Kwanza kabisa tunachukua fursa hii kukupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya ambayo kwa kweli ni ukombozi tosha kwa jamii. Hii ni mara yetu ya kwanza kujitokeza katika blogu yako tukitoa malalamiko yetu, tunaamini kabisa hii ndiyo njia sahihi kwetu wanyonge kuweza kufikisha kilio chetu sehemu husika.

Ni matumaini yetu kuwa wewe ukiwa ni mdau muhimu sana katika suala zima la maendeleo nchini hapa, basi kwa hakika kilio hiki kitasikika na hivyo wanyonge tutakomboka. Tunakuomba sana mdau kero hii itoke hewani ili wote wanaojihusisha na vitendo vya dhulma, unyanyasaji na uchafu mwingine waweze kuona na kwa hakika iwe ni funzo kwao na kupelekea kukomesha mara moja vitendo vyote vilivyokinyume na maadili halisi ya Mtanzania.

Tumeamua kumuandikia barua ya wazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kahama kupitia blogu hii adhimu kabisa na inayotembelewa na wengi ili ajionee madudu yanayofanywa na watendaji waliochini yake hivyo kupelekea kuboronga kwa halmashauri yako na kuleta chuki dhidi ya uongozi wake kwasababu ya uzembe wa watu wasiopenda maendeleo.

Chondechonde mdau, tunakuomba uweke hewani ujumbe huu, tunaamini utawafikia walengwa na kuleta tija katika suala zima la maendeleo wilayani kwetu.

Kilio chetu sisi wanyonge tunakielekeza kwako Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kahama nacho ni juu ya huyu Mhandisi wa Halmashauri yetu ya Wilaya Kahama, Mhandisi Kalokola, kwakweli tumesikitishwa sana na vitendo ambavyo anatufanyia sisi wanyonge, na tutaendelea kusikitika mpaka hapo tutakapoona hatua stahiki zinachukuliwa dhidi yake.

Mhandisi Kalokola ameagiza kujengwa madaraja kuelekeza katika maeneo yetu na kuona hiyo haitoshi kaagiza kubomolewa kwa uzio (boma) ambalo limejengwa kwa lengo la kuzuia maji, hivyo baada ya boma hilo kubomolewa kumesababisha maji kuingia katika eneo hilo na kutusababishia hasara kubwa kwa kulowesha mali yote ambayo sisi tunahifadhi katika eneo hilo.

Wakati tupo hapo katika eneo la tukio tukijaribu kutafakari juu ya hasara tuliyoipata kwa kuloweshewa bidhaa zetu, Mhandisi Kalokola alifika eneo hilo na kutoa lugha ambayo kwa kweli ilituchafua sana na kutuchanganya zaidi. Kwa kifupi kauli ya Mhandisi imetuletea mfadhaiko mkubwa na ndiyo maana tumeona ni vyema tumshitaki kwako ili uweze kumchukulia hatua. Alisema tukizidi kumfuatilia kujua haki yetu atatufutia viwanja vyetu na alidiriki kusema kuwa hatuwezi kumfanya lolote.
Kwa kweli kauli hiyo imetusitua sana, sijui jeuri hiyo kaitowa wapi huyu Mhandisi.

Nakuomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kahama ujaribu kufuatilia nyendo za huyu Mhandisi wako na vitendo vya unyanyasaji anavyovifanya kwetu wanyonge na ikibidi umhamishe maana sisi wananchi tumechoshwa na vitendo vyake, kila kukicha watu wanamlalamikia yeye, kwakifupi Mhandisi Kalokola hatufai.

Wanakahama -Kwa pamoja tuijenge Wilaya yetu.

Wapendahaki/ Wanyonge
S.L.P
Kahama.
Mpendahaki66@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. 100% confidence levelFebruary 23, 2012

    Wanyonge wa Kahama,kwanza poleni kwa unyanyasaji unaofanywa na Mhandisi wenu kama ni kweli.
    Pili,kimsingi tatizo lenu ninadhani linahitaji ufumbuzi mapema na ndiyo uhalisia wa jambo lenyewe.Lakini nimeshindwa kuelewa kama hii taarifa ndiyo barua rasimi kwenda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama au la! kama ndiyo barua rasimi basi hamjafuata taratibu maalum za kudai haki yenu.
    Mlitakiwa kuwashirikisha viongozi wa serikali ya kijiji,kata na tarafa eneo lenu wanaounda kamati ya (Huduma za jamii ya Baraza la Halmashauri kwani kabla ya ujenzi huo,walishiriki kwa pamoja juu ya uboreshaji wa muundo mbinu huo) hili wamzuie Mhandisi kutekeleza azma hiyo ovu.Na kama viongozi hao wangeshindwa kutatua mgogoro huo,ndiyo mngepeleka malalamiko yenu moja kwa moja na kwa maandishi Ofsi ya Mkurugenzi.
    Hata hivyo hamjachelewa,fuatilieni utatuzi wa suala lenu kwa kuzingatia misingi ya taratibu,sheria na kanuni za serikali.

    ReplyDelete
  2. Mchomeni moto..mtu anawatishia maisha yenu na kuharibu mali zenu kisa ana kacheo fulani..mkienda polisi hawatawasaidia,wala fidia ya mali zenu hampati..huyo mkurugenzi nae walewale...dawa kumchoma moto,wakija polisi mnawaambie alikuwa mchawi...narudia tena mchomeni moto

    ReplyDelete
  3. Mtaendelea kusikitika...na kufadhaika...hadi mkurugenzi atakapochukua hatua.

    ReplyDelete
  4. Hakuna haya ya kufika kwa Magufuli, Patrick (TANROADS) anaweza kumkaanga huyu bwana fasta fasta atie adabu. Jamaa ni mchapakazi sana na hawezi kufurahia habari hii.

    ReplyDelete
  5. 100% confidence levelFebruary 24, 2012

    leo ankala umebana maoni yetu,haya bana ila kumbuka ankala mimi hii ndiyo ajira yangu kutoa maoni kwani bosi wangu anafanya tathimini ya jinsi ninavyoshiriki kwenye mitandao jamii.Haya bana sina mengi leo ankala au umebanwa na majukumu hapa Lond?

    ReplyDelete
  6. Wana Kahama poleni na masahibu yaliyowafika.

    Kwa Taarifa yenu Mtoto wa Mkulima Mhe. MIZENGO KAYANZA PETER PINDA leo hii yupo ziarani huko Mkoani kwenu Shinyanga hakikisheni mnatoa taarifa za huyu Jamaa!

    ReplyDelete
  7. Enyi Wapenda Haki Wana Kahama, ni kuwa 'Nyerere' yaani Mhe. Pinda yupo huko kwenu kwa ziara ya kikazi leo zifikisheni taarifa za huyu Mtumishi kwa Mkuu.

    ReplyDelete
  8. Mfikishieni taarifa hizi MHE. Mizengo PINDA yupo kwenu leo , mshuhudie Mhandisi akienda endesha Boda boda na kuuza Vocha!

    ReplyDelete
  9. Huyo Mhandisi wenu anatafuta kwenda kulima Kijijini kwao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...