Mkuu wa vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akifafanua jambo mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania,Bw.Rene Meza (tatu kulia),mapema leo asubuhi kwenye ofisi za Kampuni ya Clouds Media Group,Mikocheni jijini Dar.Shoto ni Bw.Joseph Kusaga na wa tatu ni Ruge Mutahaba ambao ni baadhi ya viongozi Wakuu wa Clouds Media Group.Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Rene Meza amefanya ziara fupi mjengoni hapo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo.
Mkuu wa vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akimtambulisha mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena, Dina Marios kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania,Bw.Rene Meza.
Baada ya kutembelea vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania,Bw.Rene Meza alipata wasaa wa kukaa pamoja na wakuu wa vitengo mbalimbali na Wakurugenzi ndani ya kampuni hiyo na kuzungumza nao machache ikiwemo mikakati mbalimbali ya utendaji kazi kwa pande zote mbili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. kwa mpiga picha.... sidhani kama umewatendea haki wakuu wa clouds na mgeni wao toka vodacom kwa kuweka picha yao wakiwa mbele ya mlango wa "TOILET" tafadhali tuangalie picha tunazoweka na mazingira yake hasa Back ground.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...