Bwana Mkubwa Michuzi, nakusabahi.
Ninaomba unirushie hewani mpasho huu kwa mitandao ya simu za mikononi hapa Bongo.
Hawa jamaa wengi wamekuwa wakijitangaza kwamba wao wana gharama nafuu kuliko mitandao mingine yote hapa Tanzania, 'basi kubwa' anasema hayo hayo, 'thumuni au Volks Wagen 'Kobe' nae anasema hivyo na bila kumsahau yule mwenye bajaji ndefu au mdhamini wa ligi kuu. Kuna wakati 'basi kubwa' kweli alikuwa cheap sana, alitangaza kwamba ana-charge shilingi 1 kwa sekunde kwa kupiga mtandao ule ule.
Sasa cha ajabu sasa hivi nimeongea na mtu wa mtandao huu huu hapa hapa Dar nimetumia shilingi 175 kwa dakika 1, ina maana ni karibu shilingi 3 kwa sekunde. Swali langu ni kwamba lini ametutangazia kwamba gharama zimepanda? Mbona wakishusha wanapiga promo sana, why not wakipandisha? Kwanini wanakuwa na 'hidden charges'!?
Wakati ule kwa sisi watumiaji wa hali ya bajeti kali, tulikuwa tukiweka alfu 5 tunasogea sogea sana hata wiki inakwisha, na tulilazimika kununua line za mitandao yote ili upate advantage ya gharama nafuu za simu za mtandao mmoja, sasa mbona hali imebadilika kimya kimya? Je, huu ni si kama uhuni na unyonyaji, kupandisha gharama kimya kimya huduma zikiwa zile zile? Na wale waliokuwa wanasema thumni, inaendelea hiyo kweli!?
Kero nyingine ambayo napenda waijue ni upatikanaji wa vocha. Hii ni kwa mitandao yote. Hawa jamaa wameongeza sana 'profit margin' katika bei wanayowauzia wafanyabiashara ya jumla kiasi kwamba kwa wale wa reja reja faida imekuwa ndogo sana. Matokeo yake sasa hivi maduka mengi sana hayauzi vocha. Mangi mtaani kwangu anasema hailipi kabisa.
Anasema katika mauzo ya vocha za laki 1, anapata faida shs 3,000. Wanatumia gharama kubwa sana kwenye matangazo na promosheni na gharama hizi zinasababisha wawabane sana wasambazaji wao, wapandishe bei kwa siri kama nilivyotangulia kusema hapo juu, matokeo inakuwa kero na dhuluma kwa wateja.
Na la tatu ni kero ya meseji za promosheni. Thumuni ndo wamezidi sana. Niliwahi kuona kero hii imerushwa hapa mtandaoni lakini jamaa wana kiburi cha pesa, sijui jeuri hii wameipata wapi! Hivi TCRA hawana mabavu ya kutusaidia wateja, mara leo weka muziki, mara bahati nasibu, mata tuma pesa kutumia.....pesa upate hiki na hiki, mara sijui ofa gani, nani anahitaji yote hayo kwenye simu yake!?
Mdau.
Kweli mdau! Hawa jamaa wanatuua kwa dizaini ya kansa! Nilishawahi kusikia eti Tz ni moja wapo ya manguli ktk kutoza garama za juu ktk mitandao ya simu!
ReplyDeleteNi kweli kabisa jamani. TCRA walilazimisha na kukomalia kuwa watu wasajili simu zao na kuweka deadlines kibao, kumbe matumizi yake ndiyo tunayaona sasa....... Mtu unatumiwa meseji za promotion kibao bila kupenda. Naamini kwa nchi wenzetu huwezi thubutu kumtumia mtu meseji za Biashara bila kujua Kama yuko interested au vipi. Nimepata fununu kuwa iko agency inayohusika na mambo ya vipimo wanajipanga kupima hizo sekunde na dakika kama huwa zinatimia. Lakini kero nyingine ni ile ambapo, simu yako inakuwa imebakia muda kidogo wa hewani halafu ukitaka kupiga simu unaambiwa salio lako halitoshi kupiga! Hizo chenji wanapeleka wapi? Jamani, hivi hiyo siyo "day light robbery"? Mama Ibra, wa Tabata
ReplyDeleteyaaani mdau hapo utakuwa umegusa ukweli tupu. hawa jamaa sijui wana mpango gani na wateja wao. kila wanalosema kuhusu kupunguza gharama za simu baada ya muda mfupi inakuwa ni kinyume chake, wanaanza kuwaibia watu. gharama zinapanda mara dufu. inafika kipindi baadhi ya mitandao hata kama hujapiga simu wanakata pesa. hakika wanatukomoa sana. faida wanayoipata ni kubwa sana. pia hayo ma message ya promotion zao yanaboa sana, mara muziki, mara mapenzi. tumechoka sasa!
ReplyDeleteTurudi TTCL tu, PERIOD!
ReplyDeleteMdau OGOPA TUKIO HILI:
ReplyDelete''BEPARI ANAPOKUWA ANATAFUTA FAIDA'' ASALALEEE MKATAFUTE PA KUKAA!
Ukiona Kampuni za Mitandao zinatoa Promo ni ktk kutapata tapa kupigania Ushindani wa Kibiashara tu,,,zinakuwa ni promo za Kimtindo za kufikia Malengo,,,Maafisa wa Masoko viti vyao vya moto Maofisini mwao,,,wao sio Father Christmass kwa kugawa Sadaka wanataka FAIDA!
PIA PANA MTAALAMU MCHAMBUZI ALITOA MAONI YA ULINGANISHI KUWA KTK SEKTA 5 ZA BIASHARA HIZO HAPO CHINI ATAKAYEFANYA NA KUSHINDWA AU KUFILISIKA, HAKUNA NCHI INGINE DUNIANI ATAWEZA FANIKIWA ZAIDI YA TANZANIA!
Tanzania ni nchi yenye tariff kali ktk huduma hizi:
1-Benki
2-Mitandao ya simu
3-Storage charges/ Ghala za bidhaa
4-Nishati /Mafuta,Umeme na Maji
5-Business District Rental Premisses, Mfano Tanzania US$ 40 per Sq foot, wakati Nchi zingine ktk East Africa Kenya,Rwanda na Uganda wastani ni US$ 18 per Sq foot.(Rent ya biashara ni karibu mara 3 kulinganisha na Jirani zetu)!
TCRA mpo? au huwa hamsomi kwenye libeneke nini?
ReplyDelete