Kocha wa timu ya Zamalek ya Misri, Hassan Shehata (kushoto) akiwapa wachezaji wake mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo jioni.Timu hizo kesho zitaumana kwenye Uwanja wa Taifa katika mechi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambako zitarudiana baada ya wiki mbili huko Cairo Misri.Picha na Francis Dande

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kesho yanga lazima wakalie hawana nyimbo

    ReplyDelete
  2. mimi nina wasi wasi na aliyepost hizi picha kuwa ni mmisri. nawashauri yanga wasiogope majina wala mapost kama haya, dk ni 90 zile zile, wachezaji ni 11 wale wale, uwanja ni mmoja, lakini yanga wanawazidi hawa kitu kimoja, mashabiki walio wengi ni wetu.
    jikamateni kiume na mtupe raha watanzania kwa kuwafunga hao imalaseko walau kagoli kamoja.

    shabiki wa simba-mzalendo

    ReplyDelete
  3. umenena hafu baada ya hapo stoey nyiiingi za kipuuzi!

    ReplyDelete
  4. Huyo mwenye rasi atakuwa anatoka Afrika ya Magharibi nadhani.Mara nyingi hawa waarabu wanachukua washambuliaji kutoka nje.Kila la kheri Yanga

    David V

    ReplyDelete
  5. kila la heri yanga tunawatakia, simba wekeni upinzani wa jadi pembeni kumbukeni ni Taifa moja.. kumbukeni kushangilia kwetu ndipo kutawapa motisha hawa vijana wa Jangwani.....

    Mdau Simba

    ReplyDelete
  6. Wanafungika hao lakini kwa maandalizi ya uhakika na siyo kwa ushirikina.

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...