Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na jitihada zetu tumefanikiwa kumsafirisha marehemu HAROUN ABDALLAH OTHMAN (Maarufu kwa jina la JAMHURI) ili akazikwe nyumbani.Mwili wa Marehemu utawasili Dar Alhamisi 01/03 saa nane na nusu usiku kwa ndege ya Turkish airline (TK603)
Pamoja na hali ngumu inayoendelea kutukabili watanzania tunaoishi Ugiriki ugumu huo haukuweza kutuzuwia kutekeleza ada na mazowea ya kumsafirisha mtanzania yeyote anaefariki hapa.
Jumuiya ya watanzania ugiriki, inawashukuru wale wote walioshiriki kwa hali na mali katika kumsafirisha mwenzetu.
Tunapenda kutoa shukurani maalum kwa Kaimu Balozi wetu Rome Italy kwa kututumia haraka mno "barua ya uthibitisho" iliyoturahisishia kwa kiasi kikubwa harakati zote za kumsafirisha Marehemu.(N.B. Huduma zote za kibalozi kwa hapa yatubidi tuwasiliane na Italy)
Tunamuomba Allah amlaze Marehemu mahala pema peponi.(Amin)
INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN
Kayu Ligopora
Katibu Mkuu
Jumuiya ya watanzania ugiriki



"Inna Lillahi Wainna Ilayhi Rajioon" Mwenzetu katangulia nasi sote hiyo ndiyo khatma yetu. Mwenyeez Mungu amughufirie kwa yote na amlaze pema PEPONI ameen!
ReplyDeleteINNA LILLAH WA INNA ILAYH RAJIUUUUN
ReplyDeleteNa kila mmoja wetu ataonja Umauti, Ndio Amri ya ALLAH S.W.T,,,AMIIIN.
Innalilahi Wainna Ilayhi Rajiuun...Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kurejea kwake ni haki...Mwenyezi Mungu.Awape subra wafiwa wote Mzee Abdullah shtoto na ndugu wote...Bila kusahau kutoa shukrani zangu za dhati kwa ndugu zangu nyote mliokuweko Ugiriki kwa juhudi na jitihada zetu za kumstiri ndugu yetu huyu. Mwenyezi Mungu akusahilishieni katika maisha yenu nyote na akuzidishieni wepesi kwa kila hali...Udumu udugu wenu na imani zenu.
ReplyDeleteInna Lillah Waina Ilayhi Rajoon
ReplyDeleteMungu amlaze pema my man Karabi.
ReplyDeleteNi mmoja wa vijana waliofanya mtaa wa Kikwajuni kuwa kikwajuni enzi hizo.RIP bro.