Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa kambi rasmi bungeni,Mh. Freeman Mbowe (wa pili kulia) akijadiliana jambo na Wadau wa chama hicho waliopo mjini Arumeru muda mfupi baada ya kuwasili eneo hilo tayari kwa uzinduzi wa Kampeni ya Ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki leo ambapo Mh. Mbowe atatumia fursa hiyo kulihutubia Taifa juu ya Mustakabali mzima wa nchi yetu.
Mgombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki (CHADEMA),Joshua Nassari akiwa na Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Arusha,Mh. Joyce Mukya (CHADEMA) wakitafakari mawili matatu kabla ya kuanza kwa uzinduzi wa kampeni leo.
Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Yohana Natse akiwasili kwenye uwanjani hapo tayari kwa uzinduzi wa kampeni za Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki leo.
Mkurugenzi wa ulinzi na usalalma taifa, Ndg. Wilfred Lwakatare akiweka mikakati sawa.
Mamaaaaaa!!!!, Mbunge mdogo sana huyu, na mawazo yake yatakuwa ya kikubwa kweli?
ReplyDeletePatachimbika
ReplyDeleteDavid V
chadema bado kuna wachache wana kauli katika chama. Hakijiendeshi kichama kitaifa, ndio sababu wana nguvu only baadhi ya sehemu za mikoa. Kwa mawazo yangu,wakifanye chama cha kitaifa ili kushindana na CCM. Naamini wanaweza kukitoa iwapo watafanya mabadiliko.Wajumueshe watu wote wenye sifa katika nafasi za juu.
ReplyDeleteKwa taarifa tu CCM imechokwa kila mahali. Ni pesa chafu tu na vitisho vya polisi ndivyo vinafanya ionekane inakubalika baadhi ya sehemu.
ReplyDeleteAsante mdau hapo juu kutuarifu kuwa ccm imechokwa kila mahali, mumkini taarifa yako ni sahihi hasa ukizingatia sababu ulizoorodhesha. Ila kwangu ni vigumu kujenga hoja ni chama gani next. Nimeshachefuliwa na chadema even before they're there! Harakati zao za kitoto mno, na very outdated. Kukimbizana na polisi, kugomagoma, kususasusa, kuvunja sheria, uhalifu, orodha ni ndefu. Mustakbali wa tz ni dilemma, si kila mmoja ana upeo kuliona hilo. Cuf nao wanagawana mbao, ngalawa imekumbwa na dharuba. Ila kuna fact kwamba SI KILA kiongozi ndani ya ccm ni mbovu. Na si kila kiongozi wa upinzani ni mwadilifu. Kina Slaa wa chadema ni ushahidi wa nnachosema. Mndengereko, ukerewe
ReplyDelete