Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akisalimiana na Mzee Kayanza Pinda wakati alipowatembelea jana kuwajulia hali. Kushoto ni Mama Kayanza Pinda ambao ni Baba na Mama wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiwa katika picha ya pamoja na Mzee na Bibi Kayanza Pinda ambao ni wazazi wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nyumbani kwao Kibaoni Wilayani Mpanda Mkoani Rukwa. Mkuu wa Mkoa alikuwa Wilayani hapo kumuwakilisha Waziri Mkuu kwenye mahafali ya Kidato cha sita Shule ya Sekondari Usevya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. HATA KAMA NI MTOTO WA MKULIMA JAMANI, JARIBU KUBORESHA NYUMBA YA WAZAZI WAKO. WEKA TILES, MAKOCHI HIVYO VITI VINATIA AIBU, NDIO WALIOKUSOMESHA KWA TAABU, NI MUDA WAO WA KUONA MATUNDA PLEASE.

    ReplyDelete
  2. KATIKA WAKATI HUU WA KARNE YA 21 SIKUTEGEMEA KAMA BADO TUNA VIONGOZI WANAO TAMBUA UONGOZI NI KAZI YA WITO NA YA KUWATUMIKIA WANANCHI ILI UWE KIONGOZI WA MFANO WA NDUGU PINDA LAZIMA UMTANGULIZE MUNGU MBELE, UMUOGOPE MUNGU NA KUFANYA YALE ANAYOTAKA TUFANYE.KIONGOZI KAMA HUYU ATAPATA WAPI MAMILIONI YA KUCHANGIA KANISA. 1YOHANA3:3-8

    ReplyDelete
  3. kama wa kwetu tu nilijuwa wapo tofauti

    ReplyDelete
  4. Nimeona mahala wanapoishi wazazi wake Waziri Mkuu,

    ReplyDelete
  5. Thanks Engineer! that is how leaders should behave to fellow leaders' families in our community.Stay blessed with your family too.

    ReplyDelete
  6. yaani hamkosi ya kusema jameni lawama tu watz hata kama lingekuwa bangaloo la kufahari mgesema sana. Hataki maskendo baba wa watu labda akishastaafu ndio atafanya vitu vyake huko kijijini. Hat hivyo watz wengi husahau sana kujenga nyumba bora vijijini mwao wanajenga mjini majumba ya kifahari msimseme mwacheni!

    ReplyDelete
  7. Duu! very CHOKEST!

    ReplyDelete
  8. JAMANI ANGEWAJENGEA BONGE LA JUMBA SI MGE SEMA KAIBA PESA ZA SEREKALI ANY WAY YEYE MWENYEWE ANAJUA NINI ANAFANYA MWENYEWE

    ReplyDelete
  9. Wala tusingesema sana kama angekuwa na nyumba ya kawaida ya uhalali. Sijui kama Kutoikarabati nyumba ya wazazi waliokusomesha ndio kuonyesha ukulima jamani, hapana Kwa mshahara wake halali na kipato chake tangu alipoanza kazi nyumba ingekuwa bora zaidi na isiyo na gharama kubwa
    Ni maoni yangu tu

    ReplyDelete
  10. kwa walioishi kijijini wataelewa kwanini waziri mkuu pinda ajaweka hizo tiles zenu na hizo nyumba zenu za kulala na haja ndani
    unajua mimi mwenyewe nikimleta mama au baba yangu dar wanakaa siku 2 au 3 wanasema wanataka kurudi na mara nyingi nilikua naongea nao wanasema haa sasa tutakaa mwezi basi so baadae wanasema tunataka kuku wetu na vitu vingine awapendi kabisa maisha ya kupikiwa mafuta na pia nimewajengea nyumba km hii mzuri ya mjini awakai kabisa badala yake unakuta ni ya wageni hii ndio life style yao wazee wa zamani awapendi mambo ya kifahari km ya kisasa wanaona tabu na wamezoea na ni maisha mazuri sana ndio maana unawaona hapo na ukiuliza umri wao utashangaa so hongera sana mh pinda kwa hili acha waishi wapendavyo bila tabu

    ReplyDelete
  11. Huko sumbawanga ni full ushirikina no wonder PM anaogopa kuwajengea wazazi wake maana ukiwa na maendeleo tu wanakuua kwa uchawi. Anyway anaesema PM ni bahili sana mbona mtoto wake wa kike tunasoma nae hapa Arkansas, USA? Michuzi muogope Mungu usibane hii

    ReplyDelete
  12. Jamani Waziri Mkuu amewekeza kwenye Guest House hapo kijijini kwake kwanza, nyumba ya wazazi atairekebisha tu karibuni.

    ReplyDelete
  13. usanii tu huu,, waetuonyesha banda la mahindi lililosafishwa maalumu kutudanganya sisi wadanganyika...
    hii nimeikataa hata aje nani. ndio nakubaliana na mchangiaji aliyesema wazee wteu hawapendi mabo safi ya vijna wa kileo na mabo ya ushirikina na nin lakn si kwa kiwango hiki.

    ni mtizamo tu

    ahsante
    hsm

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...