Bwana michuzi napenda kutoa ushauri binafsi kwa taifa langu hasa zana nzima ya kilimo kwanza.

Maoni yangu ni kwamba mashamba yaliyobinafsishwa pamoja na baadhi ya maeneo mengine yenye rutuba kuzalisha zao fulani warudishe serikalini ila viendeshwe na kusimamiwa na BUNGE.

BUNGE liandae kamati mbalimbali zisimamie kilimo hicho cha kisasa na kuwe na taarifa za mara kwa mara bungeni kuhusu ufanisi na maendeleo ya kilimo hicho.

Wabunge wawajibike vilivyo kuhoji na kutoa ushauri wao pia kutumia wasomi wetu vilivyo kufanikisha kilimo bora chenye tija.

Faida itakayopatikana kwa kuuza mazao nje, iingie bungeni na itumike kwa maendeleo ya majimbo yoote.

Sidhani kama tunashindwa, kilimo kwanza ni kwetu sisi tanzania,tuwajibike kama sisi. Naamini kabisa wabunge wenyewe wanaweza kusimamia vyema.

Mdau mwenzenu..
Wangaluke@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Mdau, kwa bahati mbaya aina ya wabunge tulionao na jinsi mijadala mbali mbali inavyoendeshwa na mchakato uliowaingiza bungeni ni wazi hawawezi kuaminiwa kupewa jukumu kubwa na wakalifanikisha. Ni bora ungependekeza kamati inayoundwa na wataalamu wa taasisi kama SUA.

    ReplyDelete
  2. Mdau Wangaluke na Dhana ya KILIMO KWANZA:

    Mawazo yako ni sawa kabisa kwa maoni yangu ya kuunga mkono kama hivi:

    TIJA:
    1.Kila kitu msingi wake ni tija au faida kwa kile kitakachopatikana.

    2.Zaidi ya Bunge kinachotakiwa ni kuwa ardhi itumike kwa ufanisi na sio kwa watu kadhaa kuihodhi bila matumizi huku wakiwepo wenye kuihitaji kwa matumizi endelevu na wasiifikie.

    Mfano kwa nchi kama Italy, Kenya na Malawi idadi kubwa imehodhiwa na Makabaila, Mabwenyenye na Mabepari kama msingi na rasilimali kwa kuwekea dhaman na kuombea mikopo Benki na kwa dhamana za mitaji kwa uwekezaji mbalimbali.

    Ukiwa unasafiri kutoka Dar Tanzania ukivuka tu Namanga kwenda Nairobi unakuta mbuga na uwanda ziko wazi hakuna hata kibanda , vile ni kuwa mwenye ardhi labda yupo jijini Nairobi au London UK anafanya shughuli zake au la ajabu unaweza kukuta maetumia ardhi ya Namanga au Kajiado kama dhamana kuombea Mkopo Benki Nairobi au London huku pesa inapotoaka nafanyia biashara jijini Nairobi na sio kuhusu uendelezaji wa mradi wa eneo alilotumia kuopata fedha za Mkopo.

    URATIBU/ USIMAIMI
    1.Katika Siasa ya Ujamaa na Kilimo cha Kisasa palikuwa na Uratibu wa Miradi ya Kilimo, hii ni kuwa panakuwa na usimamizi kuhusu kujua tija na maingizo ya matumizi ya ardhi husika.

    2.Usimamizi Ulenge sifa za Mtumiaji na nia ya matumizi ya ardhi, sio kuwa na umwezo wa kuhodhi ardhi tu.

    Sio mtu achukue ardhi bila matumizi nayo, au mtu awe na dira ya ukulima wakati akipewa ardhi na pesa anafanyia mambo mengine.

    KWA HAYO MAWILI MAONI YANGU BINAFSI KUUNGA MKONO DHANA HII NAFIKIRI YATAFANYA KILIMO KWANZA KUWA NA UFANISI ZAIDI.

    ReplyDelete
  3. Duu ukiwapa huo mradi na mafedha yakapita huko si ndo watajiongezea posho mara 50 wakidai kazi ni ngumu?

    ReplyDelete
  4. Kilimo kwanza iwe Kilimo kwanza kweli kweli, sio Kilimo kwanza halafu Pesa mkononi tu, kinafuata Jembe pembeni biashara mkononi!

    Wajanja wametumia sana Fursa hii ili kufikia malengo tofauti kabisa na Dira iliyokusudiwa,

    Katika Tasnia hii wamepatikana wawekezaji wa Makundi ya namna mbili kama hapo chini:

    Mifano:
    1.Watu wanajipanga wanaunda vikundi wanahodhi ardhi, wanaandika Michanganuao ya miradi, ile pu pesa imeingia wanagawana kundi linasuasua au linakufa kabisaaa kinachofuata kila mwanachama anatumia fungu lake Kijengea Bar, Pub au Hoteli badala ya kufanya miradi ya kilimo!

    2.Watu wanajipanga wanaunda vikundi wana hodhi ardhi, wanaandika michanganuo wanavuta pesa, wanatumia kwa mambo mengine ,muda mwingine wanaandika michanganuo mingine wanakuwa kila mara wanavuta kupitia kundi na Sera ya Kilimo kwanza!

    Panakuwa na hasara kubwa tatu,
    1.Pesa hazitumiki kama inavyostahili.
    2.Ardhi inahodhiwa bila kuendelezwa
    3.Kudumaa kwa maendeleo kwa miradi isiyotekelezeka na kukosa Tija au Faida!

    ReplyDelete
  5. La Muhimu zaidi ya Bunge, inatakiwa Uratibu na Usimamizi wa makini kwa kuwa Bunge ni Bwawa la Siasa kuliko Sayansi na Utekelezaji!

    Pawe na Sera inayoambatana na Kilomo Kwanza kuwa kila Mdau au Wadau wa Miradi ya Sera hii lazima wafanyiwe Ukaguzi wa Wataalamu wa Kilimo na Usimamizi wa Miradi, wafanyiwe Uratibu na wajieleze mara kwa mara walipofikia.

    ReplyDelete
  6. Hongera kwa mawazo ya maendeleo

    ReplyDelete
  7. Ankali tuwekee bei ya madafu pls.

    ikiwezekana tuwekee bei ya madafu kila siku maana sikuhizi unatubania sana blog hii inatusaidia sana kujuwa mauzo ya madafu huko nyumbani.

    mpiga boks ughaibuni.

    ReplyDelete
  8. Hii sio kazi ya Bunge kugawa faida kwa majimbo! kazzi ya bunge ni kuisimamia serikali iwajibike hivyo ni vema Bunge kama litaacha itikadi zao za kichama na kuungana ili waweze kuisimamia serikali kwa kina.

    Kila mwaka Bunge huidhinisha bajeti lakini hizo pesa zaenda wapi...ni wakati muafaka sasa wakaisimamia Serikali ikaongeza bajeti ya kilimo na waifuatilie!

    ReplyDelete
  9. nimeipenda hiimaada, ina wavuta zaidiwatanzania popote walipo kutoa maoni yao kuhusu nini kifanyike kuliendeleza taifa letu kupitia kilimo..hapa nimepata mengi na hasa namna watu wanavyojificha kwenye kilimo kwanza kula pesa za umma...yawezekana mawazo kama haya yakachukuliwa na kuboreshwa ili kufaidike nayo kuliendeleza taifa letu jamani...lakn naungana na baadhi ya wachangiaji ambao wanasema sekta muhimu kama hizi zisimamiwe na taasisi za kitaalam zaid kuliko makundi ya kisiasa maana wanasiasa nanachofikiria ni kujiongezea posho za alawansi za safari kuliko mambo ya maendeleo...we angalia jinsi walimu hasa wa shule za msingi wanavyotesa kwa pesa ndogo lakini waheshiwa wanataka posho ya siku moja izidi mshahara wa mwalimu wa mwezi mzima....kaazi kwelikweli.
    mungu ibariki tanzania na watu wake wawe na fikra chanya

    ReplyDelete
  10. Wazawa wapewe mashamba, wawezeshwe kulima kisasa chini ya usimamizi wa wataalamu wa kilimo kwa ujumla.(wataalamu wa udongo,umwagiliaji, mifugo,sayansi ya chakula na usindikaji,masoko n.k
    Bunge linaweza kusimamia ikiwa ni pamoja na kuhakikisha bajeti ya kufanikisha zoezi hilo inatengwa hasa kwenye maeneo ya uwezeshwaji wa wananchi wa kipato cha chini.Kwa mpangilio huu wataalamu wetu wa kilimo watatumika ipasavyo,hali ya uchumi kwa wakulima itaboreka pamoja na uchumi wa nchi.Tutazalisha mazao ya kutosha pamoja na kuuza nje mazao yaliyosindikwa kwa thamani zaidi.

    ReplyDelete
  11. Kazi ya Bunge ni kuwakikilisha wananchi, kutunga sheria na kuisimamia serikali. Haya ndio majukumu ya msingi ya Wabunge na Bunge, kama mashamba hayaendelezwi maana yake ni kwamba Bunge limeshindwa kuisimamia serikali kutekeleza sera. Suluhisho hapa si kuwaongezea majukumu wabunge kwani kazi zao za msingi na wenyewe walishazishindwa. Dawa hapa ni kuwatimua Wabunge, Bunge na Serikali ili tuanze upya.

    ReplyDelete
  12. kuwapa majukumu hayo mwabunge ni kichekesho , kwani wabunge wangapi wanalima ,najuwa kila mbunge kahodhi ardhi kubwa , sasa jiulize au waulize kwa hiari yao kila mbunge alivuna mazao gani mwaka jana ??? hapo utajuwa kama sera za kilimo kwanza inafanya kazi ???
    plan B labda serikali iwape ruzuku wabunge za kulimia watachangamka ile mbaya , halafu wakati wa mavuno tufanye hesabu ya pesa iliyotumika na mazao yaliyovunwa ya kipimwa kwa bei ya sokoni ,jibu HASARA TUPU , plan C tujiulize mapesa ya JAKAYA ya kilimo kwanza yameleta faida gani ???
    sera za kilimo kwanza ni nzuri kama unavyosikia nyimbo ya Taifa , sijuwi wataalam wa uchumi wetu huwa hawajuwi kupanga ?? leo bagamoyo tunalima mananasi hadi yanaoza hakuna mteja asilimia 40 ya matunda yanaoza na bei unayouza ni sh 500 kila nanasi ni hasara tuu , hii ni kwa sababu hakuna miundo mbinu ya kuhifadhi bidhaa za kilimo iliziweze kusafirishwa nje
    Tanzania juzi serikali tumepata pesa mpya ya kuendesha KILIMO KWANZA.
    USHAURI SAHIHI MAJUKUMU YA KILIMO KWANZA KAMA TUNATAKA KUFANYA MAPINDUZI YA KWELI PESA ZOTE ZIPELEKWE KWENYE VYUO VYA KILIMO NA VYUO VYOTE VYA KILIMO TANZANIA VILIME NA KUONESHA MFANO KWA WANNCHI NA VIWEZE KUJIENDESHA KIUCHUMI KWA MAPATO YA KILIMO .TUKIFANIKISHA HAPO PLAN B IENDE KWENYE MAGEREZA YOTE YA TANZANIA ZOEZI HILI HUKO MAGEREZA LISIMAMIWE NA WATAALAMU WA VYUO NA LIKIFANIKISHA HUKO , KILAMFUNGWA AKITOKA HUKO ANAPATIWA ARDHI YA KULIMA ILI AWWEZE KUJIKIMU NA PATO LA TAIFA KUONGEZEKA

    ReplyDelete
  13. Kwa mdau hapo juu , ambaye unataka kujua bei ya madafu huko nyumbani angalia hii blog ; http://moneylondon.over-blog.com/
    utapata bei ya madafu na fedha za kigeni kila siku.
    Asante.

    ReplyDelete
  14. Mdau naheshimu mawazo yako lkn sikubaliani nayo kabisaaaaaa! Ukitaka kujua kajifunze Korea Kaskazini ndiyo utajua unachikion gea kama ni sahihi au hapana

    ReplyDelete
  15. Hapa tumeona kwamba taifa letu TZ limechagua tegemeo la maendelo ya uchumi kwa wananchi as KIlimo kwanza kama UTI WA MGONGO.
    Je hicho kilimo kinategemea hasa factor gani?.Jibu ni Maji lazima yawepo ili mtu ulime popote pale utakapo.Je maji yapo au yatapatikana na kama hayapo na hayapatikani je Serikali au TZ inauwezo wa kutegemea KILIMO? kama chanzo kikuu cha maisha ya MTZ?.Jibu ni hapana.Mfano JK alisema awezi kufanya mvua inyeshe.Kwani ni dhahiri kuwa Kilimo kinategemea maji na maji hayo niya mvua.
    So lazima Nchi ibadilike kutokana na mabadiliyo ya uchumi na factors mbalimbali duniani.Kipindi hicho maji yalikuwa yanapatikana kwa wingi ni sawa kulikuwa na kilimo kwanza ila kwa sasa hivi dunia imebadilika na watu nao wabadilike.Tuwe na tegemeo lingine e.g viwanda,Biashara,Madini,kilimo pia kiwepo.Watu waende shule,tufanye kazi zetu kitaaluma zaidi.Tuepuke errors or mistake zitakazo sababisha failure katika miradi yetu.Tuwe na error exceptions nyingi ili tuweze kuzivumbua any error which may arise or coming.God bless TZ

    ReplyDelete
  16. WATANZANIA NI WAVIVU.TUNAPENDA KUVAA MIVIATU MIKUBWAA NA MITAI. TUPIGE KWANZA KAZI. NA VIONGOZI MUSIWE WAROHO WAMADARAKA NA KUJISOMBEA ARDHI.HAWA VIONGOZI WANAJUA WANANCHI NIWAJINGA NDIO MAANA WANATUENDESHA KAMA WALEVI. INAUMAA SANA.LAKINI...

    ReplyDelete
  17. We tried back in Nyerere era, was called "Vyama vya Ushirika" how that turned out? Farmers were forced to sell their products to the Government only. And Government was too slow to pay them, you have to bribe somebody to get a cheque from Vyama vya Ushirika; as a result they ended up stocking up their crops. Because they didn’t want to to business with the government, which led to farmers started to ship out their product to the neighbouring countries. We were eating "ugali wa njano" while Mbeya have enough stock of maize to feed the whole country. Then came "Uhujumu Uchumi"...when Mwinyi became a president, first thing he did as president was to allow farmers to sell their crops to anybody. Here your solution will not work at all…

    ReplyDelete
  18. mi nadhan mdau upo sawa, kwa kuwa bunge ndio chombo cha kusimamia serikali? Kwa nn washindwe kusimamia kilimo ili kama ni lawama wapewe wao kama bunge sio kama serikali kwa ujumla wake. Mi naona wabunge wawajibike

    ReplyDelete
  19. jamani wapendwa ,leo nawaombeni tujadili utumiaji kuni na mkaa hasa kwa wakazi wa Dar ambako nishati hii inatumika sana . waziri wa misitu Ndugu Ezekiel maige ametoa hoja safi ya kuifanya nishati hii ipatikane kwa urahisi zaidi ili iwape changamoto wazalishaji umeme na gesi kuchakarika zaidi kibiashara ili nao wavute wateja au waifanye nishati ya gesi na umeme kuwa bei ya chini zaidi ya mkaa na kuni, maoni ya waziri ni kwamba huenda kama bei za gesi na umeme zitashuka kiasi cha kushinda mkaa ,basi watumia mkaa watahamia kwenye umeme na gesi na kuachana na mkaa na hapo ndipo mapori yetu yatakapojaa miti na labda na nyoka wa kumwaga. Je ?? ni kweli tannesco watakuwa na umeme wa kutosha ?? au gesi ya songo songo itashuka bei ?? yaani waache kujiongezea mishahara , washushe bei !! ndoto hiyo bana. Hongera waziri,never say never naomba tujaribu kuzalisha mkaa na kuni kwa wingi-labda tannesco watanyooka. mbali na hayo yote , mimi binafsi nina sayansi yakutengeneza majiko ya kutumia kuni tu ambayo hiyo kuni baada ya kuwaka unaendelea kutumia moto wake mpaka inageuka mkaa na bado unaendelea kuutumia kupikia. , siyo kununua mkaa uliochomwa tayari na ukiutumia unageuka majivu unatupa, hivyo unatumia mkaa mwingi sana kwa kazi ndogo na hii inasababisha kukata miti zaidi porini na kupanda kwa bei ya mkaa sasa hivi gunia linafika shilling 40 elfu hadi 50 sawa na mtungi wa gesi, niwezeshe waziri, tupo watanzania ambao hatulali- tatizo lenu serikali mnakimbilia China. ni mimi Zebedayo

    ReplyDelete
  20. BUNGE(KAMATI YA) KAMA KAZI YAKE MOJAWAPO YA KUISIMAMIA SERIKALI LINEGOTIATE MIKATABA YOTE YA KITAIFA IWE KILIMO AU MADINI KWASABABU SERIKALI IMESHINDWA KUSAINI MIKATABA YENYE MANUFAA. MIKATABA YOTE, KIFUNGU KWA KIFUNGU, IPITIWE NA KAMATI YA BUNGE KISHA BUNGE LIIPITISHE. TUKIFANYA HIVYO, MIKATABA MIBOVU YA UMEME, MADINI, NA HUU MBAYA UBAOKUJA WA MAKAA YA MAWE, MAFUTA NA GESI ITAKUWA BORA KIDOGO

    ReplyDelete
  21. Wabunge wakipewa Jukumu la KILIMO KWANZA,,,asalaleee nchi itafilisika!

    Jamaa walivyo na tamaa ya maslahi watataka nyongeza ya Mshahara kwa kazi hiyo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...