Waziri wa Nishati na Madini Mh. W.M. Ngeleja ambaye pia Mbunge wa jimbo la Sengerema akimkabidhi mkataba wa baraza la wafanyakazi mwenyekiti wa baraza Prof. A.H. Mruma ambaye ni Mtendaji Mkuu wa GST.
Wajumbe wa baraza wakimsikiliza mgeni rasmi hayupo pichani juu ya umuhimu wa baraza la wafanyakazi mahali pa kazi.
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi GST wakiwa katika picha ya pamoja , hafla ya uzinduzi ilifanyika katika ukumbi wa St.Gaper nje kidogo ya mji wa Dodoma Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) yazindua rasmi Baraza la wafanyakazi , tarehe 19 /02 /2012 imekuwa siku ya kihistoria baada ya chama cha wafanyakazi wa Serikali kuu na afya Tanzania ( TUGHE) tawi la GST kwa kushirikiana na tume ya Usuluhishi na uamuzi (CMA) kanda ya Dodoma wafanikisha uzinduzi wa baraza la wafanayakazi.
Kwa mujibu wa CMA historia ya chimbuko la ushirikishwaji wa wafanyakazi hapa nchini limetokana na Agizo la Rais Namba 1 la mwaka 1970 ambalo linaagiza kwamba , mahali popote pa kazi penye wafanyakazi wapatao kumi au zaidi na ambao ni wakudumu basi mahali hapo panatakiwa paundwe chombo cha kuwashirikisha wafanyakazi
Hongereni sana..Nimeangalia sana hiyo picha tofauti na waziri,niliyemfahamu ni mwalimu wangu tu Prof.Mruma wengine wote siwafahamu:
ReplyDeleteSisi ma-geologists ambao tunafanya kazi nje ya nchi mnatuweka pembeni sana na tuko wengi kiasi chake.Sisi kwa sisi tunaofanya kazi ya nje tunafahamiana sana..Ila hatufahamiani na hao wenzetu walioko Tanzania.Tunahitaji kufahamiana nao please.Prof. nikija likizo nitakutafuta nina namba yako ya simu tuweze kubadilishana mawazo mkuu au waweza kunicheki hapa atyini@yahoo.com