Jana jumapili ya tarehe 18/03/2012 kwenye viwanja vya KIITEC kulikuwa na muendelezo wa Bonanza la kila jumapili KITAMBI NOMA BONANZA kulikuwa na michuano ya soka pamoja na uvutaji wa kambi (Tag of War) ambapo matokeo kwa upande wa soka yalikuwa kama ifuatavyo:

KITAMBI NOMA 5 - 1 ARUSHA STARS (Nyota wa mchezo - Ramadhani Kabadi)
KITAMBI NOMA 3 - 2 ACCESS FC (Nyota wa mchezo - Sam Msukuma)
ARUSHA STARS 2 - 4 ACCESS FC (Nyota wa mchezo - Mike Access)

Na kwa upande wa mashindano ya kuvuta kamba timu ya wanawake ya KITAMBI NOMA QUEENS iliibuka washindi kwa kuivuta timu ya wanawake ya ARUSHA STARS mara nne katika raundi tano dhidi ya raundi moja ya Arusha Stars.

Mbali na michezo hiyo kuchukua nafasi pia kulikuwapo upinzani mkubwa wa kutoa burudani baina ya ACCESS FC na KITAMBI NOMA ktk viunga vya QX PUB, huku ACCESS FC wakichukua point 3 tatu muhimu baina ya kutoa burudani ya kufa mtu pale QX PUB ikiwaacha wanaKITAMBI NOMA CLUB wasiamini kilichotokea kilabuni kwao.

Kufuatia kushindwa kutoa burudani, Mwenyekiti Nd. Chalz Makwaia wa KITAMBI NOMA alijitetea kuwa vijana wake siku ya jana walikuwa katika mchakato mzito wa kupata ripoti ya mapato na matumizi ya kilabu hivyo wakashindwa kutoa 'kwachu-kwachu' kama kawaida yao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hao kitambi noma mbona sura zote za DAR....PJ wa clouds huyo mwenye jeans na tai sio chata la kinondoni hilo?...mmmh

    ReplyDelete
  2. Hahaha! MUGISHA habari za bongo? mzee wa kitambi noma upo Arusha?

    ReplyDelete
  3. Hivo vitambi mboni vikwapi?

    ReplyDelete
  4. Watoto wa ilala mmehamia umasaini?

    ReplyDelete
  5. Kweli arusha imevamiwa mzee wa abajalo kabadi kama sio yeye rudi sinza wewe!

    ReplyDelete
  6. PAUL JAMES UPO CLOUDS FM ARUSHA?

    ReplyDelete
  7. HIVI JEZI ZA YANGA, SIMBA, AZAM NI NGUMU KUZIPATA? MAANA HAPO NAONA WATU WAMEVAA JEZI ZA WENZETU WA KULE ENGLAND ANGALAU WANGEPATIKANA PIA NA WALIOVAA ZA TAIFA STAR

    MDAU IGWAMANONI

    ReplyDelete
  8. Hahaha! i like the brand name!

    ReplyDelete
  9. Kweli wadau hizi number za bongo!wana zuga tu hao!

    ReplyDelete
  10. Ankal hizi sura zote za ILALA FLAT, KINONDONI NA SINZA kazi kweli kweli wa meru wamevamiwa.....

    ReplyDelete
  11. tetetete! eti KITAMBI NOMA duu! mmekosa majina?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...