Waziri wa Nishati na Madini Mhe. William Ngeleja (wa nne kulia) akizungumza na ujumbe kutoka Sweden uliomtembelea kwenye ofisi za Wizara ya Nishati na Madini mapema mchana leo. Ujumbe huo uliongozwa na Waziri wa Biashara wa Sweden Dkt. Ewa Bjȍrling na Balozi wa Sweden – Tanzania, Bw. Lennarth Hjelmaker. Nia ya ujumbe huo ni kuangalia fursa za uwekezaji nchini hususan katika nishati jadidifu (renewable energy), mawasiliano ya simu na mitambo.
Balozi wa Sweden Nchini Bw. Lennarth Hjelmaker (wa tano kushoto) akisisitiza jambo mara ujumbe wa Sweden ulipofanya kikao na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. William Ngeleja (Mb.) kwenye ofisi za Wizara mapema leo mchana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. SWEDEN:

    Mzigo mkubwa abebeshwe Mnyamwezi, hawa Wa sweden ndio wa kupewa na kusaini nao mikataba ya miradi ya Umeme na sio Wahindi!

    ReplyDelete
  2. HAPA UMENENA, ACHANA NA WAHINDI, WAMALAYSIA NA MAKABURU, HAWANA MAADILI HAWA. FANYA KAZI NA WASEWDE, WANORWEY, WAFINN. HAWA MAADILI YAKO KWENYE DAMU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...