Sehemu ya choo kinachotumiwa na kituo hicho cha Kulelea watoto yatima cha Mkoani Arusha cha Faraja
Mwanzilishi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Mkoani Arusha cha Faraja Bw. Faraja Maliaki (aliyebeba mtoto) akiwa katika mmoja wa bweni ambalo pia linatumika kama darasa wakati wa likizo wakati watoto hao wakiwa mapumziko ya masomo akiwaeleza jana mjini Arusha wanakamati wa Kimataifa wa maandalizi wa Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) juu ya changamoto mbalimbali zinazokabili kituo hicho wakati wajumbe hao walipotembelea kuangalia sehemu itakayokarabati ikiwa ni mchango wa AfDB. Mkutano huo utafinyika mwishoni mwa Mwezi Mei hadi mwanzoni mwa Juni Mwaka huu mkoani Arusha.
Baadhi Wanakamati wa Kimataifa wa maandalizi wa Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wakibadishana mawazo na Mwanzilishi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Mkoani Arusha cha Faraja Bw. Faraja Maliaki jana mjini Arusha juu ya changamoto mbalimbali anazokutana nazo katika kuwasaidia watoto walioko katika kituo chake wajumbe hao walipotembelea kuangalia sehemu itakayokarabati ikiwa ni mchango wa AfDB. Mkutano huo utafinyika mwishoni mwa Mwezi Mei hadi mwanzoni mwa Juni Mwaka huu mkoani Arusha.
Baadhi Wanakamati wa Kimataifa wa maandalizi wa Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wakijadiliana juu ya mchango wa AfDB wa Dola za Kimarekani utakavyosaidia kuchangia kupunguza changamoto mbalimbali zinazokabili kituo cha kulelea watoto yatima cha Faraja ingawala fedha zaidi bado zinahitaji ili kuboresha maisha ya watoto wanaoishi katika kituo hicho . Mjadala huu ulifanyika jana mjini wakati wajumbe hao walipotembelea kuangalia sehemu itakayokarabati ikiwa ni mchango wa AfDB. Mkutano huo utafinyika mwishoni mwa Mwezi Mei hadi mwanzoni mwa Juni Mwaka huu mkoani Arusha.
Mwanzilishi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Mkoani Arusha cha Faraja Bw. Faraja Maliaki (kulia) akiwaeleza jana(leo) mjini Arusha baadhi ya wanakamati wa Kimataifa wa maandalizi wa Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) juu ya changamoto mbalimbali zinazokabili kituo hicho wakati wajumbe hao walipotembelea kuangalia sehemu itakayokarabati ikiwa ni mchango wa AfDB. Mkutano huo utafinyika mwishoni mwa Mwezi Mei hadi mwanzoni mwa Juni Mwaka huu mkoani Arusha.
Msaada Mkubwa sana uelekezwe kumuunga Mkono Ndg. Faraja Malieki kwa harakati zake hapo Arusha.
ReplyDeleteNi wakati sasa tuangalie mfano Fisadi nyingi zimejiri kwa watu wenye asili ya Arusha lakini ukiangalia hali ya Ustawi wa Jamii inayowazunguka huko kwao ni 'Mzungu wa Nne' ukilinganisha na Mabilioni yaliyowekwa mikononi.
Hebu angalia choo wanachotumia hawa watoto kujisaidia, milango ya manailoni yaliyo chanika chanika!
Hivi kweli hawa Matajiri wa Mabilioni hawajapaona hapo kituo cha Faraja?,,,hivi kweli huwa hawa Mabilionea Wanasali kwa ya kweli Ibada?
Kaisari anaombwa na anatoa bila faida mbele, je hawa waliofanikiwa kifedha wamemrudishia nini Kaisari ????