Msajili wa vyama vya Siasa Mh John Tendwa amekipatia usajili wa muda chama cha ADC. Pichani anaonekana Msajili akimkabidhi cheti hicho kaimu wa chama hicho  Bw.  Saidi Abdalla Miraji  ofisi ya msajili jijini dar es salaam leo.  Bw Miraji, aliyekuwa meneja  wa Kampeni za Urais wa CUF mwaka 2010,  na wenzake jana waliwasilisha rasmi kwa Msajili wa Vyama vya Siasa maombi ya usajili wa muda wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC). 
Juzi, Miraji na aliyekuwa mgombea ubunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF, Adawi Limbu walijitoa chama hicho na kutangaza kusudio la kusajili chama kipya. Jana, ujumbe wa chama hicho uliwasili katika Ofisi ya Msajili, Dar es Salaam saa 7:30 mchana ukiongozwa na Miraji ambaye alijitangaza kuwa ni Kaimu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wake, Bw Limbu.
 Viongozi wa muda wa ADC
 Viongozi wa muda wa ADC katika ofisi za msajili leo
 wafuasi wa chama hicho wakifurahia baada ya kupata cheti na bendera mkononi. Hata hivyo Msajili wa Vyama amesema ana fuatilia rangi ya bendera ya chama hicho ambayo ina fanana na CHADEMA na kwamba endepo CHADEMA  watalalamikia basi ADC kwavile wao ndio wana anza itabidi wabadili rangi ya bendera yao ili kuepuka usumbufu kwa wana chama wa vyama hivyo 

wafuasi wa chama hicho wakifurahia baada ya kupata cheti




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hivi nhivi vyama kila siku vinaanzishwa vialeta upinzani upi au kuongeza matumizi yasiyo na lazima kwa kuwa kitaposajiliwa chama kama hiki hakina uwezo wowote wa kupata nafasi ya uongozi zaidi ni kupokea ruzuku kwa manufaa yao na ndio maana wameondoka huko na kwenda anzisha ulaji wao.Lazima tufike mahali tuangalie uanzishwaji wa hivi vyama sio kila mtu kwa kuwa anahaki ya kufanya hivyo basi anafanya kuwa na vyama vingi visio na msimamo hakuleti upinzani wa kusaidia maendeleo ya nchi,sasa hao wameondoka cuf, kesho utasikia wengine tlp.

    ReplyDelete
  2. Ni vijiwe vya wachache tu kupata riziki bila kutaka kufanya kazi.

    ReplyDelete
  3. Selfishness...

    ReplyDelete
  4. Duuh kazi ipo hapa!

    ReplyDelete
  5. Hili la kuiga bendera za vyama vingine lishughulikiwe mapema

    ReplyDelete
  6. Hii nchi inabidi ipunguze vyama.
    Tena inabidi vianzishwe vyama vipya vitatu tu 3.
    Nchi inakuwa maskini kwa sababu ya maongezi mengi kuliko matendo.
    1.Vyenye mlengo wa CCM viungane na kuwa chama kimoja.
    2. Vyenye mlengo wa siasa mpya kama vile chadema cuf nakadhalika viungane na kuwa chama kimoja.
    3. Na kianzishwe chama chenye mlengo wa kuetetea mazingira ya Tanzania
    Vymam vya kidini vipigwe marufuku kwani dini haiendani na siasa .

    ReplyDelete
  7. Msajili hayuko makini,sioni kufanana kokote kwa bendera kimuundo. Rangi zilizotumika ni 3 ambazo ni sawa kwa vyama vyote yaani bluu, nyeupe na nyekundu, lakini bendera ya chadema ina alama ya V wakati ADC wana maandishi ya ADC. Msajili aangale bendera za Mali, Ghana, Guinea na Senegali zina rangi zilizokaribia kuwa sawa lakini miundo na alama zilizopo katika bendera hizo ni tofauti, hazisemwi kuwa zimefanana. Halikadhalika bendera za Tanzania, Jamaica na Afrika ya Kusini zina rangi zinazoshabihiana lakini hatusemi zimefanana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...