Kwa mara ya kwanza wanafunzi wote waliomaliza Kinondoni Muslim wanaalikwa katika re union kinondoni muslim siku ya Jumamosi tarehe 17 March Cine Club Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10.00 jioni.Kamati maalum ya kuratibu mkusanyiko huo imekwishawasiliana na uongozi wa shule pamoja na taratibu nyingine.
Nia ni kuchangisha fedha kwa ajili kuisadia shule yetu halkadharika kufahamiana wapi tulipo.Ukisikia au kusoma taarifa hii mwarifu na mwenziyo.
Kwa mawasiliano zaidi:
Vumi Cast 0756 232821,
Abbas Mbonga 0754 397520
Usikose nafasi hii pekee ya kukumbukana
Jamani wana - Kinondoni wenzangu, jitokezeni kwa wingi tujadili pia namna ya kupunguza division iv na ziro.
ReplyDeleteSikumbuki ni mwaka gani na sisi tulitoa division 1 angalau 5.
Abdulkarim S.
Mafia
Mbunge wa Mafia usikose kuhudhuria, wewe ni mwenzetu na tunakuhitaji sana.
ReplyDeleteKama utakuwa na udhuru basi tutumie mchango wako wa angalau vijisenti vimilioni kumi tu.
Abiola Jr.
Mafia kiduka cha juice
Ahsante Wadau kwa Mpango Muhimu sana wa ALUMNI:
ReplyDeleteMohamed Msekeni
KINONDONI ALUMNI
CLASS OF-1990
E-mail:msekeni1@aol.com
Imekaa vizuri!
ReplyDeleteItafaa kama tutawatafuta
1.Head Prefects/ Head Boys wote.
-Nyosingo Nyagwegwe/Afternoon-1988.
-Magoma Magenda/ Morning/Afternoon-1990.
2.Waalimu na Wafanyakazi wa Shule.
-Hoya,Makakala,Ben,Mtenga,Semkuya,Shombe,Shariff,Jariwala e.t.c
3.Wachezaji wa Timu ya Shule ambao wengine walifika mbali Kisoka hadi Yanga na Simba.
-Athumani China/Yanga
-Wicki Mbungunde/ Sigara
-Moshi Majungu/ Yanga/Sigara
Bila kumsahau Mhindi mfupi Manish.
Kama wapo hai kwa miaka yote iliyopita nyuma.
2000's, 1990's, 1980's and so on.
AHSANTE WADAU:
ReplyDeleteKinondoni Muslim Secondary School ,kwa idadi ya Waliohitimuali ambao wapo sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi wanaweza fikia idadi ya watu ktk Jiji kubwa, Wilaya au Mkoa tokea mwaka 1967 au 1972 hivi Shule ilipoanzishwa!.
Lengo la Suala hili ni:
1.Kuchangia Shule yetu,
2.Kufahamiana ni wapi tulipo n.k,
Ninapendekeza hivi:
Kwa Waliokuwa Ughaibuni nchi mbali mbali Duniani na Waliomaliza Kinondoni miaka tofauti ni muhimu washirikishwe ktk Mkusanyiko hata kama hawapo wakitaka Majina yao watume ili yaorodheshwe kwa Wahudhuriaji wa Mbali (Virtual Attendees).
Kwa Uratibu zaidi:
1.Wahudhuriaji wa Mbali wanaweza pangiwa utaratibu wa kufikisha chochote ($$$) walichonacho mkononi ili kufikia lengo la suala hili.
2.Wahudhuriaji wa Mbali watapangiwa utaratibu wa kufikisha taarifa zao ni wapi walipo Duniani.
ILI KUWA NA MTANDAO ENDELEVU KWA SIKU ZA BAADAE KWA FAIDA YETU SOTE.
KINONDONI MUSLIM:
ReplyDeleteTuko pamoja!
Bila kuwasahau Wadau muhumi sana wa Shule ni wale Wauza ice cream ,juisi, Wakaanga mihogo na Chips kule nyuma ya Shule walikokuwa Wanafunzi wanajikomaza wakati wa break ili kukata makali ya njaa na kiu na kukabiliana na masomo madarasani!
Hawa watu kama watakao patikana wapo hai ni muhimu wawepo.
Ktk shughuli hii tusiwasahau ''Mapusha wetu wa kete'' kule nyuma ya Shule Kinondoni Shamba na Kinondoni Moscow.
ReplyDeleteAtafutwe Pusha COZZA LEE-Kinondoni Shamba wa miaka ya 1984-1990 na Mapusha wengineo kwa miaka tofauti Kinondoni Secondary.
Isipokuwa kama wapo TAFADHALI....''TAHADHARI WAFIKE ILA WASIJE NA MIZIGO YOYOTE WAKAFIKIRI WATAFANYA MAUZO KUKUMBUKA ENZI ZAO LA HASHA'' Tumesha kuwa watu wazima sasa tuna majukumu na tuna jiheshimu hiki ni Kikao cha Maendeleo,Kutambuana,Kukumbukana na Heshima!
Hivi ECHESS CAFE ya Kinondoni A ipo?,,,Duhhh Bongo niliondoka mwaka 1985 niko Ughaibuni sijarudi nyumbani tokea nimalize Kinondoni Muslim Secondary School mwaka 1984.
ReplyDeleteWEWE MICHUZI KUTIA KAPUNI KAPUNI MAONI YATU KAPUNI HATA YA MAENDELEO YETU WANAKINONDONI NA TAIFA KWA UJUMLA. NJOONI KWA WINGI WANA KINONDONI TUONYESHE MFANO KWA TAIFA KWA UJUMLA. MIMI NI MUHITIMU WA 1981 JAPO NIKO MBALI NA NYUMBANI KWA MUDA MREFU NATARAJIA NITAHUDHURIA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE. NAWAHIMIZA AKINA MFAUME NYINGI, SEFU MATESA, GEBO PETER, JAMUHURI KIWELU, RASHID SALUM, USTADH ABDALLAH SALIM , MWANAMAKA NA WENGINEO SHIME WANA KINONDONI TUFANIKISHE MAENDELEO HAYA.
ReplyDeleteMimi pia ni wa 1981 enzi za uncle J,Ngunangwa,Jariwalla,Manjunath,Shombe, Shariff,hawa ni baadhi ya walimu wakati huo,najua baadhi ya wenzetu mpo sehemu mbalimbali hivyo sio vibaya tukawasiliana kufanikisha jambo hili,nawakumbuka sana akina Msabila Fundikira,Julius Makelemo,Hamid Masikini,Gebo Peter,Jamuhuri Kiwelu,Abillahi,Mohamedi Mohamedi,Mahaba Mbega,Agib Tale,Jane sesoa,sallu sammy,Patrick Mbumi na pia tuwakumbuke wenzetu ambao hatunao tena kama Jaffary Sunday.
ReplyDeleteAnkal,
ReplyDeleteIli kukuza tija kwa mahudhurio makubwa na makusanyo zaidi pana hali hii hapa chini:
AZMA KUU YA HILI SUALA NI USHIRIKISHWAJI WA WENGI KADIRI IWEZEKANAVYO ILI KUKUSANYA ZAIDI NA KUFIKIA LENGO KWA UFANISI ZAIDI.
1.Wapo waliopo nje ya nchi.
-Ikiwezekana kila nchi Duniani America,Canada, Europe nchi zote pawe na mawakala wa kutangaza na kuratibu Wana Kinondoni na mchakato mzima.
2.Wapo wengine nchini ila hawafikiki kwa njia kama ya Globu ya Jamii na Libeneke.
3.Ushirikishwaji na Mfumo wa kukusanya/ kuratibu Mahudhurio kwa watakaofika na watakao taka kufuatilia wakiwa mbali (Virtual Attendees)
1.INGEFAA SHUGHULI ITANGAZWE KUPITIA VYOMBO VINGINE VYA HABARI,TV,RADIO,MAGAZETI, FACEBOOK,TWITTER N.K ILI KUWAFIKIA WENGI KADIRI IWEZEKANAVYO.,,,ISIPOKUWA MAENDELEO YA MCHAKATO MZIMA YATAKUWA HEWANI KUPITIA GLOBU YA JAMII KIPINDI HADI KIPINDI...((((NA NDIO ITAKUWA FURSA KWA WASIOFIKIKA KTK LIBENEKE KUINGIZWA KUTUMIA LIBENKE,,,LIBENEKE OYEEEE)))).
2.KWA WALIOKO MBALI NA NCHI TUANGALIE UWEZEKANO WA KUWAPA FURSA YA KUSHIRIKI AU KUSHUHUDIA KUPITIA (ICT) yaani (Information and Computer Technology) kwa njia ya Teleconferencing facility ambayo pale IFM (Insitute of Finance Management)Dar ipo,,,hii itawezesha Walioko mbali kushiriki na kushuhudia live!