Katika siku za karibuni kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa maadili kupitia maonyesho ya majukwaani na kazi mbalimbali za Sanaa.

Kutokana na hali hii, Baraza la Sanaa la Taifa kupitia programu ya Jukwaa la Sanaa Jumatatu ya Tarehe 26/03/2012 litakuwa na mada maalum ya Unenguaji na Maleba Katika Muziki.

Mada hii itakayowasilishwa na Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) na asasi ya Sanaa ya Binti Leo pamoja na mambo mengine itaangalia hali halisi ya Sanaa ya unenguaji, maleba na matatizo yaliyopo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

BASATA inatoa wito kwa wadau wote wa Sanaa na wapenzi wa Utamaduni wan nchi yetu kujitokeza kwa wingi siku hiyo kushiriki kuchangia mwelekeo mpya wenye maadili sahihi ya kitanzania.

Sanaa ni Kazi Kwa Pamoja Tuikuze na Kuithamini.
Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI, BASATA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Unajua jambo lolote likizidi kiwango inakuwa kero badala ya starehe, ukikaa katika Luninga wakati mwingine unaona aibu akiweko mkweo, wanao, na watu unaowaheshimu nguo zinazovalia katika sanaa hasa kwa akina dada zetu wazungu wanaita "leaves much to be desired". Wamama tunajidhalilisha sisi wenyewe.

    ReplyDelete
  2. Uncle hongera kwa kazi ya kutupasha katika hili naunga mkono watu wa BASATA katika hili. Ni vyema tufike mahali tuweze kuwa na control ya uhuru tulionao, ingawa wapo wanaobisha kusema kweli mavazi na mitindo ya unenguaji imekuwa chanzo cha matatizo makubwa ya kimaadili hasa uzinifu na ngono za mapema kwa vijana.

    ReplyDelete
  3. at last jamani mi nilidhani wanapiga marufuku kumbe ndio kwanza wanaaza mjadala? wapi maadili ya mwanamke wa kitanzania? wapi tunakwenda jamani ndio maisha magumu lkn this is too much! mwanamke mwenzio anacheza wewe unatamani litokee shimo uingie!!! mambo hayo ni ya ndani jamani hizi ngoma zilikuwepo tangu hapo awali lkn nakumbuka iliitwa ngoma ya ndani tena mpiga ngoma alikuwa mmoja tu mwanaume tena na yeye kwa sasa najiuliza alikuwa mzima kweli, na ilikuwa strictly ladies na hata ikitokea mtu anachungulia dirishani basi ngoma huzimwa. sasa leo hii jukwaani!!!? tena niliwahi kusikia kwenye redio eti mangazaji anamsifia mnenguaji kwa ujuzi wa kuzugnusha tako moja lol. sidhani kama kuna haja ya mjadala ni kupig amarufuku tu. wakafanye kwenye indoor halls au bar wakibakwa shauri yao.

    ReplyDelete
  4. Tangazo halijaeleza sehemu/mahali ambapo hiyo shughuli itafanyikia wala muda.

    ReplyDelete
  5. Naomba nieleweshwe majukumu ya Basata, binafsi nilifikiri kazi yao ni kutoa adhabu kwa wahusika pale wanapobaini kuna watu wanafanya mambo yanayopingana na sheria yao.Km ni ivyo basi, mkutano huu ni wann au hawana kupata hakika kama hao jamaa wanavunja sheria

    ReplyDelete
  6. Na nyie pia mmkekiuka maadili. Mbona nembo hiyo siyo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Mnapotumia nembo yenu tumieni kichwa chenu pia. Simply use: Baraza la Sanaa Tanzania. Don't use "United Republic of Tanzania" while your court-of-arm is BASATA's. That's completely wrong.

    ReplyDelete
  7. Maonesho hayo hufanyika usiku na wanaoruhusiwa kuingia kwenye kumbi ni wale tu! Walio juu ya 18yrs hivyo sioni tatizo lolote anayekerwa asihudhurie coz hayafayiki hadharani!

    ReplyDelete
  8. Mmechelewa sana maana hao khanga moko na laki si pesa si zaidi ya chakacha na mayenu iliyopo long time!

    ReplyDelete
  9. Hawa BASATA wamekosa kazi. Walikuwa wapi siku zote bendi za Twanga, Akudo, FM Academia, Taarab na mipasho ya TOT na wengine na nyingine nyingi walipokuwa wanatoa maonesho yao?. Yaani leo hii Kanga moko laki si pesa ndiyo wameona waiwekee mjadala. Yaani wanaonea vidagaa ili kulinda watu fulani kumonopolise music.

    Mi namfagilia sana SHILOLE na Q-CHILLA kwenye wimbo huo, sijaona jipya ambalo halijafanywa na watu niliowataja hapo juu. Huu ni upuuzi sana, badala ya kulinda wasanii wanataka kulinda masilahi ya wachache. Kwenye hili BASATA wanajishushia legitimacy.

    ReplyDelete
  10. Afrika vipiiiiiii?????mbona nikitu cha kawaida, kuficha ficha mambo ndo maana umalaya hauishi ...

    ReplyDelete
  11. HONGERA BASATA:

    Tunashukuru sasa JIPI LIMEPASUKA, haiwezekani jamii inayojiheshimu na yenye Utamaduni na Maadili kama yetu ya Tanzania ikawa ni jamii ya kukata viuono na kukaa nusu uchi hovyo!

    Sawa, hata kama Wadau wanasema ''Maonyesho hufanyika ktk Kumbi maalum mida ya Usiku na ni kwa walio na umri wa zaidi ya miaka 18'' KINACHO TILIWA MKAZO NA BASATA NI KUWA BADO MAADILI HAYAJAZINGATIWA KWA KURUHUSU URUSHAJI WA HABARI NA TAARIFA HIZI ZA 'NYUMA YA PAZIA' KUWA HEWANI KTK VYOMBO VYA HABARI VYA JAMII NZIMA WAKIWEMO WALIO CHINI YA MIAKA 18 NA TUNAOHESHIMIANA NAO, WANAPATA 'LIVE BILA CHENGA' KUPITIA VYANZO BILA UDHIBITI KAMA VYOMBO VYOTE VYA HABARI, MAGAZETI NA TELEVISHENI!

    ReplyDelete
  12. BASATAaaaaaa......! mmekerwa au mnataka kukolezea mambo? Wenyekazi ya kudhibiti hayo wapo na uwezo wanao lakini wametulia kimya wanapata RAHA zao katika kanga moja.... Nyie naona mwataka posho si semeni tu....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...