Ras Makunja akiruka kama Jet Li mara baada ya kukerwa na mpiga Drum,Ugiriki.

Athesens,Ugiriki
Wandamanaji wenye hasira kali nchini Ugiriki,wameufanya mji wa Athesens kuwa uwanja wa mapambano,baada ya wananchi wa ugiriki kuingia mitaani kuandamana kupinga taratibu za mikopo kutoka nchi na mashirika fadhili yanayotaka kuikopesha fedha nchi hiyo na kuiokoa katika umasiki au ukata wa maisha unaoikumba nchi hiyo. 

juzi tu wandamanaji walivamia jengo la bunge la ugiriki ambapo wabunge walikua wakijadili hali ya umasikini na mashariti ya mkopo kutoka kwa wafadhili,askari wa kutuliza ghasia aka akina kina Ras Makunja,walikuwa na kazi ngumu ya kuwatawanya wandamanaji hao.

Hata hivyo hali ya kiuchumi katika baadhi ya nchi za ulaya inatisha na huenda baadhi ya nchi zikafilisika na ugumu wa maisha ukawa moto zaidi ya kiyama.

Ugiriki hakuna kulala.
akina Ras makunja na wandamanaji wakigombea lango la bunge.
kina ras makunja kazini ugiriki.
mmoja wa wandamanaji akiwarushia Kina Ras Makunja jiwe nchini ugiriki.
ugumu wa kazi ya kina Ras makunja.
wagiriki katika maandamano ya kulalamikia njaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Dai chako utake ubaya!,

    Mpiga Drums ametoa kali amaekuja na meza maalum kuwekea goma lake!

    ReplyDelete
  2. mi nimependa jinsi hao waandamanaji walivyojidhibiti kwa vifaa vya kuzuia gas, ushauri ni kwamba ikiwa nasi tunataka kuandamana basi polisi watugawie vifaa vya kuzuia gas za machozi na nguo maalumu za maji au kuwepo na maduka maalumu ya kuuza vifaa hivyo nchini na serekali iondoe ushuru ili vipatikane kwa bei rahisi. hapo ndipo nitakapojua kweli kuna demo krasia

    ReplyDelete
  3. Ankal yakianza Bongo utakuwa unatuwekea picha za disaini hii pia?

    ReplyDelete
  4. sasa huyo askari alipona na huo moto

    ReplyDelete
  5. Wabeba box mlioko huko bora mrudi nyumbani.

    ReplyDelete
  6. CUF na CHADEMA wakipigwa rungu kidogo wanakimbilia UN sasa Wagiriki wakimbilie wapi?

    ReplyDelete
  7. Wagiriki baada ya kumaliza pesa za Wabongo za Mkonge ambazo waliwatumikisha Babu zetu kwa kuwalipa Unga,Maharagwe na michuzi mbuzi tuu haya ndio matokeo yake.Ukipata pato lako kwa unya'gau,kuiba na kudhulumu matokeo yake ndio haya.Hawa majambazi wa Magharibi ndio yanayowapata sasa Wall steet occupiers nk.Huu ni mwanzo tuu yale yote wanayo waombea waafrica nawao yatawapata.

    ReplyDelete
  8. Hii ni style ya wanne stars walikosekana nyoka tu

    ReplyDelete
  9. Mdau wa 8 Anonyomus wa Wed Feb 15, 06:12:00 PM 2012

    NDUGU YANGU NAMIMI FIKRA ZANGU ZILIKUWA KAMA WEWE, NAKUUNGA MKONO 100% KWA 100% !!!

    ''UBAYA UKIFANYWA HUZAA UBAYA''

    MAJAMBAZI WA NCHI ZA MAGHARIBI WALITUFANYIA UBAYA SANA SISI WA AFRIKA NA SASA MUNGU ANATULIPIA KWA KUWAPA MATATIZO YA KIUCHUMI.

    UNAONA UBAYA WAO SASA?
    WANAZIDI KUTUOMBEA MABAYA NA KUTUTANGAZA VIBAYA KWAO, ZAIDI YA HAYO WANATUCHUKIA SANA NA KILA UCHAO WANAPANGA SERA ZA KUTUBANA SISI.

    LAKINI NI VILE HATUNA UBAYA NA YEYOTE MUNGU ATAENDELEA KUWA NA SISI!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...