Gadi Stephano Nkalang’ango
(11 July 1941-10 February 1980)



Miaka 33 imepita tangu alipotutoka baba Yetu mpendwa Gadi. Alipata ajali akiwa njiani kutoka Morogoro kwenda Dar-es-salaam. Alikuwa amemaliza kazi zake za ukaguzi wa mahesabu katika Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu ( Zilizopo Morogoro). Ndipo alipopata ajali sehemu ya mlandizi tarehe 08 Februari na kufariki siku mbili baadaye. Kwa kweli pengo lake halilizibiki.  Lakini Mungu ni Mwema ambaye amekuwa akitufariji na kututia nguvu siku hadi siku na sasa tu watu wazima.

Anakumbukwa na Mke wake mpenzi Hellena, Dada yake Magdalena (Mwalimu Kitururu) na wadogo zake Abasi, Naisai, Nambuyu, Nambua, Mwanahawa, Suni, Keto Bakari, Nkalang’ango, Sembua, Kosoni na Mtango.

Pia anakumbukwa sana na Wanawe Wapendwa sana Mramba (Baba Wawili), Neema (Mama Nyamaka), Ididi, Kighenda, Mshighwa (Emmanuel/Baba Alice), Nshighia (Tula/Mama Frida), Martha na Gadi Junior (Samweli) ambaye alizaliwa siku 9 baadaye baada ya baba Kufariki.  Na pia wakwe zake Wapendwa pia wanamkumbuka; Wanoga (Mama Wawili), Kosmas (Baba Nyamaka), Ansila (Mama Gadi) na Abraham (Baba Frida) na Alvin.

Wajukuu wamekuwa wakimtazama tu kwenye picha na kuangalia kaburi la Babu yao mpendwa. Wangependa leo hii wanataniana naye, wanacheza naye na kupewa hadithi za zamani lakini haikuwa mapenzi ya Mungu. Wajukuu hawa wataendelea kumi-miss kampani yake, Praise-God (PG), Praise-Jesus (PJ), Nyamaka, Gisela, Alice, Moses, Gadi, Msogoleka, Frida na Richard (Gadi).

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe [Ayub. 1:21]

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. RIP Baba, nipo pamoja nanyi ktk maombi wakati wa kumbukumbu hii@Kighenda , Mama Nyamaka, Emmanuel and my friend Samueli.
    Your Friend Tg .

    ReplyDelete
  2. Yeah ni mda mrefu RIP Mzee Nkalangango, by then tulikuwa watoto sana sana hata sikumbuki hali ilikuwaje, lakini tumekua kampanya na kina Mshigwa, Alice, Ney etc. Mungu amewakuza japo pengo la mzee kuzibika kamwe haiwezekani. Amina

    ReplyDelete
  3. RIP mzee Nkalangango..,
    Tafadhari naomba bwana Samweli anitafute kwa bwmp2005@yahoo.com nimepoteana naye siku nyingi sana.

    ReplyDelete
  4. RIP Mzee Nkalang'ango. Jamani Mramba and the team mdumishe upendo aliowaachia Mzee ili tuzidi kumuenzi

    ReplyDelete
  5. We Loved You but God Loved you more. Jina la Bwana libarikiwe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...