Hi Issa, Heshima yako.
Sijui kama blog yako inaweza kutuma swali langu la mila, utamaduni wetu wa Tanzania(Afrika) kuhusiana na mambo ya ndoa, mume na mke na yote yanayahusika. Swali ni hili:
 
Hivi, sisi waTZ(Afrika) tunatumia lugha/vitendo (gesture) gani katika ndoa zetu?  Kwa vitendo nina maanisha kila kitu tunachofanya kabla ya "kitendo cha ndoa" - Tafadhali, hili swali sio kuhusu "kitendo cha ndoa" na ninaomba kama uta-post swali langu, watakaojibu wajibu kama wanajua wanachozungumzia kutokana na mila zao au walizosikia. Maneno ya nguoni na kukoseana heshima sio dhumuni la swali hili.  Naomba majibu yawe ya kisomi, heshima na yenye nia ya kufundisha wale wote kama mimi wasiojua mila na desturi za "ndoa" za waTZ(Afrika).
 
Hili swali limeletwa na kujiuliza kwa siku nyingi kwa nini tunafanya wanayoyafanya watu wa Ulaya/Wazungu kama vile kushikana mikono, ku-kiss midomoni etc.  Je kiutamaduni waTZ(Afrika) hayo mambo yapo?  Na kama hayapo, ya kwetu ni yapi?
Sioni watu wazima/wazazi wetu wakishikana mikono au kupitishiana mikono kiunoni wakitembea au kusimama pamoja, kusalimiana kwa a peck on the lips.  Vijana ndio wanafanya hizo PDA (public display of affection).
 
Nitaelewa kama blog yako sio ya maswali kama haya, ila nilikuwa nina hamu ya kujua kidogo zaidi kuhusu mila zetu kwenye ndoa/relationships na sikujua mahali pengine pa kutuma hili swali.
 
Ukae salama,
Elle.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Asante kwa kuuliza swali lako. Mimi ni Mwanamke na nimtanzania. Mimi ninadhani ki mila zetu waAfrica/Tanzania kwa kweli mambo ya public affection hayapo. Lakini hivi sasa vijana wengi wanafanya PDA kutokana na culture nzima ya kiAfrika inabadilika kupitia Elimu na kusafiri kutoka nchi moja mpaka nyingine. Haya ni mambo tunayo jifunza na taratibu yanatubadilisha culture yetu. Kwa mfano mzuri tu zamani wazazi walikuwa wakitafutia watoto zao wachumba na ukichunguza ilikuwa either kabila moja au makabila yalio karibiana. Hivi sasa vijana wenyewe wanajichanganya na kujitafutia. Hili swali lako ni sehemu ndogo ya change in our lifestyle kama waTanzania.

    ReplyDelete
  2. Wewe una somo.

    ReplyDelete
  3. Wewe dada bila shaka umeshafikia au kupita umri wa mature, sijui unatoka kabila gani, lakini makabila mengi ya Tanzania yana desturi ya kufundisha unyago (kufunda), kama wewe hujafundishwa au kupitia unyago, haraka waulize wazee wa kabila lako ili ufundishwe hicho ulichouliza hapa mtandaoni.Ni aibu msichana wa Kitanzania kama hujui maana ya unyago.

    ReplyDelete
  4. kwa mila za ukweli kitanzania na za kiafrica there are no such things as public affection. hata makanisani tanzania akina baba wanakaa upande wao na akina mama wanakaa upande wao. mambo ya affection kwa mila zetu ni ya private, sasa dunia ya leo ndo inatuchanganya. na ukiona mwanaume anaonyesha affection kwa mwanamke in public basi ujue huyo mwanamke ni nyumba ndogo (yaani hawara) na si mkewe wa ndoa

    ReplyDelete
  5. wewe uliotakiwa utukanwe sana na ndiyo maana watu wengi ndani ya blogi yetu wamekupuuza, (a) hapo ulipo sasa hivi lazima una simu ya mkononi-jibu swali je babu zetu walikuwa na simu za kiganjani ?? yaani unataka tukuambie kwamba dunia inabadilika !!!! nenda zako huko and please think big NOT small. Zebedayo.

    ReplyDelete
  6. MIE NIMEPENDA MUULIZA SWALI KAULIZA KUHUSU UTAMADUNI NA MILA, SIKU HIZI KUKIJA MASWALI KUNA WATU HUJIBU KWA KASHFA KWENYE DINI ZA WENZAO UKICHUNGUZA SANA HUMU MICHUZI AU MTU HUTAFUTA KASHFA ILA HUYU KAULIZA KWA NIZAMU KITU NA WATU NATUMAI WATAMJIBU KWA NIZAMU, MIE NAONA ANGEKUWA KARIBU NA MILA AKAFANYA ILE MILA ANAYOTAKA NA MAADILI MAZURI KATAFUTE ELIMU HAPA WATAKUPOTEZA ITAKUWA SAWA NA USHAURI WA GAZETI TU.

    ReplyDelete
  7. mi nadhani kila zama na mambo yake.
    hivyo acha mawazo mgando.mapenzi ni sehemu ya maisha ya mwanadamu na yanasaidia kupunguza stress vile vile so inategemea sasa je,hayo mapenzi ni ndani ya ndoa au......kama ndani ya ndoa RUKSAAAAA kujisosomola weye na honey wako.

    ReplyDelete
  8. Zebedayo if you don't a point to contribute you better keep quite why provoke someone who needs to be assisted?

    Please moderator comments like these should not be torelated as they are irritating!
    For sure let this blog be for serious minded people.

    ReplyDelete
  9. WATU SIKU HIZI HUPENDA KUJA NA MADA ZAKUULIZA MICHUZI UWE UNAZIPOTEZEA KWANI GOOGLE SI IPO FACEBOOK IPO TWITTER IPO AULIZE AU ATAFUTE NAULI JAMAA SI ANAO AFUNGUE MACHO KAMA HAFUNGUI MACHO ASIKILIZE MASWALI KAMA HAYA NDIO YANALETA KASHFA ZA WATU WANAINGILIWA NA DINI ZAO KUTUKANWA MICHUZI UWE UNAPITIA SANA.

    ReplyDelete
  10. utamaduni ( culture) ni jinsi ya kuishi. Utamaduni unabadilika miaka inavyozidi kwenda kutokana na kuingiliana kwa mataifa wa rangi tofauti tofauti. Mfano, miaka 200 iliyopita waingereza waliwakuta kabila fulani linaitwa wahaya wakifua chuma. Walichukua utamaduni huo na hicho ndicho chanzo cha mapinduzi ya viwanda.( industrial Revolution). Wazungu hao walitukuta tukiwa hatuvai nguo sehemu kubwa ya miili yetu. Angalia sasa wamekopi utamaduni huo na leo tunawaona na kuwashangaa wazungu wanapotembea nusu uchi. Kama wao walikopi utamaduni wetu, na sisi siyo mgando tunalazimika kukopi utamaduni wao na kuufanya sehemu ya maisha yetu. Hoja nzuri Elle

    ReplyDelete
  11. utamaduni ( culture) ni jinsi ya kuishi. Utamaduni unabadilika miaka inavyozidi kwenda kutokana na kuingiliana kwa mataifa wa rangi tofauti tofauti. Mfano, miaka 200 iliyopita waingereza waliwakuta kabila fulani linaitwa wahaya wakifua chuma. Walichukua utamaduni huo na hicho ndicho chanzo cha mapinduzi ya viwanda.( industrial Revolution). Wazungu hao walitukuta tukiwa hatuvai nguo sehemu kubwa ya miili yetu. Angalia sasa wamekopi utamaduni huo na leo tunawaona na kuwashangaa wazungu wanapotembea nusu uchi. Kama wao walikopi utamaduni wetu, na sisi siyo mgando tunalazimika kukopi utamaduni wao na kuufanya sehemu ya maisha yetu. Hoja nzuri Elle

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...