Habari ya Kazi Brother Issa Michuzi,

Naitwa Emmanuel Nyagawa kwa sasa nipo nchini Denmark lakini ni mtanzania, kuna jambo limekuwa linanitatiza sana kuhusu wahamiaji haramu ambao wanaingia nchini kwetu kwa njia mbali mbali, hususani tukio la hivi karibuni ambalo uliripoti katika blog ambayo mimi ni msomaji wake la wale waethiopia 98 waliokamatwa katika pori mojawapo huko Morogoro. 

Tatizo langu ni namna ambavyo sheria zetu zina udhaifu katika kushughulikia mambo hasa haya ya wahamiaji haramu, huku ulaya mtu akikamatwa amezamia na hana legal documents za kuonyesha kwamba anaishi kihalali, hukamatwa on the spot anapelekwa uwanja wa ndege anarudishwa nchini kwake mara moja, sasa niliona siku moja umepost jamaa wapo wanapewa chai wakati wakisubiri kuingia mahakamani.  

Sasa serikali inaingia gharama ya kuwalea watu ambao hawana tija kwa taifa manake hao huwezi wapeleka shamba wakalima huwezi kuwapa kazi yoyote wakafanya. Wanapokuwa mahakamani wanahitaji mkalimani ili waweze kueleweka, wanahitaji mahali pa kulala, wanahitaji chakula kila siku, hivyo vyote vinalitia taifa hasara na kodi zetu watanzania zinatumika kuwahudumia watu ambao hawawezi kutusaidia kwa namna yoyote. 

Nina mashaka hata siku ya hukumu watapewa adhabu ya kwenda jela mwaka mmoja halafu baada ya hapo watarudishwa nchini kwao, sasa ukijumlisha gharama zote ambazo zitakuwa zimetumika  maana at the end of the day watarudi kwao tu, sasa kwanini maamuzi hayo yasifanyike mara wanapokamatwa wakarudishwa kwao muda huo huo??? Na gari linalokamatwa likiwasafirisha mmiliki wake apewe adhabu ya kuwarudisha kwa gharama zake under Tanzanian police escort. Hayo ni maoni yangu, (mchango wangu katika siku ya sheria). Nikutakie mema katika kuendeleza libeneke,

Emmanuel

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. hata ulaya unafikishwa mahakamni na kabla ya kusafirishwa kuna utaratibu hata wa kukata rufaa.uko ulaya ya wapi wewe,jamani waarabu wanasema kukaa kimya ni dhahabu,kama huna la kusema kaa kimya kuliko kuonyesha uongo na kutojua habari.

    ReplyDelete
  2. YOTE ULO ANDIKA NI UPUZI MTUPUU, ROHO MBAYA KABISA. WEWE MWENYEWE WAFANYA NINI NCHI YA WATU KAMA UNAVODAI! WAWACHE WATU WATAFUTE MAISHA KAMA UNAVOTATUFUTA- KUMBAVU KABISA!

    ReplyDelete
  3. Nashukur Mungu tuna watanzania thinkers kama wewe.
    Mungu afungue macho na wale walioko madakani walione,japo nawasiwasi inawezekana pia ikawa ni miradi ya wakubwa kwani ukipiga hesabu wanapswa kula milo mitatu na ina viwango.Usishangae wanalishwa pungufu na huku hesabu zao zinakamilika.
    Nchi yetu siku hizi hata kitu cha kijinga kwa wengine ni dirii kubwa.

    ReplyDelete
  4. Mimi ulietukana nakushangaa,kwan jamaa kafanya kosa lp hadi umtkane? Ni mchango wake ktk hlo,wewe ndo unatakiwa ukae kmya mana hna hoja.

    ReplyDelete
  5. Nyie mnaomwambia mwenzenu kaandika upuuzi mtakuwa wazamiaji maana you cant think out of the box. Kama mtu ni muhamiaji haramu ni kweli hawezi kuzalisha kitu chichite hapa kwetu na muhimu ni yeye kurudishwa kwao, hata kama ulaya wanawapeleka mahakamani its time for them to think out the box. Na sio kila kitu kinachofanywa ulaya tucopy na kupaste Tanzania. Eti hata ulaya wanawapeleka Mahakamani je uchumi wetu na ulaya uko sawa? Think big and Loud.

    ReplyDelete
  6. wewe unayesema ulaya wanapeleka mahakamani! jaribu kutest ukifika airport na utakachokiona ni mahakama or ratiba ya ndege ya kurudi kwenu ili uingizwe. mahakama utaiona ukifika kwenu kwani utapokelewa na maafisa na siyo ndugu zako!!acha warudishwe kwao coz ndio waliosababishwa hata tanzania kuingiziwa VISA kuja UK hawa watu. watafute maisha ila wakikamatwa hamna huruma tena.

    ReplyDelete
  7. Hawa WAhamiaji haramu kweni walikua wanataka kukaa tanzania ama walikua wakielekea africa kusini kama vile vile watoto wenu wa kibongo wanafanya.

    Kweli yanini kuwafunga jela mwaka mzima badili ya kuwarudisha ama wakiomba ukimbizi muwape.

    ReplyDelete
  8. WEWE ULIANDIKIA MADA HII NAKONA KAMA MSHAMBA FULANI WEWE UMEKUJA LINI ULAYA ? AU UNA WIKI MBILI TANGU UFIKE HUKU? UNAONEKANA KANA KWAMBA HUJUI LOLOTE LILE AU UIMELWTWA NA MWANAMKE NA TIKETI YA KULIPIWA?
    KUMBUKA TANZANIA NI NCHI YA DEMOCRACY, INAFUATIA KILA SHERIA KAMA NCHI ZINGINE ZOTE ZILZOKUWA NA SEREKALI. HAKI ZA BINADAMU ZIPO NA ZINAFATILIWA! WEWE HAO WAZAMIAJI UNAFIKIRI SIO BINADAMU, HAWAHITAJI HAKI ? NDIO MAANA BASI KAMA HUJUI . WAMEPEKWA MAHAKAMANI ILI NGAZI HUSIKA ZIWEZE KUSIKIA MALALAMIKO YAO . WEWE UNAJUA KWA NINI WAMEKUJA TANZANIA? KAMA HUJUI BASI UNGEULIZA KWANZA KWA NINI WATU HAO WAMEKUJA TANZANIA MPAKA KUJIFICHA VICHAKANI. HAPA KUNA WAARABU WOTE HAWA UNAOWAONA HAPO DENMARK WALIKUJA KWA NJIA HIZO HIZO MPAKA WAKAFIKA HAPO WALIOFANIKIWA WAMEFANIKIWA NA WALIOKUWA NA BAHATI MBAYA WALIRUDISHWA KWAO ,INATEGEMEA KWA VIPI KILA MTU NA TATIZO LAKE. SIJASIKIA WATU WAMESHIKWA ATI WAHAMIAJI HARAMU HAPA ULAYA, HALAFU WANAPANDISHWA NDEGE KURUDI KWAO BILA KUJUA KULIKONI KWA NINI WAKO HAPO BILA LEGAL PAPERS.

    WEW UNAFIKIRI HAO WATU WEUSI WOTE HAPO ULAYA WALIKUJA NA MAKARATSI KUTOKA KWAO AFRIKA? KAMA HUJUI KITU NDIO MAANA NAKUITA MSHAMBA BADO UNA KAZI SANA YA KUSOMA KAMA UMEKUJA KIMASOMO. DENMARK HAIKUUMBWA KWA AJILI YA WADENISH WAISHI PEKE YAO NA TANZANIA NI HIVYO HIVYO HAIKUUMBWA KWA AJILI YA WATANZANIA PEKEE - WEWE MBONA HUKO HAPO DENMARK UMEKWENDA KUFANYA NINI?AU UNATAFUTA NINI ? MSHUKURU NYERER KWA KUWEZA KULETA AMANI NA MAPENDO BILA SISI WATANZANIA KUBAGUANA KWA DINI WALA RANGI WALA KABILA. KUMBUKA SOMALIA NA ETHIOPIA NI NCHI AMBAZO ZINAUBAGUZI SANA WA HALI YA JUU HIVYO BASI HALI KAMA HIYO IMESABABISHA NCHI ZAO ZIWE NA MATATIZO MAKUBWA KISIASA , ANGALIA BURUNDI NA RWANDA NI NINI KILICHOTOKEA MPAKA MAMILLION YA WATU KUPOTEZA MAISHA? AU HUJUI? SASA KUPELEKWA MAHAKAMANI TANZANIA NI SHERIA ZA NCHI YETU NA NCHI ZOTE DUNIANI KWA ILLEGAL IMMIGRANTS
    KAMA HAWAKUPEWA CHAKULA WEWE ULITAKA WAFARIKI NA NJAA? NA NJAA HIO NDIO WANAYOIKIMBIA! HIVI WEWE BROTHER ZINAKUTOSHA KWELI? WEWE ISHI SASA ULAYA UTAONA MENGI ZAIDI YA HAYO. WEWE HIVI SASA UNAISHI ULAYA KWA HIYO UNASUPPORT USHOGA AU LAA ? INAKUSHANGAZA HALI HIO AU HAPANA?

    WEWE KAKA BADO UNAHITAJI KUELIMISHWA SANA MPAKA UTOE USINGIZI ULIOTOKA NAO HUKO KWENU SIJUI MUSOMA , GOD KNOWS!

    NA HUKO ULAYA WATU KAMA HAO HUWA WANAPELEKWA MAHAKAMANI NA CHAKULA NA NGUO WANALETEWA NA RED CROSS-

    AU NAWEWE NI KATI YA WALE WASOMI WANAOSEMA WAKIRUDI TANZANIA WATAWAUA WATU WOTE AMBAO HAWAKWENDA SHULE NA HAWANA HAKI YA KUISHI, SWAIN MKUBWA SHENZI TAIP
    ALLI K
    mdau mwenge,
    DSM

    ReplyDelete
  9. Haya mnaoishi denmark hizo sampuli za watu kama hao, zimetoka wapi tena !? Nafikiri watu wanaokuja Denmark wamestaarabika na huyo vipi sasa yeye hataki wageni ? Basi awe PIA KJEASGÅÅRD WA TANZANIA ambaye hataki wageni sasa wewe huku umekuja fanya nini si ungekaa tu kwenu huko, sijui mkoa
    gani umetoka wewe. mshamba wa hedi.

    UMEKUJA JUZI NINI,HAPA WEWE DENMARK?
    mdau

    ReplyDelete
  10. Uzamiaji ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo. Wazamiaji wanatoka nchi tofauti, wa makabila tofauti na dini tofauti. Lakini tukumbuke kitu kimoja. Sisi wote ni BINADAMU. Na kila mmoja wetu ana fikra ama mawazo tofauti. Lakini bado tunabaki na sifa hiyo moja ya usawa ambayo ni sifa ya kuwa BINADAMU.

    Mimi kama mimi, hizi tofauti zote zilizopo na ambazo zinatufanya mpaka tunatoleana maneno ya kashfa kama sio kutukanana, zinatokana na kundi la watu toka enzi hizo, ambao wao walikuwa na malengo yao kwa ajili ya manufaa binafsi. Kuna ile falsafa ya hao wajanja inayosema "divide and rule" na ndio maana kutoka Afrika mpaka Asia, Ulaya mpaka Amerika wamenyofoanyofoa viji-nchi na ma-nchi ili kuweza kukamilisha matakwa yao. Tuliobaki tunahangaika kwenda kwenye zile nchi ambazo tunaona zina manufaa ya kutuwezesha kujijenga, na sababu kuu ni kutaka kujikimu kimaisha na kujiendeleza katika hii dunia ya mpito. Kundi hili la kutafuta maisha nje ya mipaka ya nchi zetu lina michepuo miwili, wanaoenda kihalali na wanaotumia "panya road" aka wazamiaji. Ndugu zanguni, msione hao wazamiaji wamependa, la hasha, ni imebidi kutokana na hali kuwa ngumu. Na kama wangekuwa na uwezo basi na wao wangetumia hizo njia za halali au kubaki tu katika nchi zao. Ubinadamu ni kitu cha bure, na kuthaminiana ni katika moja ya sifa zinazotuweka katika kundi la BINADAMU!

    Awe mkimbizi, mzamiaji,n.k., inastahili kujaribu kukumbuka thamani hasa ya kuwepo hapa duniani na hii si zaidi ya kukumbuka kuwa sisi wote ni BINADAMU!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...