Ufanyaji kazi wa hawa jamaa wanaojishughulisha na ufungaji wa magari yanayopaki sehehu isiyoruhusiwa hata sio mzuri,sijui huwa wanatumia vigezo gani kufunga magari hayo,kwa maana ukiangalia kwa makini picha hizi utaona magari mengi tu yamepaki kwenye laini hiyo hiyo ilipo gari hii tena yamewekwa hapo kwa muda mrefu kuliko hili ambalo ni mtu tu kaingia dukani maramoja na kutoka.sasa sijui inakuwaje hii??
Cheki wanavyolilazimisha chuma lao kwenye tairi la gari,hivi kwa mfano kaliharibu gari hili,wanauwezo wa kulipa kweli hawa??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Nawe kwanini u park sehemu isiyoruhusiwa? Au unaiga tembo kunya? Acha watu wafanye kazi zao bwana, maana nyie kwa kulalamika tu kofia nawavulia.

    ReplyDelete
  2. dawa yake ndogo tu, USIEGESHE GARI SEHEMU ISYOTAKIWA!!! Period.......

    ReplyDelete
  3. hawa nao viherehere tuuuuuuu barabara zenyewe chache watu wapaki wapi???? watengeneze barabara sasa kazi kutafuna pesa tuu barabara zetu mbovuuuuuu hasa ya kwenda dar kuna sehemu ina makorongoooooo nchi hii kwishney

    ReplyDelete
  4. Hao jamaa ni wala rushwa kuliko Traffic mnaowasema kila siku, wao wanakula hadi Laki 1 vinginevyo ukalipe 150,000,nilikuwa Dar majuzi wakanikamua TZS 40,000 mitaa ya shule ya uhuru,nilikuwa nanunua charger ya simu ya sh.5000 dukani!!..haaa haaaa nilikuwa na haraka..ikabidi nivunje sheria,nitoe rushwa!!!..haa haaa.Hapo nadhani ni mitaa ya shule ya Uhuru.

    Mimi ninacholalamika siyo kukamatwa suala ni kwamba hakuna vile vibao(Zile P au P yenye msitari)siyo kwamba kila anayeendesha Daresalaam ni mweneyeji,kwa hiyo jiji lijitahidi kuweka vibao kila sehemu ambako ama gari zinatakiwa kupark au La basi.Siyo mambo ya kuviziana,kuviziana kunasababisha rushwa.

    David V

    ReplyDelete
  5. Tatizo ni nikutofuata sheria kama mtu anafuata sheria mambo mengine asingekuwepo na hakuna haja ya kuifunga gari maana kama gari limesajiliwa na mamlaka inayo usika tunajua lazima mwenye gari anayo acaunt yake benk kama kumpiga faini unamkata ukouko kuliko kuleta usumbufu usiyo kuwa walazima sehemu zote duniani wanafanya hivyo uwezi kununua gari kama huna caunt benk mwenye gari akifanya kosa wanamkata kupitia kwenye acaunt yake

    ReplyDelete
  6. Mbona Samaora Avenue hawapagusi????.....

    ReplyDelete
  7. Hao huwa wanalisti ya magari ambayo yalikimbia kulipa parking fees kwahio wakilikuta ni kulifunga tu sio lazima liwe limepark vibaya.

    ReplyDelete
  8. Kukata faini kupitia benki? Nchi hii haina mfumo, na magari yanahifadhi vingi. Anayetumia gari hilo utakuta ni mmiliki wa tano na kadi haijabadilishwa chochote kile upo hapo?

    ReplyDelete
  9. hiyo pia arusha ilikuwepo lakini maandamano ndiyo yaliyotoa huu ujinga wa wrong parking. Sisi tulisha wasahau manake wakikosa wanatafuta kosa lolote wanakufungia chuma

    ReplyDelete
  10. This parking fee business should be stopped... a few private people benefit from it at the cost a vehicle owners and general public.. it is a shame that one is charged 1,000 tshs in Iringa for parking where no service (vehicle security) is offered in return.. Tanzania could learn from west africa where the parking business is managed by jobless youth who also protect your car and find you a parking spot! Hawa majaa wetu wanajua kujitokeza kuchuka pesa tu!

    ReplyDelete
  11. Utajuaje kuwa sehemu hii haitakiwa kuegesha gari bila kuona alama za barabarani?.

    Mfano No parking sign na vibao vya kukataza ha kibao peke yake hakitoshi unatakiwa kuonesha kibao kinakata sehemu gani.

    Kuchora mistari ya njano miwili pembeni ya barabara ni alama ya kukataza kupaki eneo hilo any time. Msitari mmoja wa njano ni kuruhusu kupaki kuanzia saa kumi na mbili jioni mpaka asubuhi na jumapili full time. Msitari mweupe usio continuous unaruhusiwa kupaki. Sasa barabara hiyo mtu umetoka sumbawanga Arusha unapoishi umekuja Dar utajuaje kuwa huruhusiwi kupaki bila alama za barabarani?.

    Huu ni mradi wa kipuuzi sana, watu wanaacha kuonesha watu cha kufanya na kuwawinda ili walipe fine. Nafikri lengo la fine si kukusanya mapato bali ni kuhakikisha taratibu za jiji zinafuatwa.

    Mi simlaumu dereva nalaumu watendaji wa jiji kwa kuliacha jiji kama mtoto yatima. Hawafuatilii nini kimefanyika wapi na kinatakiwa kufanyiwa nini, wanawaza madili ya ufisadi tu.

    ReplyDelete
  12. Ukiegesha gari sehemu isiyo takiwa hilo ni kosa lako na hiyo ni kosa la ki-trafic ambayo faini yake ni tsh 30000 na si vinginevyo, kwa hiyo hao jamaa wanavunja sheria tuu, wamepewa kibali na manispaa ya kufanya hivyo ila ni makosa maana hiyo unatakiwa ukalipie trafic na sio kwao, hivyo tuwe tunajua hiloo. Arusha hakuna hiyo maana watu walii-suu manispaaa kwa kuvunja sheria ndio wakawaondoa hao jamaa, unatakiwa kukamatwa na Trafic kwa ajili ya wrong parking na faini yake ndio hiyo hapo.

    Tuwe makini watanzania.

    ReplyDelete
  13. Nadhani hamujamuelewa mdau. Kama hamuwajui hawa jamaa watawakomesha na nyie. Utapaki gari pamoja na watu wengine, la kwako litafungwa na watakung'ang'ania vilivyo. Kwanza maeneo hayo hayana alama ya No Parking. Wateteeni tu hawa wezi, lakini ipo siku mtakoma ubishi....

    ReplyDelete
  14. Na siku hizi wale wenye ma-breakdown mabovu nao wamenzisha mtindo wa kuvuta magari yaliyoegeshwa pembeni ya barabara mbali na katikati ya mji. Hii naiona sana barabara ya Shekilango, Dar es Salaam. Kuna siku walivuta magari kama 50. Cha ajabu ni kwamba hakuna sehemu yoyote yenye ishara (vibao) inayokataza watu wasipaki magari pembeni ya barabara hiyo. Yaani siku hizi watu wanakurupuka tu na kuamua kutafuta pesa kwa mabavu. Serikali iwe makini na mambo haya kwani uvumilivu una kikomo.

    ReplyDelete
  15. Kweli wabongo mnachekesha..yaani mmezoea kuvunja sheria mpaka mtu akivunja sheria mnamtetea? Kweli upunguani ni kitu cha ajabu...!!

    ReplyDelete
  16. Hao ni viherehere tu hawana njia ya kupata overtime (bakshishi) wanavizia makosa!!!kwani hilo ndilo tatizo la msingi kuliko maatizo yote yajiji???Mbona barabara zimekatwa wiki nzima hawazibi viraka??
    Wii mtupu

    ReplyDelete
  17. ANON WA Wed Feb 22, 06:18:00 PM 2012

    Watu wanachokiongelea siyo kuvunja sheria bali ni biashara ya kuviziana. Sheria ya barabarani ya mwaka 1973 iliyofanyiwa marekebisho madogo sanaya kurasa nne mwaka 1990, inaweka wazi kuwa barabara inatakiwa kuwa na alama za kuwaelekeza watumiaji nini kinatakiwa wakiwa wanaendesha wapi.

    Ukaingalia hapo ni barabara ambayo hakuna alama yoyote ile inayokataza parking wala ianayokubali parking. Maana yake ni kwamba mtumiaji anaweza chagua cha kufanya.

    Inabidi sasa tuanzishe chama cha wamiliki wa magari Tanzania ili kulazimisha mamlaka kuweka alama barabarani. Mtu akipaki sehemu yenye alama inayokataza anatakiwa kulipa.

    Tatizo kuna watu wanaona huu ni mradi na kuwaambia watu kwa kuweka alama sahihi maana yake wengi hawatavunja sheria na hivyo mapato kupungua.

    Lengo liwe kuufanya mji kuwa mahali pazuri pa kuishi kwa kufuata sheria siyo kuuchafua mji kwa kulazimisha watu kuvunja sheria ambayo kwa ujumla si kuvunja. Mimi nntajitolea kuwa sacrificial wakinifungia nitawaomba wanipeleke mahakamani na kuweka wakili hata kwa tahamani ya mara alfu ya hela ya fine ili kutaka mahakama itoe hukumu ya kuwataka wasikamate mtu kama hakuna alama za kuakataza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...