Kamanda Misime wa kanda ya kipolisi Wilaya ya Temeke akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kusimamia zoezi la kuzima moto katika kiwanda cha magodolo cha Pan African kilichopo Chang'ombe jijini Dar es salaam, kiwanda hicho kimeteketea kabisa kwa moto  kutokana na mlipuko uliotokea kwenye mashine za kunolea visu vya kukata magodolo kiwandani hapo, Kamanda Misime amesema hakuna taarifa ya mtu yeyote kupoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo la moto
Askari wa vikosi vya kuzima moto wakiwa kazini wakati walipokuwa wakizima moto kiwandani hapo
Magari ya vikosi vya kuzima moto yakiwa yamejipanga katika kiwanda hicho yakiendelea na kazi ya kuzima moto.
Hiki ndiyo kiwanda chenyewe kama kinavyoonekana kikiwa kimeteketea kabisa.
Askari wa kikosi cha kuzima moto wakizima moto huo.
Hawani baadhi raia wa kigeni ambao ni wafanyakzi wa viwanda vya jirani na kiwanda hicho.
Watu mbalimbali wakiangalia tukio hilo. Picha na John Bukuku wa FULLSHANGWE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. hivi hawa wachina wanafanya nini bongo?????

    ReplyDelete
  2. raia wa kigeni wamechoka namna hiyo hiyo hela ya kulipia kibali wanaipata wapi - hao ni lazima wanaishi kinyemela huko kwenye magodown na laiti wangalimuona mpiga picture wangezaa naye , huo ni mtaji wa uhamiaji kila mwezi wanaenda kuchota fungu hapo - jamani !

    ReplyDelete
  3. Insurance scam hiyo!

    ReplyDelete
  4. Lakini kutokana na inflation lazima viwanda vingi viungue kwani wanaogopa hasara na wanavichoma moto wenyewe ili walipwe na Insurance bila kujua wanaongeza tatizo la inflation. Tatizo makachero wa bima wakienda nao wana fungu lao ili watengeneze ripoti nzuri ya kumfever mwenye godown/kiwanda kushawishi alipwe. Hii "nji" bwana! sijui tutaponea wapi manake madhara ya inflation yanaangamiza watu wa tabaka la kati na chini tu huku wasababishaji wakubwa wakiendelea kupeta!

    ReplyDelete
  5. Dah! Kweli hawa Wachina wamechoka. Sitashangaa nikiambiwa kwao walikuwa ombaomba, lakini Bongo wanaitwa wawekezaji.

    ReplyDelete
  6. WA-TANZANIA SIE WATU WA AJABU MSHAANZA RAIA GANI WAMECHOKA SABABU WACHINA HAO WANAPIGA KAZI HIYO, NYIE ENDELEENI KUZARAU NA KUCHAGUA KAZI KWA KUZARAU NDIO NYIE MNAONA WAZUNGU WAKIENDA MAMA NTILIE NI KITU CHA AJABU NA USHAMBA WENU, UKIJA KAMA MTALII NCHINI VIZURI WAKALA MITAANI KULIKO NYOTA TANO HOTELINI,WENZETU WANAHANGAIKA NA BOX SIO KUKAA KWENYE MAGOGO VIVU AU KIJIWE NAKUKOROMA MCHANA MTAANI JITU ZIMA NA WA KWANZA MTU KULALAMIKIA SERIKALI. Kitwana

    ReplyDelete
  7. Kaka Michuzi habari zilizo nifikia sasa hivi ni kwamba huo moto umemua msichana anaitwa Mariam.Alikuwa kibarua kwenye hicho kiwanda. Kaka mtu kaja kumulizia leo asubuhi baada ya kutorudi nyumbani jana basi kutoa tarifa ndo wakatafuta kumbe kafia kule juu kaungua uso wote. Nadhani moshi ulimzinda akashindwa kushuka kwa haraka. Leo asubuhi police wa changombe wameitwa kuchukua maiti yake. So sad!

    ReplyDelete
  8. Wachina wanapiga kazi tu, wanalala godown na kuamkia kazini. Baada ya mwaka mmoja wanafungua ofisi na kuendelea kupiga kazi! Wabongo starehe, pombe, chuki, wikvu na maneno meeengi, utafikiri wapenzi wa Simba!

    ReplyDelete
  9. wabongo bwana kazi kusema wenzao eti wahamiaji sijui wachina wamechoka

    hivi sisi tuliokuwa tumejaa huku ughaibuni mbona hatusemwi au raha kujaa kwa wenzenu na wenzenu kuja kwenu ni dhambi?

    bongo tunaongoza kwa ubaguzi mtake msitake hata huko china wabongo wamejaa.

    ReplyDelete
  10. MWENYEZI AMLAZE. MAHALI PEMA PEPONI! HAPO ICHUNGUZWE KAMA MDAU JUU KASEMA HIZI SCAM ZINAUMIZA WASIO HUSIKA MARA NGAPI NCHINI HAPA INATOKEA ALAFU TUNAONA WANAFUNGUA BADAE KIWANDA KIKUBWA ZAIDI MFANO KLABU MAWINGU. KITWANA

    ReplyDelete
  11. kumbe magari yenyewe ya zima moto bado ni yale ya enzi za mkoloni yaani hata lift tu hayana. mbaya zaidi yanatumia maji badala chemical, kaazi kweli kweli. lazima kila kila kitu kiteketee kwa mtindo huu...

    ReplyDelete
  12. huyo wamemtoa kafara

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...