Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaban Bin Simba Ofisini kwake jijini Dar es salaam leo. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ankal,

    Kuna viongozi wachache sana Tanzania ambao naridhika nao, na mmoja ni Mhasham Mufti Simba. Nimefurahi kumwona hapa kwenye blogu ya jamii.

    Mimi kama mwalimu na mdau mkubwa wa masuala ya elimu navutiwa na msimamo wa Mufti Simba kwa msimamo wake kuhusu suala hili. Anafahamu vizuri na anahimiza kuwa maendeleo yanatokana na elimu. Nami nilishaandika habari zake hapa.

    ReplyDelete
  2. Ma'ansha'Allah Mufti wetu anang'ara,,naona sasa ananafuu sana,,,,Mwenyezi Mungu akuja'alie maisha marefu yenye Afya tele Sheikh wangu,,,Ahlam UK

    ReplyDelete
  3. Mbele, hivi kwa nini watu hawako kama wewe? Yaani naona wewe hupenda ukweli na uwazi wa kweli.

    ReplyDelete
  4. Mbele unapenda kucoment mambo ya udini

    ReplyDelete
  5. mbele ame-comment ukweli. Udini ni kumbagua mtu kwa misisingi ya kidini.

    Mbele hajafanya hivyo, bali Mbele anajitahidi kufuta udini Tz na duninai. We uliyekomenti ndo unaonekana mdini kwani comment ya mbele imekuumiza. Unapenda u-hasi tuu.

    Mbele yuko mbele kutaka haki kwa woote bila kujali dini ili nchi hii iendelee na siyo kubaki tunabaguana tukidhani kwa kufanya hivyo ndo Mungu atafurahi na kutupeleka paradiso.

    Mfuatilie mbele utakuta anasema ukweli penye kuwepo hata kama unamuumiza yeye. Hilo huliwezi wewe.

    ReplyDelete
  6. Mbele unampenda sana Mufti Simba.Naomba umuulize shule zilizo chini ya taasisi yake ya BAKWATA inafanya nini katika hili.Mwulize kuhusu shule kama Al Haramain,Kinondoni,Jamhuri kule Dododa nk.
    Unampenda au unamkejeli au unatukejeli sisi wa imani yake?
    Hivi unajua kiwango chake cha elimu yoyote ile aliyo nayo?
    Hivi unajua historia yake kabla ya kufika hapa alipo?

    ReplyDelete
  7. Ndugu anonynous wa Jan 19, 06:00:00 unayeuliza kama namkejeli Mufti au nawakejeli watu wa imani yake, napenda kusema kuwa sina tabia wala wazo la kuwakejeli watu kutokana na imani yao. Nimeishi na watu wa dini mbali mbali, kuanzia Tanzania hadi huku Marekani, na nimeishi na watu wasio na dini. Sijawahi kuwakejeli au hata kuwazia kuwakejeli. Naheshimu imani za watu na nawaheshimu wasio na imani ya dini.

    Nimefundisha wanachuo wa dini mbali mbali, kuanzia Chuo Kikuu Dar es Salaam, ambapo nilianza kufundisha mwaka 1976. Waislam wengi nimewasomesha pale. Na utawakuta kwenye nyadhifa mbali mbali kuanzia Visiwani hadi Bara. Tafuta kokote nchini na duniani uone kama utamkuta mu-Islam yeyote atakayekuambia nimewahi kuikejeli imani yake. Nafahamu wewe ni binadamu na hutaweza kuwatafuta wote. Lakini basi, siku ya kiyama itakuja, na hapo ndipo mambo yatakapothibitika.

    Kinyume chake, kwenye hizi blogu kuna watu ambao wananikejeli au kunibeza pale wanaposikia kuwa mimi ni m-Katoliki. Yaani kuna watu ambao wanaamini kuwa kwa vile tu mtu ni mKatoliki, basi wanampakazia hili au lile. Hayo yamenisibu kwenye hizi blogu. Kama wewe ni mpenda haki na ukweli, ningeomba uwasakame watu wa aina hiyo.

    Kuhusu elimu, ni kwamba mimi, pamoja na elimu yangu yote ya vyuoni, daima nimekuwa na mtazamo kwamba babu zetu na bibi zetu walikuwa na elimu pana na ya kina ambayo haipatikani shuleni. Natambua kuwa hata mtu ambaye hajaenda shule anaweza kunifundisha mengi.

    Ukifuatilia historia yangu, utaona kuwa ninazunguka sana kutafuta elimu kutoka kwa watu hao. Nimejifunza mengi kutoka kwa wazee wa kiIslam kuanzia Lamu na Mombasa, hadi Zanzibar, baadhi yao wakiwa hawajaenda shule. Nimezunguka vijijini Tanzania bara, kuanzia Ukerewe hadi Mbinga, nikijifunza kutoka kwa wazee, wengine wao ambao hawakusoma hata darasa moja.

    Mufti Simba namhesabu kwa misingi niliyoelezea katika ujumbe wangu wa mwanzo, nikiwa ni mwalimu. Kama nilivyosema hapa juu, mtu anaweza kuwa ameelimika sana hata kama hajaenda shule. Na kuna wengi wameenda shule lakini hawajaelimika. Mimi mwenyewe, baada ya kusoma sana shuleni, na kupata shahada za juu kabisa, nilianza kujitafakari upya, nione kama nimeelimika au la. ndipo nikatambua umuhimu wa kutafuta elimu kwa wazee vijijini na watu wengine ambao pengine hawakwenda shule. Ndivyo ninavyofanya. Ningependa wengine waige mfano huo.

    Masuala ya hizo shule za wa-Islam sijayafanyia utafiti. Kutokana na hilo, sina haki wala wadhifa wa kuyaongelea. Nikijitia kuyaongelea, naona itakuwa ni kejeli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...