![]() |
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda |
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda leo (Jumapili, Januari 29, 2012) atakutana na madaktari waliofanya mgomo kwenye ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Madaktari hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wanaomba kuonana na Waziri Mkuu na mara zote Waziri Mkuu amekubali kuonana nao lakini hawakutokea.
Pamoja na kukubali huko kwa Waziri Mkuu, tarehe 25 Januari 2012 katika Mkutano wake na Wahariri wa Vyombo vya Habari aliwaomba Madaktari kuwa alikuwa tayari kuonana nao lakini hawakutokea.
Ili kuendeleza jitihada za kutaka kuonana na madaktari hao, Waziri Mkuu alituma Uongozi wa Serikali ukiongozwa na Mawaziri wa Afya na Ustawi wa Jamii; na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kuonana na Madaktari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Starlight tarehe 27 Januari 2012.
Kwenye Mkutano huo madaktari waliwasilisha malalamiko yao na kuomba kuonana na Waziri Mkuu. Kufuatia maombi hayo, Waziri Mkuu amewaandikia madaktari hao barua ya kuwataka kuonana nao leo, tarehe 29 Januari 2012 kwenye Ukumbi wa Karimjee, saa 4:00 asubuhi.
Kabla ya kufikia uamuzi huo, kulikuwa na mawasiliano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Uongozi wa Medical Association of Tanzania (MAT) na baadaye Mwenyekiti wa Muda wa Kamati ya Madaktari kuhusu mgomo wa Madaktari unaoendelea.
Aidha, Viongozi mbalimbali wa Serikali wamefanya mazungumzo na Wawakilishi wa Madaktari na Madaktari wenyewe kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Starlight ili kuweza kupata ufumbuzi wa matatizo yaliyowasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu anawasihi Madaktari wote kuhudhuria mkutano.
hili nalo lina sura nzito kama ngiri huh!
ReplyDeleteKuna habari kwamba MAT wameahirisha mazungumzo kwa kuwa walichelewa kupewa taarifa; baadhi ya madaktari wapo mbali. MAT wameomba kukutana na W/ Mkuu kesho. Je kuna ukweli kuhusu hilo?
ReplyDeleteWewe anony wa kwanza wewe..acha kumtukana kiongozi/mzazi wetu.
ReplyDeleteDavid V
ANOY wa kwanza. shukuru Mungu umezaliwa jinsi ulivyo. tukisema Mungu akuadhibu kwa kukupa mtoto itakuwa tunapa adhabu mtu mwingine kabisaa. Hivyo Mungu akupe watoto wazuri kabisa kwa mtizamo wako. ila adhabu yako bado siwezi kumchagulia Mungu.
ReplyDeleteanony 1 muogope Muumba,fikiri kabla hujatamka kwani hakujiumba yeye
ReplyDeleteMadaktari hawakutokea kwani wengine wanakaa nje ya Dar na wasingeweza kufika kwa siku moja na ndio maana wakaomba mkutano wao ufanyike jumatatu, lakini PM yeye akatoa maagizo makali kuwa warudi kazini kuanzia leo vinginevyo watakaso kazi, Naomba ieleweke kuwa fani ya daktari ni tofauti na fani nyingine....madaktari wanaolazimishwa kurudi kazini ndo wakifika huko utasikia kapasuliwa goti badala ya kichwa, anaumwa tumbo kapewa dawa za malaria, nk. Ebu Serikali ijaribu kuwa serious katika hili.....
ReplyDelete