Beki wa timu ya Taifa ya Congo, Issama Mpeko akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Stars, Uhuru Seleman wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 0-0.
Mshambuliaji wa Taifa Stars, Nsa Job (kulia) akichuana na beki wa timu ya taifa ya Congo DR, Mampuya wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 0-0.
Hekaheka katika lango la Congo.
Kocha wa timu ya Taifa Stars, Jan Poulsen (kulia) akipeana mkono na kocha wa timu ya taifa ya Congo, Claude Le Roy baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 0-0.Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii.
Safi sana kocha Poulsen, timu uliyoichagua ni nzuri, angekuwa Maximo angetuharibia tu na visingizio vyake kibao -ooh timu haina vijana, mara haifundishiki, ooh haina nidhamu, mara ohh wachezaji wangeanza kufundishwa wangali wadogo.
ReplyDeleteTaifa Stars imeoza naamini hata ikipambanishwa na dada zao Twiga Stars haitoweza kushinda, nadhani umefika wakati tuelekeze nguvu zetu zaidi kwa hawa Twiga badala ya kuendelea kupoteza muda na hela nyingi kwa ajili ya hawa wachezaji wasiojitambua!
ReplyDelete