Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akitoa neno lake la shukrani katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Kushoto ni Mhe. Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga G.K. Rwakibarila na Mhe. Jaji Pellagia Khaday wa Mahakama Kuu Kanda hiyo.
 Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Kanali John Mzurikwao, Mhe. Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga G. K. Rwakibarilla, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya, Mhe. Jaji Pellagia Khaday wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, na Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda ya Sumbawanga Prosper Rwegerera wakiangalia Kwanya iliyokuwa ikitumbuiza katika Sherehe za Siku ya Sheria Nchini Leo.

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. G.K. Rwakibarila akikaribishwa kukagua Gwaride maalum lililoandaliwa kwa heshma yake katika kuadhimisha Siku ya Sheria Nchini Mkoani Rukwa Leo.

Mhe. Jaji Mfawaidhi G. K. Rwakibarila akikagua Gwaride hilo.

Gwaride maalum lililoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa kufanikisha Siku ya Sheria Mkoani humo likitoa salam za heshma kwa Jaji Mfawaidhi Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga mara baada ya kukaguliwa.

 Mhe. Jaji Mfawidhi akiteta jambo na wenzake mara baada ya kukagua Gwaride la heshma.Picha zaidi Bofya Hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hongereni Rukwa nyie sio Mkoa wa pembezoni tena mnakuja juu, ngoja barabara ije

    ReplyDelete
  2. wounderfull, Rukwa is coming now with new face is no longer tupa uchawi

    ReplyDelete
  3. Michuzi naomba hii comment yangu usiitupe kapuni!!!Tanzania hamna sheria na upotezaji wa muda na kodi ya wananchi kufanya hiyo siku ya sheria huko Tanzania.Sheria ya Tanzania imeendikwa vitabuni lakini utekelezaji wake ni wa mashaka sana.Huko polis na mahakama,mahakimu ndio wanuka rushwa.Ukiwa na kesi na una fedha ni ngumu sana kufungwa,au ukifungwa ni kiini macho na huko gerezani unaweza ishi kama mfalme,unaonga kuanzia bwana jela hadi mkuu wao.Inatia kichefuchefu na hasira nilikuwa na ndugu wa kribu waliopatwa na matatizo ya kupigwa na kuporwa mali zao,kiasi cha kutaka kupoteza maisha yao, na waharifu wanajulikana na walikamatwa na ushaidi huko,ila waharifu walikuwa na ndugu wenye vyeo na fedha,walitoa rushwa na waliachiwa huru na kesi ikaanza kupigwa danadana.Hadi leo hii kesi imekwishwa.Inatia uchungu sana.Wale ndugu walipata bahati ya kuja ughaibuni,hawataki tena kusikia nchi ya kichefu chefu kama Tanzania,uraia wao walichaukana na sasa wana maisha mazuri tu huku!
    Msema kweli Australia

    ReplyDelete
  4. sasa hawa kina ras makunja wamependeza kweli kwali,sema tu muziki wao ni wa kialamia sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...