Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (SACP),Mohamed Mpinga akizungumza mapema leo jijini Dar,mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya usalama barabarani (pichani chini),iliyoandaliwa na Rotary Club wakishirikiana na Jeshi la Polisi,kitengo cha Usalama Barabarani sambamba na makampuni mbalimbali ikiwemo na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel.Kamanda Mpinga amewashukuru sana wadau wote waliojitokeza kuunga mkono kampeni hiyo ambayo ni mahususi kabisa katika suala zima la kupambana na kuhakikisha ajali zinapungua barabarani kadiri iwezekanavyo.
Kampeni iliozinduliwa leo,baada ya kuandaliwa na Rotary Club na kushirikiana  na Jeshi la Polisi,kitengo cha usalama barabarani sambamba wadau mbalimbali.
 Mkurugenzi Miradi wa Rotary Club,Bw.Zainul Dossa akiwashukuru wageni waalikwa mbalimbali waliofika na kuifanikisha hafla ya uzinduzi huo leo jijini Dar.Picha zaidi bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. SAWA SAWA MANDALO NA ROTARY WABONGO NA KIMOBO IMEKUWA TABU SANA SIKU HIZI.
    WATU HATUJUI NINI MADHARA YA KUENDESHA GARI HUKU UNATUMIA SIMU AIDHA KWA KUTUMA UJUMBE AU KUONGEA.
    KWA NINI HATUZIMI SIMU KABLA YA KUWASHA GARI ILI KUONDOKANA NA KUPOKEA SIMU HUKU UKIWA KWENYE CHOMBO CHA MOTO?
    KUNA MADEREVA WAJUZI WA KUENDESHA MAGARI TENA KWENYE MBIO ZA MILIMANI HUKO TANGA, KENYA , DAKAR RALLY, YOU NAME IT LAKINI CHOMBO KIKIKATAA KINAKUPELEKA KINACHOTAKA NA KUCHUKUA MAISHA AIDHA YAKO AU YA WATU WASIO NA HATIA.
    ILI KUKOMESHA HII TABIA, SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA POLISI IKAMATE MTU YEYOTE ATAKAEKIUKA AMRI HII, AFIKISHWE MAHAKAMANI NA KUNYANG'ANYWA LESENI. HILO NDIYO FUNDISHO.
    SI SIMU TUU. PIA KUNA TABIA YA MADEREVA KUENDESHA GARI WAKIWA MBWIIIII WENGINE HATA KUSIMAMA HAWAWEZI. AKIINGIA GARINI NA KUSHIKA USUKANI, ALLAHU YA'ALAMU WASO HATIA.
    KAMA RUSHWA IKIPIGWA VITA, KAMPENI HII ITAFANIKIWA. MANAKE NDIYO ITAKUWA YALE YALE; "MAMA MANDIMBO WEKA CHUNGU NAKUJA NA KITOWEO SASA HIVI". MJOMBA KATIA MAGWANDA ANAWINDA SALENDER BRIDGE MUDA SI MREFU ANARUDI NA MIZIGO. BONGOOOOO WEEEE TUNATISHAAAAA. DUH!

    ReplyDelete
  2. Madereva wa Tanzania ifike wakati wafahamu maana ya pundamilia(mistari inayomruhusa muendesha gari kusimama na mwenda kwa miguu kupita).Kwani haina maana kusuburi gari lipite kwenye pundamilia wakati ni haki ya mweendesha gari kumsuburi mwenda kwa miguu kupita.

    ReplyDelete
  3. Wabongo kuwaambia wasitumie simu wakati wanaendesha magari ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Bongo ukionekana unaendesha gari huku unazungumza kwa mbwembwe kwenye simu au kutuma SMS inachukuliwa kama ni ishara ya mafanikio na utajiri.

    ReplyDelete
  4. Mdau namba 2 nakubaliana na wewe. Eti ukisimama kwenye pundamilia madereva wengine nyuma yako wanakupigia honi kama wewe ndiyo umefanya makosa.

    Na hiyo simu ndiyo usiseme tena. Mara kadhaa naona madereva wanayumba barabarani tena wakati ule wa heavy traffic. Ukimpita halafu ukaangalia utaona anasoma au kuandika message na wala hajali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...