Assalam  Alaikum Kaka.
 kwa muda sasa vilio vya wazazi na waalimu vimekuwa vikisikika kuhusiana na tuhuma za vijana wa shule kujihusisha na matumizi ya vileo.mimi ni mwalimu katika shule moja mkoa wa kielimu Temeke,DSM.

Nimepigania kupinga  hili jambo la kukodisha wafanya biashara wa kuuza vileo katika shule yangu hadi nikaonekana ninaajenda yangu ya siri.Ukweli nakwamba ninaandika roho inaauma kuona baadhi ya waalimu hawana uchungu na maisha ya watoto amabao sisi tumepewa jukumu la kuwalea kwa kipindi cha miaka saba (7).

Baadhi ya waalimu wamekuwa wakifaidika na vijisenti vya upangishaji na mikataba ambayo mwisho wa siku inaharibu mwelekeo wa watoo wetu.

Hebu UNCLE wewe na timu yako kwa muda wenu njoo hapa shuleni  (kurasini primary karibu na UHAMIAJI HQ) uone duka la vilevi tena vikali waliyopewa dhamana ya kuharibu wanafunzi na uongozi wa shule.
naomba ufiche jina langu 
nisiharibu salary slip yangu.asante
Ticha 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Duh pole mwalimu, wewe kweli ni mzalendo na uchungu na profession yako.

    Lakini mwalimu mkuu na kamati ya shule ndiyo wa kulaumiwa hapo. Inawezekana vipi kuruhusu kitu cha aina hiyo halafu tunasema kwa kutoka kipovu mdomoni eti watoto wa siku hizi hawana adabu?

    Mimi nilidhania maduka ya shule ni kwa ajili ya vitu kama stationery au hata vyakula vidogo vidogo kwa ajili ya wanafunzi.

    Lakini vinywaji vikali, mmmmmmmmh tunapotea hapo.

    ReplyDelete
  2. Hata ughaibuni hairuhusiwi kuwa na bar ndani ya shule. Kununua sigara mpaka uonyeshe ID ili watu wajue umri wako kama uruhusiwe kuuziwa sigara au hapana. DUH shule ya msingi ina bar?

    ReplyDelete
  3. walimu ni miongoni mwa watu wenye kuonyesha maadili sasa wanaporuhu haya jamii yetu ina walakini

    ReplyDelete
  4. FEDHA sio BORA kuliko MALEZI BORA!

    Uongozi wa Shule inabidi walielewe hili na kama wao wananufaika sisi tutakwenda mbele ya sheria zaidi kwa sababu hatuwezi kabisa kuruhusu 'upuuzi huu' wa aina hii ya Malezi kwa Jamii ya Watoto wa Tanzania!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...