Pamoja na Kwamba kuna kibao kinachohamasisha usafi katika eneo hilo,lakini ndio kwanza uchafu umejaa kana kwamba hicho kibao kimewekwa kwa utembo tu.
Kama haitoshi na hapa pia kuna kibao kingine tena uzuri wake hiki kimeantikwa lugha yetu ya kimatumbi,lakini bado mwendo ni ule ule.kwakweli bado tuna safari ndefu sana ya kutaka kulifanya jiji letu kuwa safi.hapa ni Msasani njia panda ya kuelekea CCBRT.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Unapoandika usitupe takataka hapa inabidi uwape watu alternative watupe wapi? Vinginevyo hali hii itaendelea kushamiri.

    ReplyDelete
  2. Mkuu,
    Hiyo ndo TZ aka Bongo. Miaka ya tisini mwishoni UN walilisaidia jiji kwa kuanzisha idara ya Waste Management. Na walifanya kazi wale mabwana kwani walikuwa watu na fani zao. Jiji lilikuwa safi na baadhi ya majiji ya Afrika walifika Bongo ku-learn. Baada ya madiwani kurudi tena baada ya tume ya jiji, wakaiua ile deparment eti iwe chini ya mganga wa wilaya!!!! Na wale wataalam wa mazingira wakaondoka na matokeo yake ndo hayo!!! Bongo tambarareeeeee....

    ReplyDelete
  3. Ankali kweli hali sio shuari,namuunga mkono mchangiaji namba mbili. Nilibahatika kufanya kazi multinet afrika ltd mawakala wa uzoaji taka enzi hizo za miaka ya tisini.
    Ukweli kuna bylaw nyingi za mipango miji ambazo watu wanatakiwa wachangie garama za ukusanyaji wa takaka lakini Kama sheria zipo lakini hazifuatiliwi,na pia hakuna utaratibu ulio wazi ambao unafahamika kutoka local government,au serikali ya mtaa lazma kunakua na madhara Kama hayo ya uchafu unao zagaa.

    Mfano nchi zilizo endelea wanautaratibu wa ukusanyaji taka ngumu. Labda kila juma nne na ijumaa ni siku ya kuzoa ucha wa kawaida. Na siku ya J tano ni siku ya kuchukua uchafu Kama chupa,boxi (recycling)sasa yote yanawezekana. Sio kwamba sisi tunazalisha taka zaidi hapana. Ni utaratibu tuu na ufuatiaji wa kutekeleza sheria sio tuu zibakie vitabuni,au kuwekewa bango. (pendezesha jiji lako)

    remember your junk is someone else treasure.

    Mdau Washington.

    ReplyDelete
  4. Huu ndio ufahamu wa watupa taka eneo hili

    Keep our city dirty.
    Sio marufuku kutupa taka eneo hili Ruhusa serikali ya mtaa

    ReplyDelete
  5. Kwanza: Usafi unatoka ndani ya mtu mwenyewe kabla ya sheria. Ina maana unapofanya usafi kwenye nyumba yako kuna mtu anakupangia?
    PIli: hivi hii hali inawakera wana mtaa? kama inawakera wenyewe kama mtaa wamechukua jukumu gani? maana maeneo mangine wana mtaa wanachanga hela wanawalipa vijana then wao wanazoa au wanalipia gari then gari inapeleka inakotakiwa.
    Tatu: swala la usafi inabidi lipewe kipaumbele na jamii husika halafu serikali itowe incentives kwa ajili ya kukamilisha usafi. lakini kama usafi mnakimbizana na kufukuzana kama mnafukuza wezi lazima tu mazingira yatakuwa machafu. Kama ilivyo police jamii na ulinzi shirikishi pia ni muda muafaka kwa wakazi wa Dar waanze ulinzi shirikishi kwenue maswala ya Usafi maana ni aibu jiji linanuka chafu wakati serikali na wizara na viongozi wote wako hapo.
    Nnne na Mwisho viongozi na wote waliopo Dar na wao waone kama ni tatizo maana wageni wote wa nchi hii wanaanzia Dar, tunatoa taswira gani kwa dunia? kama unakaaakwenye gari ya kiyoyozi , nyumba ya kiyoyozi lakini unapita pachafu penye harufu halafu huchukui hatua yoyote kama kiongozi tukuweke kwenye kundi gani?
    mi nafikiri Usafi wa jiji la dar its high time hata rais aingilie kati kama walioko chini yake wameshindwa kazi. Elimu duni, afy mbaya, ugumu wa maisha hata takataka jamni? We need to think loud and critically on this!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...