Wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya sekondari ya wasichana Korogwe wakiwa kwenye mahafali hayo huku wakiwa na majonzi makubwa kufuatia ajali iliyotokea shuleni hapo ambapo watu saba walijeruhiwa vibaya baada ya gari alilokuwamo mwanafunzi  mmoja kuwagonga kabla ya sherehe.
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta nchini Bw. Moshingi (kushoto) akimkabidhi madawati mkuu wa shule hiyo Bi Mauki sehemu ya madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 8.8 waliyotoa benki hiyo kuisadia shule hiyo, msaada huo umekabidhi shuleni hapo baada ya mahafali hayo.
 Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Posta nchini Bw. Sabasaba Moshingi, akizungumza katika mahafali ya shule ya sekondari wasichana ya Korogwe baada ya sherehe hizo kuendelea ingawa watu wote katika ukumbi huo walikuwa na majonzi makubwa kufuatia ajali ya wanafunzi nane waliogongwa na gari wakiwa kwenye uga wa shule hiyo. Wengine pichani ni Mkuu wa shule hiyo Bibi Annisia Mauki, mjumbe wa bodi Bw. Philip Mbaruku na kushoto ni Meneja wa benki ya posta Tanga, Bw. Warioba.
Mkuu wa shule ya wasicha Korogwe Bibi Annisia Mauki akisoma risala ya shule kwenye mahafali hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Posta nchini Bw. Moshingi (kulia) na kushoto ni mjumbe wa bodi ya shule hiyo Bw. Philp Mbaruku.
Picha na Mashaka Mhando wa Globu ya Jamii,Tanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...