salama mzee michuzi,

nataka nitoe mapendekezo yangu kuhusu uundwaji wa balaza la mawaziri litakalolenga katika kubana matumizi na kutoa tija kubwa kwa wananchi kama unajua kwamba zaidi ya nusu ya bajeti ya nchi inatoka nje kama misaada na kutokana na kuyumba kwa uchumi dunia serikali ya Tanzania inatakiwa kuchukua hatua muhimu katika kubana matumizi ya serikali na kufanya hivyo kutaondoa hata matatizo kama ya migomo ya madaktari kutotokea tena.

Baraza langu la mawaziri litakuwa dogo sana na lenye uwezo wa kuwafikia wananchi Baraza limegawanyika katika serikali kuu na serikali za mikoa

SERIKALI KUU NI

kutakuwa na waziri mkuu
makamu waziri mkuu
waziri wa fedha na uchumi
waziri wa mambo ya nje
waziri wa mambo ya ndani
waziri wa ulinzi

SERIKALI ZA MIKOA

kutakuwa na ofisa wa mikoa
ofisa wa Elimu wa mkoa
ofisa wa Afya wa mkoa
ofisa wa maji na kilimo na mifugo wa mkoa
ofisa wa watoto na wanawake wa mkoa
ofisa wa usafirishaji na miundombinu wa mikoa
ofisa wa mazingira na utalii na maliasili wa mkoa
ofisa wa michezo kazi na vijana wa mkoa
mwanasheria wa mkoana mambo ya katiba
ofisa wa biashara wa mkoa

hawa maofisa wa mikoa watapa mishahara ya kawaida na watakuwa wanareport kwa mkuu wa mkoa na mkuu wa mkoa atakuwa anakuja bungeni kujibu maswali ya wabunge kwani sijapata kujuwa kazi ya wakuu wa mikoa Tanzania hapo tutakuwa tunaweza kubana matumizi makubwa ya serikali na wananchi watakuwa wanaweza kwenda kuwaona maofisa wa mikoa rahisi kuliko mawaziri ambao wengi wanaishi upanga na mikocheni na wananchi wengi wenye mataizo wapo mikoani na vijijini.

naomba ushauri kutoka kwa wanalibeneke wengine kama wanamawazo tofauti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Hii hierarchical architure yako inahitaji wasomi kuwa kwenye different ranks ili kutekeleza agenda. Remember TZ government is run by politicians and not professionals. In ur system u nid more dr, lawyers, accountants, engineers, scientists and you need what we call distributed systems of leadership. currently, TZ system does not require you to be such profesional to lead hence works. anyway I like ur idea.
    ras.

    ReplyDelete
  2. Utabadirisha baraza la mawaziri mara kadhaa, lakini shwala la msingi siyo kubadilisha balaza au maofisa wakazi wa mkoa au wilaya, bali ni mishara, walipe watu mishahara mikubwa halafu uone kama hawatajituma au watagoma.

    ReplyDelete
  3. Mawazo mazuri. Tanzania inaukubwa karibu sawa na state ya Texas lakini kuna mawaziri kibao. zanzibar kuna idadi ya watu milioni moja, lakini kuna wizara karibu 15. Siyo vizuri kulinganisha Marekani na Tanzania, lakini wenzetu wana idadi ya watu karibu milioni 350. Kuna wizara 15 tu. Kuna waziri mmoja tu wa usafirishaji ambaye pamoja na mambo mengine wizara yake inahakikisha ndege 15,000 angani kwa dakika moja hazigongani.Sijui Dr. Kikwete angekuwa rais wa Marekani, wizara ya usaafirishaji igekuwa na mawaziri 100? Nafikiri hata University of Maryland ingekuwa na waziri wake wa uchukuzi maana inamiliki zaidi ya ndege 50. nafikiri angekuwa na mawaziri 500 wa ulinzi, kila aircraft carier yenye ndege za kivita na helcopters 100 ingekuwa na waziri wake. Ukienda kwenye elimu unakuta vyuo karibu 10,000. Kila vyuo 50 vingepata waziri wake wa elimu. Tukumbuke kuwa white house na baraza la mawaziri hakuna mtu ambaye jina lake linaanzia na titles kama "Dokta", injinia, muheshimiwa, mkuu, mtukufu, mstahiki, Daktari BINGWA nk. wanatumia majina ya kawaida tu lakini mwendo mdundo. Angekuwa mtazania pale white angejiita Quadruple Bingwa Dr. Rugashemererwa/PhD@ Havard-Esq.Kumuona inabidi kuweka appointment ya miaka miwili.

    ReplyDelete
  4. Hakuna Afisa Utamaduni(Dharau??????). Utamaduni ndio kila kitu, utamaduni huleta uzalendo, hujenge tabia ya uaminifu, utunzaji wa mali, utamaduni wa ulipaji kodi etc etc

    ReplyDelete
  5. Kwa mapendekezo yako haya unataka Mh. Magufuli ashike wadhifa upi?? Kama hujapata pa kumuweka basi fikiria tena au mwambie Mtoto Wa Mkulima ampishe.

    Abiola Jr.
    Mafia kiduka cha Juice

    ReplyDelete
  6. Good idea but goes back what Nyerere introduced "Madaraka Mikoani" nobody understood him. There are should be no Regional commissioners. Merge regions into provinces to make it at least 10. These provinces should control their own resoucres and administration as outlined by the new constitution. Heads of these provinces must be elected by wananchi the same way the president is elected to make them accountable. Zanzibar must be one of the region or get it separate from the mainland.

    ReplyDelete
  7. MzeeKifimboChezaFebruary 15, 2012

    Michuzi,

    Hebu sahihisha kichwa cha habari hapo juu jamani.

    Ni baRAza jamani sio baLAza.
    Mbona siku hizi hawa madogo wa dot.com wanatuchafulia sana lugha jamani?

    ReplyDelete
  8. Ustawi wa jamii ipo wapi?

    ReplyDelete
  9. Hapa kwa TZ haiwezekani kamwe maana utasikia sijui wazee wa CCM wanalalamikia haya mabadiliko kwa kuwa yamekuja too fast na wao hawajazoea kwa hiyo tuwasikilize wazee wetu tusije potoka. Hii nchi laana tupu tu na ndiyo maana sasa manabii feki wamejazana kuuza unga na kuibia watu huku serikali inawachekelea tu.

    ReplyDelete
  10. Sina utaalamu sana na Muundo wa Utawala na uakisi wake katika matumizi ya Serikali.

    Isipokuwa naona ili kukabiliana na wimbi la kuanguka kiuchumi na kuepeuka Utegemezi wa Misaada kwa vile hao Mabosi wetu nje wamefilisika na ndio kama tuna vyoona Ugiriki migomo kila uchao.

    Nadhani zaidi ya kuchukua tahadhari yenye kulenga kubana Matumizi ya Umma na Bajeti, Serikali Kuu iangalie zaidi ''Muundo wetu wa Kiuchumi wa Ujumla na zaidi Vianzo vya Mapato na Mihimili ya Uchumi:

    Ni dhahiri kuwa MAKUSANYO YA MAPATO, NDIO YANAYOTOA UWEZO WA KUELEKEZA MATUMIZI YETU:::WAKATI MAKUSANYO YANATOKANA NA VIANZO VYA UCHUMI:::NA HIVYO VIWILI NDIO VINAJENGA UWEZO WA KUJIMUDU NA BAJETI KUTIMIA.

    HIVYO BASI NI VEMA TUBADILISHE MFUMO WA UPATAJI WA MAPATO YA NCHI UNAOJENGA UCHUMI:

    -TUJARIBU KUPUNGUZA UTEGEMEZI WA SEKTA YA KILIMO KAMA NJIA YA PATO LA TAIFA LICHA YA KUWA NDIO KINAAJIRI ASILIMIA KUBWA YA WATANZANIA, KWA VILE KILIMO KINAATHIRIWA ZAIDI NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA DUNIANI NA TABIA NCHI.

    -TUANGALIE ZAIDI SEKTA ZA MADINI NA UZALISHAJI WA PILI (PROCESSING INDUSTRIES),kwa mazao ya kilimo,madini,wanyama na rasilimali zingine KUWA NJIA YA MAPATO.

    -TUANGALIE PIA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII KUWA NJIA YA MAPATO.,,,Wanyama Pori, Misitu,Mazao ya Bahari, Mazingira,Kuimarisha Mbuga za anyama na Uwekezaji wa Mahoteli na Vivutio vya Utalii N.K.

    -TUANGALIE ZAIDI HUDUMA ZA KIBIASHARA, NA MATANGAZO SAMBAMBA NA MICHEZO KAMA NJIA YA KUKUZA UCHUMI NA AJIRA BADALA YA MICHEZO KAMA BURUDANI LICHA YA KUFANYA KIWANGO CHA CHINI KIMAFANIKIO.

    -TUANGALIE ZAIDI MAONYESHO YA BIDHAA ZETU (PROCESSED GOODS) NJE NA KUZIWEKA KATIKA VIWANGOKUKIDHI USHINDANI NDANI NA NJE,ILI KUONGEZA PATO LA TAIFA

    PANA UWEZEKANO NJIA HII IKAMIMARISHA ZAIDI UCHUMI WETU KWA KUONDOA ''INFLATION'' (UKATA WA KIFEDHA) KWA THAMANI YA FEDHA KUTOYUMBA IKAZAA MATATIZO YA KIFEDHA NA KIUCHUMI YANAYOTOKANA NA DENI LA SERIKALI LINALOKUA KWA KUKOPA KWA RIBA KUBWA (TREASURY BILLS) KWA VILE ''INFLATION INATIBIWA KWA KUONGEZA KIWANGO CHA RIBA ''INTEREST INAYOKUZA MADENI''.

    HIVYO KWA NJIA HII HATA LIKIUNDWA BARAZA LA MAWAZIRI LENYE WIZARA 100 KTK SERIKALI YENYE UCHUMI IMARA UTAMUDU KULIENDESHA.

    ReplyDelete
  11. Jamaa amekuja na mchanganuo mzuri ila sasa tatizo ni kwamba mfumo wetu wa siasa haulengi kumsaidia mtanzania wa kawaida bali kutengeneza nafasi kwa vigogo wa serikali na familia zao. imagine sasa tuna waziri wa mambo ya ndani, wakuu wa mikoa na makaimu wao. makatibu tawala wa mikoa na makaimu wao bado hujafika wilayani.... yaani ni kichefuchefu ukiuliza kazi zao nini hazieleweki ni kama magogo yanayokula tu. Mi naunga mkono mapendekezo ya huyo bwana. nadiriki kusema kuwa ni creative. Inawezekana tu kwa kuondoa utawala dahalimu waccm unaoungwa mkono hata na ankal michuzi, najua na yeye yupo kimaslahi japo ukweli anaufahamu na watanzania tumeufahamu.

    ReplyDelete
  12. Jamaa amekuja na mchanganuo mzuri ila sasa tatizo ni kwamba mfumo wetu wa siasa haulengi kumsaidia mtanzania wa kawaida bali kutengeneza nafasi kwa vigogo wa serikali na familia zao. imagine sasa tuna waziri wa mambo ya ndani, wakuu wa mikoa na makaimu wao. makatibu tawala wa mikoa na makaimu wao bado hujafika wilayani.... yaani ni kichefuchefu ukiuliza kazi zao nini hazieleweki ni kama magogo yanayokula tu. Mi naunga mkono mapendekezo ya huyo bwana. nadiriki kusema kuwa ni creative. Inawezekana tu kwa kuondoa utawala dahalimu waccm unaoungwa mkono hata na ankal michuzi, najua na yeye yupo kimaslahi japo ukweli anaufahamu na watanzania tumeufahamu.

    ReplyDelete
  13. Mada nzuri kweli,sisi wengine ambao hatuna elimu ya haya masuala ya uongozi/uchumi tumeweza kuelimika na hasa kupitia maoni ya mazuri ya wadau hapo juu na mtoa mada mwenyewe.Nawashukuru.Hii ni moja ya kazi za Blog-Kuelimisha.

    David V

    ReplyDelete
  14. Good! imetulia ila it needs some minor ammandement...Wizara kama ya Miundombinu na Mawasiliano ni bora iwepo kwenye central government, pia wizara ya elimu is also better to be in central government...vinginenyo imekaa vizuri

    ReplyDelete
  15. Wed Feb 15, 08:28:00AM 2012

    -UPATAJI MAPATO YA NCHI UNAOJENGA UCHUMI:

    -UTEGEMEZI WA KUPATA FEDHA KWA KUTEGEMEA KODI YA VITU KAMA MAFUTA NA KUPANDISHA GHARAMA ZA NISHATI KAMA UMEME, HUZIDISHA ''INFLATION'' YAANI UKATA AU MFUKUKO WA BEI, HIVYO BASI KADRI UTEGEMEZI HUU UNAVYOPUNGUZWA NDIO NAFUU NA KUIMARIKA KIUCHUMI KUNAVYOKUJA.

    ReplyDelete
  16. Hi,

    i am agreed with you. Changes does not come from anywhere. We Tanzanians we have to put our thoughts and conversations into action, educate the next person to you, relative or family in the village. Let us mobilize the youth and and let our voice heard. If we are not carefully the next generation will suffer extremely.
    1.The country should 50% of all income from the mines
    2.Everything should be done in Tanzania, forbid exporting of raw mines(employment opportunity and circulation of money)
    3.Tax heaven, if you cahnged the name of business after five years, you still pay the capital gain.
    IF YOU CANT PACK YOUR SHIT AND GO.
    MADINI NA ARDHI HAVIOZI

    ReplyDelete
  17. jamaa hapan kaongea lamaana kwani hata mimi sijui kazi ya mkuu wa mkoa

    ReplyDelete
  18. Inapendeza. Ongeza wizara moja e.g. wizara ya serikali za mikoa, ambayo itakuwa juu ya serikali za mikoa. wizarani humo kuwe na wakurugenzi wa hizo sekta e.g mkurugenzi wa afya, etc ambao watawakilisha mitazamo ya sekta hizo kitaifa badala ya maofisa wa mikoa kuwakilisha bungeni

    au
    hawa wakurgenzi wawe chini ya naibu waziri mkuu.

    ReplyDelete
  19. Mawazo yako ndugu yangu yapendwa na wengi nami nikiwemo.Yaonekana ndoto lakini yawezekana kabisa.Mimi si mtaalamu wa miundo lakini nashawishika kuwa wataalamu wapo na waweza kuifanyia kazi.Na si lazima watoke nje ya nchi.

    Kusema ukweli baraza la mawaziri ni kubwa mno,makatibu wakuu ni wengi mno,wabunge nao ni wengi mno.

    Kama ulivyopendekeza hayo yote yaweza kufanywa na wakuu wa mikoa na wasaidizi wao,na migawo ya matumizi ikafanywa na hazina chini ya waziri mkuu na kamati yake.

    Hapa tujadili hoja ya msingi iliyotolewa na mdau,sasa wengine tayari wameanza kuingiza jazba yao na maneno yanayokwenda nje ya hoja.

    Kusema kumuona Dr.Bingwa lazima appointment!wapi hakuna hii.Sisi tuko ulaya ndo kumezidi,huku hata mtu mngonjwa appointment ndefu.Huku usipokuwa mwangalifu waweza kufa.Ndo maana wengine akitaka aonwe haraka anajiangusha barabarani ili ambulance imchukue ili aonwe haraka na waganga vinginevyo atakufa akisubiri appointment ndefu.Uongooo!Unayekataa unaishi wapi wewe.

    Tuendelee na hoja ya msingi kama alivyoilete mdau.








    Kila kitu unajua watanzania bwana,kila kitu unatujua watanzania bwana,nyie watu mumefanya au mumejaribu kulaumu tu huku mkikaa hukuhuku.Nendeni katoeni uzoefu wenu sasa.

    Tuendeleze hoja ya msingi ya mdau.

    ReplyDelete
  20. Mjadala mzuri wanapongeza Wadau na 3&5 ni kweli tunahitaji small govt kutokana na nchi yenyewe ilivyo kwani baraza la mawaziri,manaibu,makatibu wakuu ni kubwa takriban 100.Nimzigo mkubwa kwa watanzania walipa kodi pesa zote zinaishia kwenye mishahara na marupurupu yao.Pia mfumo wa viongozi wa mikoa na wilaya kuteuliwa na Rais umepitwa na wakati,viongozi wengi wa mikoa na wilaya ni wale waliostaafu jeshi,walioangushwa ubunge ambao wanaelewana na Rais ndio wanapeaw nafasi hizo.Ukweli wengi wao hawana uwezo kushika nafasi hizo kutokana na elimu zao.

    ReplyDelete
  21. hamna lolote wamekalia kubebana tuuu, miwizara kibao miundo mbinu bure kabisa , kwanza haya mawizara ndo yanaongoza kwa rushwa yanafilisi nchi tuu yangepunguzwa sana, kwa kazi zipi hasa zaidi ya ufisadi?

    ReplyDelete
  22. Katiba mpya iyende na wakati mambo ya kupeana vyeo kwa kujuana yaishe pili upuuzi unaoendelea sasa wa titles[Dr,waheshimiwa,Eng,CPA,MBA nk] unatapisha kwani viongozi hawa wamelewa hizo titles na kuharibu mambo.Mfano wizara ya afya Madoctor watatu Dr Mponda,Dr Nkya na Dr Mtasiwa wamesababisha Maafa ya watanzania Masikini.Kumbuka PHD,DR,ENG,CPA nk itakuwa na manufaa kwa taifa kama Utu na Uzalendo utawekwa mbele,wengi wao wamesoma wameondoa Ujinga na kubaki na Upumbavu.[Educated Fools.]

    ReplyDelete
  23. Mkuu wa mkoa tunavyoabiwa anamuwakilisha Rais,ukweli Mikoa inahitaji Viongozi wa kuchaguliwa waliosomea uongozi ili kuinua maisha ya wananchi,kwa kubuni miradi ambayo itutoa ajira nakama hakufanya kazi yake vizuri hatachagulwa tena hii ndio Demokrasia ya kweli.

    ReplyDelete
  24. Wakenya wameunda katiba mpya hasa kutokana na yaliyowapata mwaka 2007/2008 Mwenyezi Mungu atuepushe na hayo ambayo imepunguza kiasi kikukwa viongovi wakuteuliwa. .Ilatusipokuwa wangalifu amani tunayojivunia itaondoka.Viogozi tatueni kero za wananchi husuan haki zao mishahara nk.Katiba mpya iwape wananchi madaraka zaidi kuliko ilivyo sasa viongozi wa wilaya na mikoa wawe wakuchagulwa tuu,na wabunge wakuchaguliwa na sio wakuteuliwa na Rais kama ilivyo sasa nasiwepo wa viti maalum ili kubana matumizi.

    ReplyDelete
  25. Wadau madini yetu yanamalizwa na hayanufaishi wananchi kutokana na Ulafi wa Viongozi wasio waaminifu ambao wanashirikina wachimbaji hao.Kuna viongozi wasataafu ambao sasa wanakubali makosa yao katika kupitisha muswada wa sheria za madini walipokuwa bungeni.Swali jee waliopo watarekebisha sheria hizo ili wananchi wanufaike?Viongozi kumbukeni dhamana mliopewa ni kubwa na Mweyezi Mungu na kesho Akhera mtajibu nini?

    ReplyDelete
  26. WINGI WA WACHEZAJI KATIKA TIMU SIO KIGEZO CHA USHINDI WA MECHI, INAWEZEKANA MKAWA WENGI KTK TIMU LAKINI MKAFUNGWA NA WACHACHE!

    IDADI KUBWA YA WIZARA NA MAMLAKA YA MADARAKA SIO KIGEZO CHA UFANISI WA SERIKALI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...