Basi la Abiria la kampuni ya Super Najmunisa lifanyalo safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza,likimalizikia kuteketea kwa moto mara baada ya kupata shoti ya betri.ajali hiyo imetokea jioni ya leo maeneo ya Berege Mkoani Morogoro wakati basi hilo likiwa njiani kuelekea jijini Dar es Salaam kutokea Mwanza.hakuna mtu yeyote aliedhulika kwenye ajali hiyo isipokuwa mizigo yote ya abiria hao iliteketea kwa moto.
Basi hilo nikiendelea kuwaka moto.
Sehemu ya Abiria wa Basi hilo pamoja na wamazi wa maeneo ya jirani na kijiji hicho wakiwa wamekaa pembeni kuangalia jinsi gari hilo linavyoteketea kwa moto bila ya wao kujua la kufanya wakati huo.
Poleni sana abiria kwa tatizo hili kubwa lililowapata.
ReplyDeleteWENYE MABASI LAZIMA MUWALIPE INSURANCE HAWA ABIRIA.
Ni kitu cha kushangaza, bado najiuliza je ?? hili bus lilikuwa na chupa za unga wa kuzimia moto ?? (fire extinguishers) au ni kukatisha ticketi tu za abiria na kuangalia nani ana samaki sato alipie box lake !! maana haiwezekani mpaka bus zima likateketea mpaka abilia washindwe hata kuokoa mizigo yao ndani ya buti, bus halikulipuka kama bomu au je ndani ya buti kulikuwemo na mitungi ya gesi ?? au mafuta ya aina yoyote ile ? kama ni shoti ya betri ,moto umeanza taratibu kwanza kwa kutoa harufu-je hio muda haukutosha buti kufunguliwa na watu kutoa mizigo yao ? i dont get it, we cant be that slow thinking. Nene okungwa Magese.
ReplyDeleteokungwa Magesa, uhai wa watu ni muhimu sana kuliko hiyo mizigo iliyoungua, na siku zote tunaaswa ajali ya moto inapotokea tukimbie mbali,abiria wangetaka mizigo yao hakika lazima kungekuwa na majeruhi hata vifo kabisa, kikubwa ni wenye mabasi kujali zaidi service za magari yao kila mara na hasa haya ya njia ndefu.
ReplyDeletemimi
okungwa magese, kama moto umeanzia chumba cha betry ni kwamba moto umeanzia chini na ni karibu na katika ya basi kwa hiyo ni vigumu kuona, ni vigumu kupata harufu mapema kwasababu gari inakwenda mbele tena kwa kasi, hivyo harufu inapulizwa na upepo kwenda nyuma. mpaka kupata harufu ni baada ya moto kuwa mkubwa ua gari lisimame, moto utaenea haraka kwa kuwa unachochewa na upepo. fire extinguisher bottle zilizomo kwenye mabasi ni ndogo kupambana na moto ulioshamili ila inaweza kuzima moto unaoanza hasa ikipata mtumiaji mzuri. baada ya kukueleza hayo nadhani itakuwa rahisi kwako kujua ni nani slow thinker.
ReplyDeletepengine basi limekingwa na bima kubwa, likiungua lote anafidiwa jingine, likiunguwa nusa anafidiwa nusu halafu akaanze kuhangaikia matengenezo, nani anataka hilo?
cha maana tumshukuru mungu hakuna abiria aliye dhurika. LABDA TUWAULIZA MAAFISA WA FIRE IMEKUWAJE 'STIKA YA FIRE' IMESHINDWA KUZIMA MOTO?? WAKATI MWENYE BASI KALIPIA STIKA??
Biashara za kichawi .hayo ni makafara.
ReplyDelete