Kumekuwa na uhaba wa picha na habari kutoka vyama vya siasa, ukiondoa CHADEMA na CCM, kiasi hata inaonekana kuna kutoa kipaumbele kwa vyama hivyo tu. Hii bila shaka inasababishwa na changamoto za maofisa uhusiano/habari wa vyama vingine, ambao hawachangamkii ipaswavyo fursa hii isiyo gharama ya kutangaza vyama na shughuli zao. Yaani ukiona picha na habari za chama fulani zinashamiri humu ujue kuwa maafisa habari wake wanachangamkia fursa hii bila ajizi na si vinginevyo.

Globu ya Jamii inasimamia kwa dhati sera yake ya HATUBAGUI, HATUCHAGUI; ATAYETUZIKA HATUMJUI. Hivyo shime vyama vya siasa amkeni na mlete habari zenu zichapishwe bila malipo, sharti likiwa mradi usichafue hali ya hewa ama usijeruhi hisia za mtu/watu.

Lete habari zenu tuzichapishe  bila malipo kupitia
issamichuzi@gmail.com




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hata hivyo vyama vingine vyote vinatakiwa vijiondoe kwani tunahitaji vyama viwili tu kwani ndo vinaonekana vina nguvu. Vyama vingine ni miyeyusho tu vinapoteza muda wa wananchi. Tunahitaji vyama vikuu kama vile Democratic na Republican! Vyama vingine nchini vijiunge na CCM au CDM itategemeana na mapenzi ya mtu.

    ReplyDelete
  2. Ankal Habari kupokea hambagui sio?,

    Lakini Maoni mnaweka mengi kapuni hasa yaliyokuwa dhidi ya Chama fulani,,,,

    ''NO ONE IS PERFECT EXCEPT GOD''

    ZINGATIA YA KUWA JINSI CHAMA CHAKO KINAVYOKOSOLEWA NDIVYO CHAMA KINAVYO JIREKEBISHA NA KUIMARIKA ZAIDI!,,,UNAPOVAA SHATI HALAFU UKOSI UKAPINDA KISOGONI HUWEZI KUONA HATA KAMA UTATUMIA KIOO LAKINI MWENZIO NDIO ATAONA NA KUREKEBISHA! AU SIYO?,,,
    (NA HII WEKA KAPUNI PIA).

    ReplyDelete
  3. Mficha Maradhi Umauti humuumbua!

    Habari za Vyama vingine vya Siasa mnatumiwa sana tu, 'kutokana na sababu zenu' lakini mnachofanya ni kuwa mnaziweka KAPUNI!

    ReplyDelete
  4. mawasiliano je, Mbona

    ReplyDelete
  5. Kuhusu Habari Mjomba sawa!,

    Hii blogu inaaminika na kukubalika sana kama Social Platform,

    Sasa basi nia ni kujenga na sio kubomoa kwa vile mtu akichanwa huku inakuwa ndio nafasi nzuri kwake kujirekebisha 'No one is perfect except God' !

    Tatizo Ankal ni kuwa baadhi ya watu wako unawakingia sana kifua tukiwa chana humu wewe unaweka kapuni.

    Ni afadhali uwe na utaratibu wa kum fowardia msg Muhusika ili ajue watu wanamchana vipi na ajirekebishe kuliko kuweka kapuni na kufuga maradhi na ubovu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...