Home
Unlabelled
UNAWEZA GUNDUA NINI KWENYE PICHA HII??
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
tumewekwa mbali na marekani?
ReplyDeleteyetu kubwa sana?
???
Ankal
ReplyDeleteBendera ya Tanzania imegeuzwa, mistari ya njano na nyeusi huwa inaanzia kwenye mlingoti na kushuka chini upande unaopeperushwa sana na upepo, kilichotokea ni kuwa kamba iliwekwa vibaya.
Bendera ya US iko kichwa chini miguu juu, bendera ya Bongoland iko migulubaja!
ReplyDeleteBendera zote zimepauka isipokuwa ya Tanzania
ReplyDeleteBendera yetu imewekwa chini juu. Na hili ni kosa ambalo limekuwa likirudiwa rudiwa sana hasa kwenye ofisi za kibalozi na taasisi za umoja wa mataifa. Wanaohusika watoe elimu hiyo!
ReplyDeleteflags are upside down!
ReplyDeleteSimple. Hizo nyingine tatu vibaraka wa hiyo ya kwanza.
ReplyDeleteUSA flag, ipo nyumambele hahaha
ReplyDeleteBendera ya marekani imegeuzwa upside down....by obamamtoto
ReplyDeletempandisha bendera ya tanzania alikuwa na haraka,imefuata upepo tuu. hahaaaa
ReplyDeleteHivi hiyo bendera ya marekani haiko upside downkweli.
ReplyDeleteHapo utagunduwa hiyo bendera ya Marekani imewekwa ndivyo sivyo (juu chini, kulia kushoto) na huo mlingoti mwingine ndo mtupu, hauna japo tambara.
ReplyDeletebendera ya marekani iko juu chini,nyota hizo zinatakiwa kuwa juu
ReplyDeleteupside down
ReplyDelete1.)Bendera Hizo ni Za Marekani,Kenya,East Africa Community and Tanzania.....
ReplyDelete2.)Tatu kati ya Hizo zimepauka ya Tanzania tuu ndio Haijapauka
3.)Bendera ya Marekani imegeuzwa iko juu chini
4.)Milingoti ipo SITA.....
Bendela ya taifa la marekani imetundikwa juu chini
ReplyDeleteNchi mbili za Jumuiya ya Afrika Mashariki bila kuwepo Uganda na badala yake kuna Bendera ya Marekani.
ReplyDeleteDuh! bendera yetu ya taifa ipo upside down! who is responsible????!!! ni aibu kweli!
ReplyDelete1.Mlingoti mmoja hauna bendera.
ReplyDelete2.Kuna bendera 4.Ya Marekani,ya kenya,ya hotel huska,na ya Tanzania kwa mfuatano.
3.Bendera 2 ya Marekani na ya Tanzania zinapepea clock wise ie.kuelekea kulia na bedera 2 ya hotel husika na ya Kenya zinapepea ant clock wise ie.kuelekea kushoto
4.Kuna milingoti ya bendera mitano.
5.Bendera ya Kenya mlingoti wa tatu haija kusa kipivoti cha mlingoti.
Asante.
kawatundika kichwa chini miguu juu wamarekani!
ReplyDeleteBendera y a USA iko juu chini.
ReplyDeleteNadhani bendera ya USA, Kenya na ya Tanzania zimegeuzwa juu chini!
ReplyDeletehiyo bendera ya Marekani hicho kibox chenye nyota 52 hakikaagi hapo chini huwa kinakuwaga juu pembeni upande wa kushoto..... Mdau wa siku nying Texas USA
ReplyDeleteHizi bendera zimetundikwa juu chini (zinaangalia chini)
ReplyDeletean "odd" combinations anyways, Minofu stars and stripes imepinduliwa kichwa chini mijuu guu! lol! Thanks
ReplyDeleteBendera ya America imegeuzwa kichwa chini mijuu guu.
ReplyDeleteBendera ya Marekani imegeuzwa. By ComWiz1
ReplyDeleteBendera ya marekani iko upside down.heeee!
ReplyDeleteBendara ya Tanzania imefungwa chini juu. Inaitwa kwa kimombo "Flag desecration" au Flag Abuse (bofya link hapo chini kwa habari zaidi)
ReplyDeleteKuna nchi ambazo zina sheria haswa inayosema bayana kuwa kuidhihaki bendera ya nchi hiyo ni kosa. Je Tanzania kitendo hicho ni cha kuvunja sheria? na ni sheria ipi haswa?
Ankal, si ajabu kuwa mfunga bendera huyo wala hakujua kuwa amekosea kufunga bendera kwani elimu na ufahamu wetu wengi ni duni sana.
http://en.wikipedia.org/wiki/Flag_desecration
Alex bura, dar
Ze Benderaz upside down!
ReplyDeletesi useme tu kwani imekuwa chemsha bongo? Kuna mambo mengi kwenye picha:
ReplyDelete1. Milingoti miwili haina bendera;
2. Bendera zilitakiwa ziwe za uganda, kenya, Tanzania, Rwanda na Burundi na marekani! za TZ, Ke, sijui, marekani na ipi vile?! ndiyo zipo;
3. Tafsiri ya nbr 2 hapo juu malizia
nmegundua nguzo moja haina bendera
ReplyDeletebendera imepinduliwa! Sioni ubaya li nchi lenyewe si la kupindua pindua tu kwani nani anajali?
ReplyDeletebendera zote ziko upside down
ReplyDeleteupside down
ReplyDeleteMambo mawili. Kwanza, bendera ya USA imewekwa miguu juu..maanake nchi imepinduliwa. Pili, nadhani jamaa alitumwa akaweke bendera ya U-ganda akaenda kuleta ya U-SA.
ReplyDeleteAnonymous Allen Natai :)
Naweza kugundua kwamba mtoa mada ana "agenda" maana kuuliza tutagundua nini kunaashiria tayari muhusika amewaza kitu. Labda angetueleza amewaza nini alafu na siye tuchangie. Au siyo wadau?
ReplyDeleteBendela ya marekani imegeuzwa juu chini
ReplyDeleteBendera ya Tanzania imegeuzwa
ReplyDeleteBendera ya nchi yangu Marekani imewekwa chini juu, na pia TZ japo ina bendera yake lakini si nchi ya kujivunia kutokana na uongozi mbaya.
ReplyDeleteNimawazo yangu, nimegundua kwamba Tz niyamwisho kwa kila kitu
ReplyDeleteBendera ya marekani imegeuzwa!
ReplyDeletebendera ya marekani na kenya zinapepea lakini ya bongo imekataa kupepea nadhani imezingwa na bendera nyingine haipati upepo wa maana
ReplyDeletebendera ya tanzania hiyo rangi ya buluu inatakiwa ikae juu na hiyo ya kijani ikae chini
ReplyDeleteimegeuzwa.
Duuh jamaa wamegeuza bendera ya Marekani up side down. Ni vema wangeuliza kabla ya kupandisha bendera hizo endapo wangekuwa hawana hakika. Hayo ni makosa makubwa.
ReplyDeleteUS Flag iko upside down
ReplyDeletemkuu, bendera ya Obama haijawekwa sawa. It's upside down!
ReplyDeleteNilijua wanakosea kwa kutotambua bendera ya nchi yao kumbe hata ya Marekani haitambuliki inakaa vipi kwa urahisi wake.
ReplyDeleteTupo tupo tu.
Huyu mtu aliyepandisha bendera hizi nadhani tayari alikuwa amepata chupa kadhaa za ulabu!au kama ana makengeza basi macho yake ni kama ya mijusi au ya kuku,haiwezekani bendera zote tatu za U.S.A, U.R.T na E.A.C ziwe upside down.Michuzi umetunyima haki ya kujua uzembe huu umetokea wapi,ilipaswa utujuze ili wahusika wawajibike au wawajibishwe kwa namna moja au nyingine
ReplyDeletebendera ya Marekani iko kichwa chini au macho yangu tu sina uhakika
ReplyDeleteBendera ya Marekani wameibanjua chini juu!
ReplyDeletebendera ya marekani imewekwa juu chini, sehemu ya bluu na nyota nyeupe ilipaswa kuwa juu, ni kosa la kiitifaki
ReplyDeleteBendera ya Marekani wameiweka kichwa chini miguu juu!. Kaaaazi kwelikweli.
ReplyDeleteBENDERA ZOTE ZIMEGEUZWA UPSIDE DOWN
ReplyDeleteBendera inegeuzwa kichwa chini miguu juu ..............ndio maana inabidi turudishe JKT au mnasemaje wadau??
ReplyDeleteNaona bendera ya kenya imepauka na hiyo ya pili kutoka ya TZ choka mbaya,,na lingine upepo ulivuma kweli kweli na zikavuata mkondo..
ReplyDeleteBendera ya Marekani imegeuzwa blue na hizo nyota zinatakiwa ziwe juu kushoto
ReplyDeleteflag ya U.S.A imegeuzwa up-side-down..
ReplyDeletebendera ya bongo ina kasoro kwenye kamba
ReplyDeletebendera ya bongo ina kasoro kwenye kamba
ReplyDeleteBendera ya USA imewekwa juu chini. Nyota zinatakiwa ziwe juu na sio chini.
ReplyDeletenimegundua kuwa aliyepandisha bendera anaundugu na OSAMA kwahiyo ameamua kuiweka kichwa chini bendera ya marekani.
ReplyDeletenyota za bendera za marekani zinatakiwa ziwe juu na pia bobgo inaonyesha imeshika mkia pia kwenye milingoti
ReplyDeletebenderani zimegeuzwa chini juu?
ReplyDeleteBendera ya America imegeuzwa.
ReplyDeleteBendera ya Marekani imepinduliwa chini-juu.
ReplyDeleteamerican flag fly upside down!!! so funny!
ReplyDeleteamerican flag fly upside down!!! so funny!
ReplyDeleteHahahaaaaaa!!!! Naona bendera ya Obama haija tendewa haki.....
ReplyDeletenaona huyo aliyopachika bendera ya marekani ana bifu nayo
ReplyDeleteduh!!!!! safi sana us flag juu chini chini juu
ReplyDeleteMwenye hoja ya bendera, siku zijazo tafadhali badilisha Kiswahili ili iwe:
ReplyDeleteUNAWEZA KUGUNDUA NINI KWENYE PICHA HII?
Maelezo:
Unapotumia kitenzi (verb) kilichofanyiwa unyambulishi (conjugation), na kisha kikawa kinafuatiwa na kitenzi kingine ambacho hakibadili kiambishi awali cha nafsi (subject prefix), basi inabidi kitenzi cha pili kibaki katika uhalisia wake (infinitive).
Mfano:
Ninapenda kusoma blogu.
Siyo sahihi kusema:
Ninapenda soma blogu.
Lakini kwenye sentensi yangu ya kwanza pale juu ni sahihi kwa sababu:
... siku zijazo tafadhali badilisha ...
Kitenzi "zijazo" kinabeba kiambishi awali cha nafsi ya nomino "siku" ambacho ni "zi" wakati kitenzi cha pili "badilisha" hakina muundo unaoanza na "ku" wala kiambishi nafsi kwa kuwa chenyewe kiko katika mfumo wa "amri" (imperative)inayopoozwa na neno tafadhali.
Aidha, haiwezekani kusema"kubadilisha" kwa kuwa hiki kitenzi kinamhusu mhusika anayepewa ujumbe, na siyo nomino "siku".
Kitenzi cha pili kingeweza kuwa "ubadilishe" iwapo ningetaka kutumia amri ya upole moja kwa moja (kama ilivyo kwenye subjunctive), lakini si lazima.
Nimeahidi mahali fulani kwamba nitakuwa natoa masomo ya namna hii kila linapotokea kosa na nikaliona ili kuiepusha nchi yetu na tatizo kama tulilonalo kwenye Kiingereza. Tutakuwa taifa la ajabu mno. Sidhani kama tuna sababu ya kuwa na Kiswahili kibovu kama Wakenya.
Msomaji atakayehitaji msaada zaidi, aniandikie:
Mobhare Matinyi,
matinyi@hotmail.com.
bendera ya Marekani iko juu chini (up side down). I hope this is not in TZ!...
ReplyDeleteNdugu AF.
Bendera ya US imegeuzwa, chini juu.
ReplyDeletenimegundua kuwa, mlingoti wa kwanza hauna bendera ni hayo tu!
ReplyDeleteMi nimegundua kuwa kulikuwa na upepo mkali sana.
ReplyDeleteMdau Norway.
BENDERA YA IVORYCOAST IKO NUSU MLINGOTI TEH TEH TEH.
ReplyDeleteMNH JAMANI TUKUMBUKE HILO LA KUGEUZA UPSIDE DOWN BENDERA ZA WATU LILIMGHARIMU MZEE OBAMA MWAKA JANA KWA KUWAALIKA MARAISI KTK MKUTANO FULANI HUKO USA NA KWA BAHATI MBAYA AU KUTOKUJUA BENDERA YA UFILIPINO IKAWEKWA UPSIDE DOWN,YULE SIJUI ALIKUWA RAISI AU MUWAKILISHI WAKE ALIMUAMBIA OBAMA KUFANYA HIVYO TAFSIRI YAKE KWA HUKO KWAO NI KWAMBA NCHI IPO VITANI,ILIBIDI OBAMA AOMBE RADHI HADHARANI KWA KOSA HILO,SASA HAPA KWETU SIJUI WENYE BENDERA WATASEMAJE KUHUSU HILO ILA WAMAREKANI NAFIKIRI HAWAMAINDI SANA ILA KWA ANGALIZO TU TUWE MAKINI KWANI KUNA MATAIFA MENGINE NI WAKOROFI HATA KWA KOSA DOGO INGAWA LINAWEZA KUWA KUBWA JK ANAWEZA KUAMBIWA AOMBE RADHI
ReplyDeletewewe MOBHARE MATINYI kachunge ng'ombe achana na kiswahili cha kwenye blogu,au kama unajua kiswahili nenda mashuleni na vyuoni kafundishe hapa si mahali pa kufundishana lugha unless mtu aombe msaada huo
ReplyDeletekuna milingoti sita.miwili haina bendera.
ReplyDeletebendera ya marekani ip upside down.kuna upepo unaoelekea upande tofauti na uelekeo wa bendera.hivyo bendera zinapepea uelekeo tofauti na uliotarajiwa.
USA and Bongo Flags are upside down
ReplyDeletePicha imewekwa kinyume ingekuwa enzi zile za picha za mikanda (film cameras) tungesema umegeuza 'negative' wakati wa kusafisha!
ReplyDelete1. Upepo mkali umezielekeza bendera upande mwingine.
ReplyDelete2. Bendera za Tz na USA zimekosewa.
3. Aliyepandisha bendera ni mfanyakazi wa EAC therefore ni mkenya, ndo maana kapatia ya kenya na ya EAC na kaziweka juu-chini za TZ na USA.
4. Wabongo wengi hatuna la kufanya ndo maana tunapoteza muda kuchambua yasiyo na msingi, na yale yenye msingi hatujacomment kabisa (tazama idadi ya comments kwenye articles zingine za blog hii)
5. Sijui nafanya nini hapa...
Mlingoti wa kwanza una bendera ya Ivory cost lakini haikonekani ktk hii picha kwa sababu inapepea nusu mlingoti tokana na kipigo toka kwa zambia afcon 2012.
ReplyDeleteNyie mnaosema bendera ya tz iko juu chini mmeiona wapi? mbona mnapenda kuikandia inchi yetu? Ya usa ndio imegeuzwa.
ReplyDeleteBendera ya Marekani kichwa chini miguu juu!
ReplyDeleteMichuzi
ReplyDeleteNajua una tabia za kunitia kapuni, na pia naona nimechelewa kidogo kuweka maoni yangu kwenye habari hizi za bendera ya mericani.Kuna jamaa wamesema kuwa ni funny.Wajulishe wadau inawezekana kuwa bendera hapo juu ilikuwa upside down by mistake. Lakini bendera yako kuwa upside down ni namna ya SOS, yaani kuomba msaada kwenye matatizo makubwa."It signify dire distress...extreme danger to life" Flag code.