Mkuu wa Polisi Jamii wa Kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha,Issaya Doya akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa VodacomTanzania Mwamvita Makamba, wakati wa sherehe ya kakabidhi rasmi kituo hicho kilichakarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Foundation kwa thamani ya shilingi Milioni 17,tangu kijengwe mwaka 1967.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC) Thobiasi Andengenye akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,wakati wa hafla ya kukabidhiwa kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha , kilichokarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Tanzania kwa thamani ya Shilingi Milioni 17 tangia kijengwe mwaka 1967.katikati ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Karatu ( OCD ) Mathias Nyange.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo cha Polisi Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangia kijengwe mwaka 1967,kwa gharama ya shilingi milioni 17.Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye na kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya kaskazin Nguvu Kamando.
Ni vizuri kuonyesha makampuni kwa kiasi yanavochangia katika social responsibility ila sioni mantiki kuandika hyo milioni 17 katika kila picha ujumbe ni kuonyesha hela iliyotumika au ukarabati wa kituo? ni maoni yangu tuuu I stand to be corrected always
ReplyDeleteINAFURAHISHA KWA KITENDO HICHO KWANI NI MOJA YA SERA ZA POLISI KATIKA JAMII TUNAOMBA WADAU WANGINE WA POLISI KUENDELEA KUCHANGIA VITENDEA KAZI VYA KITUO HICHO MUHIMU KATIKA SEKTA YA UTALI
ReplyDelete