Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi akimpa zawadi ya Kitenge, Waziri wa Serikali za Mitaa kutoka Rwanda Mhe. James Musoni ikiwa ni zawadi maalum kwa ajili ya mkewe. Katika ziara hiyo Waziri huyo wa Rwanda aliambatana na Gavana wa Jimbo la Mashariki Bibi Odette Uwamariya. Cheo cha Gavana nchini Rwanda ni sawa na cheo cha Mkuu wa Mkoa nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika akimkaribisha Waziri wa Serikali za Mitaa wa Rwanda Mhe. James Musoni na ujumbe wake kutembelea maeneo mbalimbali yaliyo chini ya Ofisi hiyo mjini Dodoma jana.
Mhe.Mkuchika akipokea zawadi kutoka kwa Mgeni wake Waziri wa Serikali za Mitaa wa Rwanda Mhe. James Musoni. Viongozi hao na ujumbe wao pia walipata fursa ya kutembelea Chuo cha Serikali cha Serikali za Mitaa cha Hombolo kilichopo Dodoma ambapo Mhe. Musoni aliahidi kuanza kuleta watumishi wa Serikali za Mitaa kutoka Rwanda kuja kujifunza elimu hiyo katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma.
Mkuu wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Casmir Rubagumya (kushoto) akimpa ufafanuzi Waziri wa Serikali za Mitaa wa Rwanda Mhe.James Musoni wakati Waziri huyo alipotembelea Chuo Kikuu cha Dodoma jana.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kumpokea Mh. Musoni ambaye alitembelea Ofisi hiyo jana. Mbali na TAMISEMI, Waziri wa Rwanda alipata fursa ya kutembelea Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Chuo Kikuu cha Dodoma,LAPF na Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...