Mbunge wa Bumbuli Mh January Makamba akifafanua jambo ndani ya kipindi cha Jahazi cha Clouds FM kuhusiana na hoja yake binafsi aliyoitoa hivi karibuni, ya kuliomba Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania liazimie, kwa kauli moja, kuitaka Serikali, katika Mkutano ujao wa Saba wa Bunge, kuleta Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Upangaji wa Nyumba za Makazi (Rental Housing Act):

1.Itakayoweka utaratibu na udhibiti wa sekta ya upangaji wa nyumba nchini kwa ujumla,2.      Itakayowezesha kuanzishwa kwa Wakala wa Udhibiti wa Sekta ya Nyumba – Real Estate Regulatory Authority (RERA),3.Itakayoainisha wazi haki na wajibu wa wapangaji na wenye nyumba,4.Itakayoweka utaratibu wa haraka na rahisi zaidi kwa wapangaji na wenye nyumba kupata haki zao,5.Itakayodhibiti na kuweka adhabu kwa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wapangaji,6.Itakayoweka utaratibu wa ukaguzi wa viwango na hali za makazi ya kupanga,7.Itakayozuia na kuweka adhabu kwa utaratibu wa kutoza kodi ya nyumba kwa miezi sita au mwaka mzima.
Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kutoka Clouds FM,Ephrahim Kibonde akitaka kupata ufafanuzi zaidi kutoka kwa Mh January Makamba kuhusiana na Sheria ya Kudhibiti Upangaji wa Nyumba za Makazi (Rental Housing Act),shoto kwake ni Kilaka Wasi wasi Mwambulambo.
Watangazaji wa Kipindi cha Jahazi cha Clouds FM wakifanya mahojiano mafupi na Mh January Makamba kuhusiana na masuala mbalimbali ama mchanganuo wa Sheria ya Kudhibiti Upangaji wa Nyumba za Makazi (Rental Housing Act).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. wadau hiyo picha imekaaje? makamba ndio mtangazaji au kibonde ndio mtangazaji mbona kama kichwa chini miguu juu

    ReplyDelete
  2. Clouds fm ni radio inayotuabalisha mengi watanzania tulio nje ya nchi na ndani ya nchi.Kwa hili nawapa hongera sana mr Kibonde.
    Pili nawashukuru wabunge vijana ambao wanatimiza ahadi zao na wajibu wao kutuabalisha watanzania ndani na nje ya nchi juu ya mambo mengi ambayo ni endelevu kwa Taifa letu,hususani Zitto,Makamba,na wengineo.
    Ombi langu la dhati:
    Tunayoyaona kupitia media outlets yawe ndiyo mkakati wetu hata tukiwa tunafanya majukumu yetu mbalimbali tuliokabidhiwa na jamii.Nakuja!

    ReplyDelete
  3. TATIZO NAONA MAKAMBA JANUARY ANATAKA KULETA MAMBO YA AMERICAN SISI TUMEZOEA KIBONGO BONGO! MAMBO YA MWEZI MWEZI YAMEPITWA NA WAKATI BONGO SIYO KAMA MAREKANI SISI PESA IPO NYINGI TUNAWEZA KULIPA HATA MIAKA SITA KWA MKUPUO DEAL NI NYINGI NA WATU PESA IMEJAA SASA KAMA MAKAMBA HUNA CHA KUONGEA BUNGENI USITULETEE MAMBO YA MAREKANI HAPA.

    ReplyDelete
  4. unaleta hoja amabayo serekali yenyewe haiwezi kukidhi nyumba. kwanza wakidhi nyumba za viongozi badala ya kuishia kukakaa kwenye mahoteli na kuwaumiza raia majasho yao.

    ReplyDelete
  5. Na swala la upangaji wa NHC kalizungumziaje?,,,Maana kama ni haki sawa kwa mpangaji na mpangishaji!Naona wapangaji wa miaka nenda rudi NHC wangeangaliwa kwa jicho la huruma,,,Wapo wengi wao wamepanga nyumba hizo na ni mbovu kwa miaka zaidi ya 40,,Je serikali bado inataka waendelee kupanga eti mpaka watakapojengewa zingine za kuwauzia?,Jamani kwa hakiza binadamu,hiyo kweli ni sawa?Mtu unapanga nyumba mpaka unazeekea humo,kisha eti wajenge wakuuzie,,Kwa shilingi ngapi,au kwa muda gani wa kudaiwa huwo mkopo wa nyumba?Jamani kusema kweli haya ni mauwaji,,kutofikilia haki za binadamu,,,Tatizo WaTZ hatuna umoja na moyo wa Imani,Tungeweza kushirikiana hao watu wakauziwa nyumba hizo,,maana kodo zao zilishajenga nyumba kibao za NHC,Mtu usikae kusema 'Kwa nini wao wauziwe,eti kwa kuwa wewe huishi katika nyumba za NHC,,Mimi mwenyewe siishi katika nyumba hizo lakini nawaonea Imani mno hao wapangaji wa NHC.
    Ahlam,,,UK

    ReplyDelete
  6. Hiyo sheria ya Makamba inaelemea upande moja, inawapendelea wapangaji zaidi kuliko wenye nyumba. Nadhani Makamba angeangalia wenye nyumba pia kwani nao wametumia investment kubwa mpaka nyumba kusimama. Ni gharama kubwa sana kujenga nyumba kuliko ambavyo wengi wanavyofikiri. Sheria ya leo na ambayo Makamba anaitaka inadidimiza kabisa wenye nyumba. Tuangalie na kuweka balance ili kuwe na win-win situation bila upendeleo, mfano sheria haisemi adhabu ambao anatakiwa kupewa mpangaji anapokataa kulipa kodi au anapokataa kuondoka kwenye nyumba (to vacate),au anapofanya uharibifu kwenye nyumba. Ningependa kumkumbusha Mhe. Makamba kuwa wenye nyumba pia ni raia kama raia wengine wa nchi yetu ambao wanapaswa kulindwa, Siyo kwa sababu wanamiliki nyumba ni mafisadi, ieleweke walifanya kazi kwa kadiri ya uwezo wao na kumudu kujenga nyumba zao. Navyofikiri Makamba anatafuta support kutoka kwa majority, lakini aangalie na haki za owners pia.

    ReplyDelete
  7. Na wenye nyumba wakiamua kugoma hawapangishi nyumba zao ana pakuwaweka hawa raia. hali halisi ya maishi ya Tanzania ni tofauti na hali halisi ya marekani.
    unafikiri watu kuchukua kodi ya miezi sita ni wajinga? Tanzania mtu anakuja kupanga kwako hana address hata uaribifu ukitokea huna pa kumpatia lakini marekani kuna social security number ambapo mtu akienda kupanga nyumba na kufanya uharibifu au kukataa kulipa kodi ile namba yake itambana information zake zitapelekwa kwenye credit bereaue ikishafika huko ina affect score zako kwa hiyo unakuwa huwezi kupata nyumba tena, hupati mkopo, yaani kwa kifupi unakuwa umebanwa.

    ReplyDelete
  8. haya anayoongelea ni kujipendekeza kisiasa kwa wananchi na hili lisipoangaliwa vizuri litaibua vuguvugu la migogoro mikubwa na kusababisha watu wengi kukosa makazi.

    kwa kuwa Bumbuli bado hapajajengeka kama mijini angehakikisha miundo mbinu ya Bumbuli pamoja na ujenzi vinakaa kwa mpangilio madhubuti alafu aintroduce system ya proper address kwa kila mwana kijiji kijijini kwakwe, apeleke computer za kutosha na umeme awawekee ili kazi zisishindikane kufanyika, aweke na mawakala wa upangishaji, a set up credit bureau hii itamfanya mwenye nyumba yake awe secured na wakorofi wasiotaka kulipa kodi na waharibifu apeleke na insurance companies ambazo watu wata insure nyumba zao, akimaliza nyumba zitakazo jengeka huko ahamasishe na kutilia mkazo watu wapangishwe mwezi mwezi baada ya hapo akiona hii imefanya kazi ailete mjini na hapohapo aweze kuwapa wananchi wake mbinu za kipato ile wawe na uhakika wa kupata kodi ya kila mwezi.

    ajaribu kwanza kwa hili eneo dogo tuone huu utaratibu utachukua muda gani??????


    Faty baby.

    ReplyDelete
  9. mimi sielewi swala la upangaji wa nyumba na umiliki au uuziwaje baadae wa nyumba vina wiyana vipi? Nyumba za serikali ziendelee na zibaki kuwa za serikali kwa kuwa nimekupangishia nyumba yangu umekaa muda mrefu ndio unadai haki ya kuuziwa nyumba?

    Ahlam hebu fikiria hili vizuri tena halafu urudi tena hapa kunielewesha. Mfano wale watu waliopewa nyumba za kukaa pale ngarenaro Arusha na kodi ilikuwa haifiki hata elfu tano kwa mwezi hiyo kweli utasema ilitosheleza kujenga nyumba? hizo pesa zingine za biashara walizokuwa manaserve kwa muda wote hawakupanga mipango mizuri ya baadaye? NHS imeeendesha mradi wa nyumba kwa hasara kwa muda mrefu mno!!!!!!!!!!!

    We need change.

    ReplyDelete
  10. Mdau uliyezungumzia NHC unataka waTanzania waungane ili wawatetee nyie msiojua maana ya kulipa kodi?Kama nyumba mbovu si mhame kuna nyumba kibao huko mtaani mkajaribu kupanga! Acheni hizo, nyie mnatunyonya tu kwa kodi zenu kiduchu mnazolipa halafu mnataka siye tuwatetee?

    ReplyDelete
  11. achane kujipendekeza nyie.mnajifanya mnataka kuwasaidia wasiokua na nyumba kimaneno muonekane na nyie mnaneno.huwezi kuifanya nchi ya Tanzania kama ulaya kama kweli unataka kuiweka hyo hoja yako kwanza anza na miundombinu kwani maendeleo yamekuja kabla ya miundo mbinu.sio unalala unaamka unapeleka vitu visivyoeleweka bungeni.kwanza serikali ianzishe mladi wa nyumba na kuanza kuweka hizo system zenu za ulaya tuone itakuaje

    ReplyDelete
  12. Hoja imekaa vyema ila nikweli kuwa haiangalii wenyenyumba kwa upande mwingine.

    Makamba ukija na hoja hii tena bungeni, tafadhali ongezea kifungu hiki;-

    -Nyumba za NHC zote za mjini hasa za DSM, kama Posta, Faya, Kitumbini nk mbona zinakaliwa na watu wa asili ya asia tu, au ni mpangoi wa serikali? Hawapo keko, hawapo temeke, hawapo ubungo...pole mimi!

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  13. Sawa kabisa mdau unayetaka balance kwenye sheria hii. Mpangaji akikataa/akichelewa/akiondoka bila kulipa mwenye nyumba atapataje haki yake?. Makamba afahamu kwamba nchi hii hakuna credits record wala hakuna address system, mtu akitoka mlangoni hujui utampata wapi tena.

    Kulipia muda mrefu ni insurance against this risk. It is a premium we pay because we are so backward that If a tenat walk out of the house without paying, there is no possibility to recover the money.

    David M

    ReplyDelete
  14. Makamba afanye utafiti, asikurupuke. Sheria anayoitaka ilikuwepo, ikiitwa Rent Restriction Act ya mwaka 1964. Sheiria hii iliweka mazingira ya kumlinda mpangaji lakini ilifutwa mwaka 2005 kwa madai ya "liberalization". Kwamba upangaji utawaliwe na nguvu ya soko. Sasa mheshimiwa si anaturudisha tulikotoka? Waloifuta ile sheria si ndo hao hao? Watakubali kuirudisha?

    ReplyDelete
  15. Huyu Makamba watu wanaenda mbele yeye anarudi nyuma.

    ReplyDelete
  16. Nyie mnaosema eti hakuna addtress system sijui nini nadhani hamjasoma vizuri huu walaka wa mh January. Kwani si mpangaji anakuwa analipa monthly then kama hajalipa kwa mwezi husika then wewe mwenye nyumba unabaki na nyumba yako na fedha za deposit ambazo huyu mpangaji anatakiwa kuzilipa during commencement of the contract (mwanzo wa mkataba. Sasa tatizo liko wapi hapo??? Na kwa taarifa yenu watu wengi wanaopanga maeneo mengi karibu namjini ni wafanyakazi ambao wana address za maofisini kwao. Hii hoja ni nzuri sana ya mh Makamba na inamlenga mtanzania wa hali ya chini/ kati.

    Nashauri msome hiyo proposal vizuri kwanza na kuacha pokopoko zenu bila hoja za msingi.

    ReplyDelete
  17. Sasa kwa mfano wewe anon wa Wed Feb 15, 09:43:00 AM 2012.

    Kwani wasi wasi wako ni nini??? Subiri tu hao wenye mamlaka wakatae kuiruhusu bas. Tuko watanzania wengi tunaopanga na pia tuna nyumba tunapangisha, hii mada inatugusa sana na tunaiona ya msingi sana.

    ReplyDelete
  18. Anonymous 09:43 Am 2012, nikuerekebishe siyo Rent Restriction Act ya mwaka 1964 ni ya mwaka 1984 na kwewli baada ya Trade liberalisation ndo ikaenda na maji.Tanzania sheria zipo ila utekelezaji wake huwa hauko sawa. Na pia utingaji wa sheria uangalie hali halisi y amasiha ya watu na si ku-copy kutokana na sheria za nje especially Uingereza.

    ReplyDelete
  19. Mbona na mahojiano na Zitto hujaweka?

    ReplyDelete
  20. Nadhani lilio muhimu ni kuweka balance katika hiyo sheria ili wapangaji na wenye nyumba wote waweze kupata hai iliyo sawa. Ni kweli suala la nyumba linatawaliwa na hali ya soko lakini ikumbukwe kwamba tatizo kubwa tunaloliona sasa hivi ni kwa wenye nyumba kutaka kurejesha pesa zao walizotumia kwa muda mfupi ilhali katika suala hilo ni kwamba ili kurejesha mawekezo yao inatakiwa kuchukua muda mrefu. Hivyo nina muunga mkono mehshimiwa makamba katika suala hilo alilolianzisha ila ninachomsihi ni kuwa ufanyike utafiti wa kutosha ili haki iweze kupatikana kwa watu wote.

    ReplyDelete
  21. Nimejifunza mengi toka kwenu nyie wote wachangiaji maoni, kwani mengi sikuyajua kuhusu upangishaji bongo, kidogo sasa napata mwanga, asante.

    ReplyDelete
  22. WEE BRO MIMI NI MTANZANIA AMBAYE NAISHI HOLLAND , HOJA YAKO NAONA KAMA UMETOKA USINGIZINI, KWANI WEWE KAMA KIJANA MPYA WA KITANZANIA NA KIONGOZI MTARAJIWA SIDHANI KAMA MKURUPUKO HUO UNA MANTIC. WEWE UNAJUA 100% KUWA TANZANIA HATUNA DATA SYSTEM, BADO SANA KATIKA DIGITAL LEVEL. WEWE KAMA UNGEKUWA NA NYUMBA UNGETHUBUTU KUMPANGISHA MTANZANIA AMBAYE HUNA UHAKIKA NAE JINSI GANI ANAVYOWEZA KULIPA RENT YA NYUMBA YAKO. HUANA UHAKIKA KAMA ANA INSURENCE, AU ANA UHAKIKA WA KUKULIPA WEWE PANGO KILA TAREHE 1 YA MWEZI. WALIMI HAPO TU WENGINE HAWAJALIPWA MISHAHARA YAO WALA HAIJULIKANI NI LINI WATALIPWA HALAFU WEWE UKAMPANGISHE MTU HUYO ! KUMBUKA NA WEWE KAKA MZAZI UNASOMESHA WATOTO NA UNATEGEMEA PESA HIZO NDIO ZA KUWALIPIA WATOTO WAKO SCHOOOL FEEZ, HALAFU HUJALIPWAAPAKA MWALIMU APATE MSHAHARA WAKE NDIO AJE AKULIPE, HIVYO NA WATOTO WAKO WAFUKUZWE SHULE? KW3A SABABU HUNA PESA YA ADA.FIKIRIA KAKA KWANZA KABLA HUJAKURUPUKA KUTOA MADA NA NINI UNACHOTAKA CHANGIA ! WATANZANIA SIO WAJINGA ATI WANAOMBA PESA YA PANGO IN ADVANCE ,KWANI WAPANGAJI WENGI HAWAAMINIKI , WAKIVUNJA KITU KATIKA NYUMBA YAKO WEWE UTAJITENGENEZEA ? AU HUJUI SHERIA ZA UPANGAJI WA NYUMBA DUNIANI? HAYO MAWAZO NI SAWA ILA KWA NCHI YETU BADO SANA KAMA UMEFIKA MAREKANI UMEONA KILA MKAZI ANA JULIKANA NA SOCIAL SECURITY YAKE INAJULIKANA NA NANI MUAJIRI WAKE HIVYO NI KWAMBA MOJA KWA MOJA MWENYE NYUMBA ANALIPWA NA MUAJIRI WA MPANGAJI WA NYUMBA YAKO ,HIVYO UHAKIKA UNAO, SIO HAPO KWETU BONGO HATA MTOTO ANAZALIWA LEO HOSPITALI HAKUNA BIRTH CERTIFICATE. MPAKA UFUKUZIE UKATOE RUSHWA VIZAZI NA VIFO NDIO UANDIKIWE YA FAKE! KWELI WEWE NDIO KIONGOZI MTARAJIWA UNA MAWAZO HAYO?NAONA BADO UNAWAJIBIKA KURUDI SHULE KUONGEZA ELIMU ULIOKUWA NAYO NAONA NI FINYU MNO.
    NCHI YETU HATA MITAA HAINA MAJINA SASA WEWE MPANGAJI UTAMANGISHA KWA ADRESS GANI? HAPO MATAPELI WAKO KAMA UTITIRI: NIGERIA CAMEROON, SENEGAL,WAKENYA , WAGANDA ,WACONGO NA WAZAIRE AMBAO BADO HAWAJASTAARABIKA KABISA, KWELI WEWE UNAWEZA WAPANGISHIA NYUMBA YAKO WATU KAMA HAO KWA MALIPO YA MWEZI MMOJA MMOJA? NA UKAELEWANA NAO? NDUGU YANGU HAPO NAONA UMEONGEA HEWA AU ULITAKA KUUZA SAUTI YAKO REDIONI,THATS ALL!
    PIGANIA KWANZA DATA ZA KILA MTANZANIA AJULIKANE NA WAPI ANAPATA MAISHA NA KILA RAIA AU MKAZI AWE ANAJULIKANA KATIKA NATIONAL DATA SYSTEM HAPO KIDOGO TUNAWEZA TUKAKA MEZA MOJA NA KU DISCUSS HILO.

    NAMALIZIA NA KUWASHAURI WENYE NYUMBA MSIKUBALIANE NA WAZO HILO KATUKATU. KWANI BADO SANA KWA SISI WATANZANIA , LABDA ANOTHER 3 GENERATION TO COME

    HAPO TU STUDIO ULIPO, HAWANA DATA.
    WAULIZE HAPO MBARAKA MWINSHEHE WA MOROGORO JAZZ KAFARIKI TAREHE GANI NA SAA GANI KATIKA AJALI GANI NA GARI LA NAMNA GANI NUMBER PLATE YA GARI HAWAJUI WALA HAWAKUMBUKI SASA WEWE MJAMAA ANGALIA SANA TUNATAKA VIONGOZI SASA WALIOKUWA NA ELIMU YA KUTOSHA SIO KUBEBANABEBANA TU KINYEMELA!!!!!

    mdau AMSTERDAM

    ReplyDelete
  23. Asante sana kaka yangu makamba mi naona kuna watu wanaotoa maoni hawajajui nini kinachoongelewa.hili naomba kibonde ulizungumzie sana kwenye kipindi chakona kwenye radio yetu ya clouds maana sisi watu wa chini tunanynyasika sana kuhusu ulipaji wa kodi za nyumba .ninaomba lijadiliwe haraka iwezekanavyo na kama ni kuanza lianze rasmi iwe july mwaka huu wenye nyumba wanatupa wakati mgumu.tusaidieni tu tuweze kulipa kodi kila mwezi na si kwa miezi sita wala mwaka maana tunaangaika sana na wenye nyumba wanafanya tu maamuzi yao kupandisha kodi kila mara bila hata kuangalia ubora wa nyumba ukiuliza unaambiwa ciment imepata wakati nyumba ni ya mwaka arobaini na saba jamani naomba kila chombo cha cha habari kieleze huu utaratibu na magazeti yaandike.kwa hili sana nimeona tunaenda mahali si kila siku kujadili mafisadi mnaacha vitu vinavyowasaidia watu.maana hata hawa wenye nyumba wanatuonea sana na kutupa vitisho ukichelewa kulipa kodi bila utaratibu tunaomba tujue sheria zote ili tuepuke kunyanyaswa.

    ReplyDelete
  24. Kaka January, siasa ya ujamaa na kujitegemea ilikwisha pita miaka mingi sana, hata kabla Nyerere hajang`atuka. Hiyo mambo ya kusema mpangaji alipe kwa kila mwezi sio tanzania ya sasa. Mimi ni mmiliki wa nyumba Mbezi Beach, nimejenga nyumba ya thamani sana na imechukua miaka mingi kikamilisha , unakuja kukaa nyumbani kwangu bila deposit ya miezi6 au mwaka sahau! kama ni mwaka utalipia mwaka na ikifika miezi 3 kabla ya muda wako kwisha nitakupa notice kama utaendelea, na nitakuja kuchunguza nyumba kama ina uharibifu wowote nitakata kutoka kwenye deposit niliokuwekea.

    Mpangaji akikimbia, na nyumba tayari kisha iharibu ina maana mimi ndio nikaitengeneze kwa rent alionilipa ya mwezi mmoja ? Faida itakuwa ku renovate kila mwaka ?au akinambia hata pesa ya kulipia kodi mwezi huu ni muache yeye ni ndugu yangu? au alinisaidia kujenga hii nyumba? Acha mawazo ya TANU, hata CCM imebadilika sasa. TANZANIA NI KWA KWENDA MBELE!

    mdau mbezi beach
    dar

    ReplyDelete
  25. jamani watanzania acheni ushabiki wa kuongea tu kama hatuishi hapa bongo ni ofisi gani inatoa mshahara wa miezi sita au mwaka? kwa nini wenye nyumba nao wasipokee kodi ya mwezi.kama ndo umeanza kazi na unatafuta nyumba unaambiwa unatakiwa ulipe kodi ya mwaka hela hiyo inaipata wapi? na hapa bongo kuna watu wanaoitwa madalali hupati nyumba hadi upite kwao .Akikupeleka tu kuona nyumba iwe mbaya au nzurilazima umpe elfu tano hata kama hujaipenda sasa tz tunaenda wapi? mbona wenzetu wa kenya kodi wanalipa kila mwezi? ina maana nyumba za hapa bongo ni nzuri kuliko za nairobi? tuache ushabiki sheria ziwekwe za wenye nyumba na wapangaji mpangaji mwenye uwezo wa kulipa kwa mwaka alipe na wa mwezi mmoja naye alipe .

    ReplyDelete
  26. Ndio maana nimesema wabongo,wengi wetu tuna kiroho cha kwa nini!Nyie wadau mliosema kwa nini NHC wawauzie nyumba wapangaji wake wa muda mrefu,kwani wakiendelea kupanga wewe unafaida gani?au wakiuziwa utapata hasara gani,Hizo nyumba za huko Arusha ngarenaro huwezi kuzilinganisha na za Dar kama maeneo ya Upanga,kodi ni kubwa karibia sawa na wapangishaji binafsi,,na kila mara inapanda,,mimi si mkazi wa huko ila nilikuwa nasema tu kiutu,,mimi naona wabongo hatuna huruma wa kuhurumiana,,kila mtu anatetea nafsi yake,,sasa wewe mdau hapo juu uliyesema huwezi kusaidia watu wauziwe,,Je sasa hivi wakiambiwa watoke uingie wewe utakubali au utakataa?Ndo maana nasema wengi wetu ni Ya'arabi Nafsi!
    Anyway!!!Wote sisi WATZ ni kifo cha mfa maji,,,hata kama unajuwa huna uhusiano na NHC,huna faida wala hasara na hizo nyumba,utapigana mpaka wanao panga katika nyumba hizo wasiuziwe,kwa kuwa huishi humo
    Ahlam,,,UK

    ReplyDelete
  27. HUYO AHLAM ANALETA TU USHABIKI WA KIYANGA NA SIMBA. UNASEMA WATU WAPEWE NYUMBA KWA SABABU WAMEKAA MUDA MREFU? HIZO NI NYUMBA ZA NHC HATA KAMA HAZITUHUSU LAKINI NHC HAWAZIHATAJI? SI MALI YAO? KWA HIYO UNATAKA KUNIAMBIA UKIKAA KWENYE NYUMBA YANGU KWA MUDA MREFU UNA HAKIKA YA KUDAI KUUZIWA? HIVI NDUGU YANGU UPO DUNIA GANI? UNASEMA UPO UK? UK GANI HIYO? KUKAA MUDA MREFU KWENYE NYUMBA HAKUKUHALALISHI KUMILIKI! NYUMBA NI MALI YA NHC PERIOD.

    ReplyDelete
  28. Ahlam unasikitisha kwa kweli hebu jisikilize tena. we are living in a capitalist world. mwenye nyumba yake amejenga nyumba akiwa na business plan baada ya muda kadhaa anataka kuongeza investment ingine.

    Una jua kuna watu wengine mnaongea tuuu kwa sababu huko manchi za watu mnajizalisha ili mpewe nyumba za bure kutoka kwa state utakuwa na mawazo au ufunuo wa kuwaza saa ngapi maendeleo wakati kila saa wewe unajiweka kama charity case ulimwengu hauendi kihuruma huruma baby watu wanapambania maendeleo na kujikwamua kiuchumi kuwaza kiujima na ujamaa hautaweza hata kuwasaidia hao wanaoitaji msaada wako.

    ReplyDelete
  29. Yaani unaweka address ya kazini kwa hiyo ofisi ndio itakulipia kodi ukikataa kulipa au ukifanya uharibifu? people be realistic, kuweka address ya kazini haimaanishi muajiri amekubali kuwa guarantor wako wangapi wanafanya hii kitu na pindi mtu anapofia ndani ya nyumba, kakataa kulipa, au kafanya uharibifu bosi anaruka katukatu au unapewa jibu kwamba huyu mtu hayuko kazini siku nyingi unabaki kuhangaika mwenyewe. Na hasara juuuuu.

    Wengi mnaotetea hii mada si wamiliki wa majumba na hamna experience ya upangaji wala umiliki wa manyumba.

    This is a very delicate issue.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...