kitaifa!
Nakuona mzee patoo.., aka mzee wa query
ReplyDeleteBP
Well done wadau wa Chang`ombe PS, Michuzi naomba uwaambie waweke contact zao basi ili tuisaidie shule yetu ya zamani,ndimi Mdau Daktari ughaibuni.
ReplyDeleteSidhani kama Tangazo hili la Kukutana lilitangazwa vya kutosha.
ReplyDeleteMimi nimemaliza hapo Mwaka 1978 sikuwahi kuliona wala kusikia Tangazo hilo la Wito wa kukutana na ninawajua wenzangu wa Miaka hiyo ya 47 ambao tuna nafasi nzuri tu na tungeweza kusaidia kile tukiwezacho.
Miaka hiyo Mwalimu Mkuu alikuwa anaitwa Mr. John Shilatu.
Muwe mnatangaza vya kutosha vitu kama hivi. Tuna nia nkubwa tu ya kusaidia shule zetu maana ndizo zilizotujengea Msingi.
Ahsanteni
Nawapongeza ila chonde chonde msiwe mnajitafutia umaarufu kwa misaada yenu
ReplyDeleteHuu ndio upendo na uzalendo unaopaswa kuwa ndani ya mioyo ya watanzania. Natumia hili walioadhimia litafanikishwa kwa moyo na kwa wakati kama vile tunavyokuaga na moyo kwenye michango ya harusi.
ReplyDeleteTunaomba jinsi ya kuwasiliana na hawa wanakamati. Asante
ReplyDeleteTanzania hatuna utamaduni wa kufanya matengenezo. Sisi tunajua kutumia tu lakini siyo kukarabati/kutengeneza kidumu. Serikali inasubiri wafadhili waje kufanya ukarababti. Haya lakini tutafika tukiwa hoi bin taaban.
ReplyDeleteNitasaidiaje?.... nipo US.
ReplyDeleteMwalimu Nachenga /ATEMU WALISHAITWA KWA MUUMBA LONG TIME MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA
ReplyDeleteJosiah malekani...lol mdarisalama tuwasiliane tukupatie hizo computer unazotaka...fungua facebook page iwe rahisi
ReplyDeleteNimefurahia kuiona shule yetu ya Changombe Nilimalizia la saba(1981),Kama madau aliyopita Mwalimu John Shilatu alikuwa mwalimu mkuu.
ReplyDeleteTukipatiwa contact tunaweza kuchangia maboresho ya shule na mahitaji yake.Changombe hoyee!