Habari Mkuu Michuzi, na pole kwa majukumu.....naomba sana uweke habari hii, ili Wadau tujadiliane kuhusu swala hili.
Hawa Jamaa wa Chama cha Kisiasa cha nchini Italy, maarufu kwa jina la Lega,wanalalamika warudishiwe hela zao zilizotolewa kwa msaada nchini kwetu,kwani wamegundua hela hizo zimetolewa huko kwetu Tanzania na kuamua kuandamana...sasa hawataki kabisa, wanachotaka warudishiwe mshiko wao.
Mimi kama Mtanzania nimeona aibu sana kuhusu swala hili, ni kudhalilishana tu....tena maandamano na bendera yetu ya Taifa letu, hivi inakuwaje hii wadau hebu tujadili swala hili....na wahusika wanalichukuliaje hili?
Kwa habari zaidi tembelea; www.barakachibiriti.blogspot.com
Mdau
Chibiriti.
Tumezidi kuomba na sisi. Dhahabu tunayo, tanzanite, tunayo, almasi tunayo, mafuta tunayo, gasi tunayo. Tuacheni kuwa omba omba. Tutumie rasilimali zetu kujiendeleza wenyewe. Siasa ya ubepari na kujitegemea ni imperative!
ReplyDeleteMdau tunaomba ufafanuzi, pesa hizo zimetolewa na nani na wamekabidhiwa akina nani na ni kiasi gani na zimetolewa kwa makubaliano gani. Kama pesa zimetolewa ili kuimarisha kanisa, basi ni makosa kwa waitaliano kudai pesa kwa kudhalilisha bendera yetu. Nimetaja kanisa kwa sababu misaada ya Italy na Ireland huwa ni kwa ajili ya kanisa na siyo taifa. Ingawa misaada hiyo huwa haisemwi kama inapewa kanisa. Na kama mustakabali ndiyo huo wa kanisa basi hawana haki ya kutudai watanzania wote, isipokuwa wawasiliane na polycarp Pengo wawasilishe madai yao.
ReplyDeleteUngefafanuwa hizo pesa walitowa kama MSAADA kwa MSAADA? au zilitolewa kwa KUOMBWA na SERIKALI YETU ya Wa-Tanzania au TANZANIA? Kama tuliomba kwa sababu fulani na hizo sababu hazikurizisha au TULITUMIA sipo wanahaki na pesa yao. HAO WALITOWA MSAADA? au MKOPO?.
ReplyDeleteKAMA WALITOWA SERIKALI YAO WENYEWE KAMA MSAADA WANATAKIWA KUDAIANA WENYEWE HUKO. TANZANIA NAYO IJIFUNZE WAPI PAKUTAKA MSAADA NA NIYA YA KUZALISHA HATA IKIDAIWA WANAWEZA KULIPA. MZ
duh hii noma tunadaiwa mpaka basi naona tunapoelekea kuna hatari tukauza nchi au kuweka bondi ili tulipe madeni....................fezeha kubwa sana mwe!
ReplyDeleteKwani hizo pesa mlizipata pata vipi hadi zidaiwe namna hii? Aibu kubwa sana hii. Na usikute zimefanyiwa 'mkurabita' zamani.
ReplyDeleteNimeona mkuu, ni kweli unajua ukiwa na jirani halafu kila siku unagonga kuomba chumvi atakudharau. Tumezidi kuwa omba omba na hiyo mipesa haimsaidii mtanzania ila hao viongozi. Naona aibu lakini tuna haki ya kuaibika. Sioni kosa lao kudai pesa zao kama kweli walitupatia maana haikutusaidia watanzania bali viongozi na familia zao.
ReplyDeleteWAAFRIKA NDUGU ZANGU TUANZE KUJITEGEMEA WENYEWE SASA,MISAADA HAMNA TENA,WAZUNGU WENGI HUKU NJAA NYINGI SANA...HAKUNA ULAYA YENYE AFADHALI KWA SASA HATA BABA YAO UINGEREZA IKO HOI SANA.
ReplyDeleteSisi tulipofika za kwetu kama ni za rada tulifanya sherehe kurudishiwa. Kama kuna mahali tunatakiwa kurudisha hela za watu na turudishe
ReplyDeleteNa mimi niliona na nikasikitika sana kuona hawa jamaa wanafanya mambo ya kudhalilishana. Tunaomba serikali yetu iombe maelezo juu ya ili swala maana ni swala zito mno, hawa jamaa hawawezi kuchezea bendela yetu ovyo ovyo.
ReplyDeleteMdau toka Italy
BANDUGU NI KWAMBA, HIZO HAPA ITALY KUNACHAMA KIMOJA KINAITWA LEGA NORD AMBACHO KINASIFA YA UBAGUZI SANA. SASA VIONGOZI WAKE WAMEWALIZA WAFUASI WAKE KWA KUDUNGUA BAADHI YA HELA KWENYE FUNGU LA CHAMA NA INAVYOSEMEKANA JAMAA WAMEGUNDUA KUWA HIZO HELA ZILITUMWA TANZANIA KWENYE INVESTMENT FLANI BILA MATAKWA YA WANACHAMA WAKE. SASA JAMAA KWA HASIRA WAMEAMUA KUANDAMANA NA BENDERA YA TANZANIA NA YA CHAMA CHAO WAKIONGEA MANENO MACHAFU JUU YA VIONGOZI WAO NA JUU YA TANZANIA. SASA MIMI KAMA MDAU NILIYOPO HAPA ITALY NIMEGUSWA SANA NA KLI JAMBO NA NAOMBA SERIKALI IFUATILIE KUPATA UFAFANUZI WA UCHEZEAJI WA BENDERA NA TANZANIA NA MANENO MACHAFU WALIYOKUWA WANAYASEMA KUHUSU TANZANIA.NAOMBA TUJADILIANE MASWALA YA MAANA NA SI KUONGEA VITU VISIVYO NA KICHWA WALA MGUU KWA MFANO WANAOSEMA TUMEZIDI KUWA OMBA OMBA!!ILO SIO SOLUTION SOLUTION NI KUTAFUTA NAMNA YA KUZUIA ISSUE KAMA HII ISITOKEE SANA!! WANGEKUWA WABONGO WANAKASHFU ITALY HUKO BONGO JAMAA WANGETUFANYIA FUJO SANA. ASANTENI!
ReplyDeleteMDAU MWENYE UCHUNGU NA TANZANIA KAMA MWALIMU NYERERE!
NAPENDA TUENDELEE KUDHALILISHWA HIVIHIVI LABDA TUTATIA AKILI NA KUANZA KUTUMIA MALI ZETU NA KUACHANA NA UOMBAOMBA.WATUTUKANE PIA ZAIDI NA ZAID ILI MKASIRIKE SANA.HAIINGII AKILINI NCHI INA KILA KITU,UNAACHIA WATU WANAKUIBIA KIZEMBE KABISA HALAFU KILA SIKU UKO MLANGONI KWAO KAZI KUOMBA TU.NDIO MANA HATA MAKAO MAKUU MLIHAMISHIA DODOMA ILI MCHUKUE UDHOEFU WA WAKINA MATONYA KWENYE SEKTA YA KUOMBA.MAMBAVU ZENU NYIE
ReplyDeleteNATUMIA CAPITAL LETTERS KWA MSISITIZO MTANISAMEHE WADAU, ILA WATANZANIA INABIDI TUAMKE SASA, NA TUSEME IMETOSHA.
ReplyDeleteMI NADHANI VIONGOZI TULIOWAWEKA WATUWAKILISHE WAMESHINDWA WANANCHI TUNA KITU CHA KUAMUA.
HEBU FIKIRIA HATA KAMA UNAFANYA BIASHARA NA WATU WA TAIFA HILO AU UNAOMBA SPONSOR YA KUSOMA WANAKUCHUKULIAJE?
WANAHABARI MMESHAPEWA PA KUANZIA FANYENI KAZI YENU HAYA MAMBO YAJULIKANE NA WANANCHI TUWASHINIKIZE VIONGOZI WALIOSHINDWA KAZI WATUPISHE, NGUVU TUNAYO, SABABU TUNAYO, NA UWEZO TUNAO. HEBU FIKIRI ISSUE YA MGOMO WA MADAKTARI HAWA JAMAA WAPO KIMYA KANA KWAMBA HAWAJUI JINSI WATANZANIA WANAVYOATHIRIKA.SHIME WATANZANIA KILIO NA MWENYE NACHO.
Tumezidi kuomba. Miaka 50 ya uhuru sasa tunatakiwa kuacha kuomba omba na kujitegemea. Uchumi tunao ila tunaufisadisisha wenyewe!
ReplyDeleteWewe Anony wa kumi toka juu usiwe mjinga, ukajilinganisha na mlima Kilimanjaro wakati wewe sio hata kifuu. Kwanza hapo juu hukueleza lolote. Umaficha ficha mambo: Kwa nini usiwaendee hao jamaa wanaoandamana na kuwauliza kiunagaubaga kuwa hizo pesa zilitumwa kwa nani hapa TZ? Hujui hata kufuatilia mambo harafu unasema unauchungu!!! Farasi wewe!!
ReplyDeleteAnony wa pili toka juu MAMBO NDIYO HAYOOOOOO.
ReplyDeleteMIPANGO SI MATUMIZI::::
ReplyDeleteTatizo kubwa nchini kwetu ni pesa kutumiwa kinyume na ilivyotarajiwa.
Wacha huko nje humuhumu ndani Bodi ya Mikopo inatenga pesa kwa Wanafunzi wa Elimu ya juu kwa Masomo, wanatokea akina Ester Budili na Wenzake wanaiba pesa wanajengea majumba na kununulia magari!
Sio mara ya kwanza Tanzania kudaiwa irudishe pesa za Msaada ,Norway iliwahi shinikiza fedha zao warudishiwe,,,Tanzania ilifikia kuwa na uhusiano mbaya na NORWAY kufuatia matumizi mabaya ya fedha za Msaada!
kutokana na maelezo yako cdhani kama ni nchi nzima yenye makosa. Kilichopo hyo investment ifuatiliwe na kama hzo pesa bdo zipo zirudishwe kwa wenye chama. Serikali yangu ya tanzania ni vyema mkanegotiate na hcho chama kwani wanachofanya c haki
ReplyDeleteWe anony Wed Jan 25, 05:12:00 AM 2012,
ReplyDeletefarasi mamako..fala tu wewe watu tupo hapa kujadili jambo la maana wewe unaanza kuja na kutukana watu as if hayo matusi unayajua wewe mwenyewe.Kama matusi kila mtu anayaweza na usijione kama unaakili wakati ni kifuu tu cha nazi tu kilichotupwa jalalani. Unalala chini ya mnazi halafu unajifanya unajua kutukana watu wakati kwenye hii blog yetu tukufu watu tunajadili mambo mbalimbali ya maendeleo.Pambavu sana!