Mojawapo ya picha za mwisho mwisho za Mwimbaji/mwigizaji Whitney Houston ikionesha akitoka kujirusha na marafiki zake katika kiota cha Tru Hollywood jijini Los Angeles Alhamisi usiku
Mwili wa Whitney Houston ukiondolewa katika hoteli ambako inasemekana alikufa akiwa bafuni
Waombolezaji wakiwa wameweka maua na ujumbe wa kumkumbuka Whitney. Chanzo na habari kamili BOFYA HAPA
Kunradhi: Mapema usiku huu ripota wa zamu wa Globu ya Jamii aliweka kimakosa picha na habari kwamba Whitney Houston yu hai bado. Ukweli ni kwamba msanii huyu hatunaye tena na mashabiki wake dunia nzima wanaomboleza. Baada ya kuiondoa haraka habari hiyo, tunawataka radhi wadau kwa usumbufu kutokana na habari hiyo ambayo ilitokea mwaka 2001 na kurushwa hapa leo kwa bahati mbaya -Michuzi
Mwenezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Tutaendelea kumkumbuka kupitia nyimbo zake tamu. Ametanguli nasi nyuma yake. TAUS KINGI
ReplyDeleteSawa na kifo cha mvuta bangi mtaani tu; wote walipaswa kujua madhara ya madawa ya kulevya! Ama kwa kuwa huyu maarufu?
ReplyDeleteEEh jamani. Hata waliokufa mnawanyanyasa. Watanzania too much.
ReplyDeleteTulimpenda na kumkubali sana kwa kupitia music, na sio mihadarati.......kwani ilikuwa ni kitu personal tukinachompa stimu. Mchango wake ktk jamii ulikuwa ni kuimba nyimbo zenye ujumbe maridhawa. Kwa hiyo mnaomponda jaribuni kusikiliza songi zake........achaneni na ile midude aliyokuwa akifakamia, kwani ktk verses zake hakuwahi kuitaja!! RIP shem
ReplyDeleteNashukuru Michuzi kwa kuweka mambo sawa. Ila huyo repoter wa zamu inabidi awe makini na uletaji habari kuepuka kuwachanganya wasomaji. Hata hivyo tunashukuru kazi nzuri mnayoifanya kutujaza mambo mengi ya kitaifa na ya kimataifa!! Keep it up!!
ReplyDelete