Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limesema kuwa litawaalika mabingwa wapya wa Kombe la Mataifa ya Afrika, timu ya taifa ya Zambia 'Chipolopolo' katika mashindano yake ya Kombe la Chalenji mwaka huu ambayo huenda yakafanyika nchini kwa mara ya tatu mfululizo.

Maamuzi ya mwisho kuhusu mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Chalenji yataamuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambao watatakiwa kusaka wadhamini wengine washiriki huku Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), inayomaliza mkataba wake wa miaka mitatu mwaka huu ikiwa na nafasi ya kuchangia juu ya kuyabakisha mashindano hayo nchini.

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili kutoka Gabon, Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, alisema kuwa ameshampa taarifa Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Zambia (ZFF), Kalusha Bwalya kuhusiana na nia hiyo ya kuwaleta mabingwa hao kama sehemu ya kuzipa changamoto timu za ukanda huu.

Musonye ambaye alikuwa kwenye fainali hizo kama mmoja wa makamishna wa mechi mbalimbali alisema kwamba kushiriki kwa Zambia kwenye mashindano ya mwaka huu wakiwa na taji la Afrika kutawaongezea morari wachezaji wa timu nyingine ambao watatumia uzoefu wa vinara hao kukuza viwango vyao.

"Inajenga na inaimarisha timu pale wachezaji wanapokuwa wanajiandaa kwa mechi dhidi ya mabingwa wa Afrika au klabu kubwa, timu au yenye nyota wa kimataifa," alisema Musonye.

Alisema kuwa kama ilivyokuwa kwa TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliyoalikwa katika mashindano ya klabu ya Kombe la Kagame baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika, ndivyo mwaka huu watakavyojaribu kuwapata Zambia ili kutoa fursa kwa wachezaji wa ukanda huu kupata uzoefu kutoka kwao.

Alisema kwamba anaamini Zambia ambayo ni mwanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Kusini mwa Afrika (COSAFA), itatoa maandalizi mazuri pia kwa timu ambazo zitakuwa zimefuzu kushiriki fainali zijazo za Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika Januari mwakani nchini Afrika Kusini.

Tanzania ambayo iliyokuwa mwenyeji wa mashindano ya Chalenji mara mbili mfululizo, ilitwaa ubingwa mwaka juzi lakini ‘ikachemsha’ mwaka jana baada ya kuishia katika hatua ya nusu fainali na mwishowe kombe likatua kwa Uganda ‘The Cranes’.

CHANZO: NIPASHE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kwa nini wabongo tusipate wivu wa kimaendeleo na kujenga taifa stars ili angalau tuweze kushiriki katika haya mashindano.

    ReplyDelete
  2. Hawa watoto wa Zambia tukikutana nao lohh watatuchakaza bao hadi 110 yaani kila mchezaji wa Taifa Stars mabao 10 kuanzia Kipa hadi namba 11,,,!

    Tukikutana nao naomba Kaseja weka mpira kwapani tuwaachie pointi 3 ili tusiumbuke Nyumbani mbele ya Raisi wetu, ni vile Wachezaji wetu Majeba na wao Zambia Wadogo wadogo,,,!

    ReplyDelete
  3. Waje kushusha viwango vyao?(Natania!)

    David V

    ReplyDelete
  4. wakija tunawafunga na mpira wetu huu wa kubutua, hata mkibisha lakini ndivyo itakavyokuwa

    ReplyDelete
  5. Itakuja timu ya vijana tuu akina Katongo na Mayuka hawawezi kuja. hawa CECAFA wanawaza pesa tuu kuwa watu watajaa ila nina hakika kabisa haitakuwa Zambia ya AFCON.

    Mzozaji

    ReplyDelete
  6. Mchagga ni mchagga tu hata ukimpeleka chuo cha kumpenda mkewe akahitimu, akirudi ni yaleyale mke kwake ni trakta tu

    ReplyDelete
  7. Ahhh Zambia watatufunga mabao kama Basketi Ball au Neti ball!.

    Wanaweza turuhusu tucheze kwa miguu na mikono na wao kwa miguu tu pamoja na hivyo lakini wakatufunga pia!

    ReplyDelete
  8. Itasikitisha sana kama tutakutana nao Zambia watatufunga mbele ya JK Raisi wetu Mpendwa aliyejitolea kila hali kuhakikisha Timu isonge mbele matokeo yake jitihada zake anashuhudia anavuna mabua!

    ReplyDelete
  9. Yaani Bongo sasa imekuwa ni mwenyeji wa kudumu wa Chalenji?

    ReplyDelete
  10. Mdau wa 9 Anonymous Thu Feb 16, 07:47:00 PM 2012

    Bongo imekuwa mwenyeji wa kudumu wa Chalenji,,,hiyo ni dalili tosha kuwa Bongo uwezekano, Bongo tambarale!

    Hii ndio unakuta unaandaa Ubwabwa unakaa kwenye nafasi ya 'Uandazi' (yaani kugawa sinia) mwisho unakuta Ubwabwa umeisha Jikoni unaambulia patupu!

    Hii inaonyesha Wabongo maisha hayatukamata sana kwenye kuyakimbiza, tuna muda mwingi wa social than commitment ukilinganisha na wenzetu majirani!

    ILA BAHATI MBAYA MPIRA HATUUWEZI TUMEBAKI NA USHABIKI WA MAGAZETINI NA VIJIWENI!

    ReplyDelete
  11. Watanzania Ushindi wetu wa Mpira ni wa MAGAZETINI na VIJIWENI kwa kutaja listi kwa misingi ya Majina na sio Viwango wa wachezaji,,,kama alivyokuwa Mmarekani anashinda vita ktk sinema za Hollywood tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...